Joyce Meyer Ministries KiSwahili

Joyce Meyer Ministries KiSwahili Kumshiriki Kristo - Kupenda Watu. Ukurasa rasmi wa Facebook wa Joyce Meyer Ministries Kiswahili Ahsante kwa msaada wako kwenye Joyce Meyer Ministries.

Ukurasa wa Facebook wa Joyce Meyer Ministries kwa lugha ya Kiswahili umetolewa kwa ajili ya marafiki wa Joyce Meyer Ministries na unasimamiwa na huduma hiyo. Shauku yetu ni kukutia moyo na kukupasha habari zinazohusiana na mambo yote yanayohusu Joyce Meyer Ministries katika lugha ya Kiswahili.Sisi k**a sehemu ya jamii, tunakaribisha maoni yako, mawazo yako na tunatazamia kwa hamu utupe maoni yako.Tafadhali kumbuka kuwa maoni yanaweza kupitiwa tena ili kuhakikisha kuwa kanuni zilizobainishwa kwenye Masharti ya Utoaji Huduma ya Facebook zimezingatiwa na kufuatwa. Kwa hivyo, maoni yote yatakayotolewa kwenye ukurasa huu yatafanyiwa uamuzi na wasimamizi wa ukurasa, ambao wana haki ya kuondoa maoni yoyote, vipachiko, au picha zozote wakati wowote na kutokana na sababu yoyote.Tunakuhimiza utoe maoni yako kwa uwazi na uaminifu na tunatumai kuwa kuhusika kwako katika jamii yetu ya Facebook kutaendelea kuwa kuzuri na kwa kufurahisha. Ikiwa ungependa kuongeza maoni au kupiga ripoti kuhusiana na vipachiko visivyofaa, tafadhali tuma barua pepe kwa: [email protected]. Kwa maombi na usaidizi wa marafiki na wabia wetu kote ulimwenguni, tunajitahidi kutoa ujumbe wa Kristo ulio na ubunifu na unaofaa pamoja na upendo wake kwa watu. Kwa usaidizi wako, tunaweza kutimiza lengo letu la kufikia kila taifa na kila mji, kila siku kwa Injili ya Yesu Kristo.

13/10/2026

Wale Wanaomngojea Bwana

'Yesu alisema ni afadhali Yeye aende ili Roho Mtakatifu apate kuja. Na sasa Roho Mtakatifu yuko pamoja na kila mmoja wet...
13/10/2026

'Yesu alisema ni afadhali Yeye aende ili Roho Mtakatifu apate kuja. Na sasa Roho Mtakatifu yuko pamoja na kila mmoja wetu, kila mahali, na wakati wote. Hukosi kamwe msaada, hukosi mwongozo, na huwi peke yako kamwe. Msaidizi yuko pamoja nawe leo... hapo hapo ulipo.

Je, umewahi kuhisi "umepandwa" mahali ambapo hutaki kuwepo? Labda Mungu amekuleta hapo kwa kusudi—ili uangaze nuru Yake ...
13/10/2026

Je, umewahi kuhisi "umepandwa" mahali ambapo hutaki kuwepo? Labda Mungu amekuleta hapo kwa kusudi—ili uangaze nuru Yake pale ambapo inahitajika zaidi. Stawi na uchanuke mahali ambapo Yeye amekupanda!

12/10/2026

Hupiti katika maisha peke yako—Mungu ni mwaminifu, naye hatakuacha kamwe bila msaada. Haijalishi unapitia nini, kumbuka hili: Unapendwa, wewe ni wake, na Yeye ana mpango mwema kwa ajili ya maisha yako. Usimruhusu mtu yeyote akushawishi uache kuamini ukweli huo. - Joyce

Je, unahitaji kutiwa moyo na nyenzo za Kikristo ili kukusaidia katika safari yako ya imani? Victor amebadilishwa milele ...
12/10/2026

Je, unahitaji kutiwa moyo na nyenzo za Kikristo ili kukusaidia katika safari yako ya imani? Victor amebadilishwa milele na mafundisho ya Joyce Meyer nawe unaweza pia! Zipate hapa: https://tv.joycemeyer.org/kiswahili

Ndiyo! Tunataka kukuombea. Asante kwa Esther kwa kushiriki ushuhuda huu mzuri wa nguvu ya maombi. Kwa nini usishiriki ma...
12/10/2026

Ndiyo! Tunataka kukuombea. Asante kwa Esther kwa kushiriki ushuhuda huu mzuri wa nguvu ya maombi.

Kwa nini usishiriki maombi yako hapa chini? Tunakupenda na tuko hapa kwa ajili yako!

Leo ni siku ambayo unaweza kuanza mchakato wa uponyaji katika maisha yako. Leo ni siku ambayo unaweza kuokolewa. Leo ni ...
11/10/2026

Leo ni siku ambayo unaweza kuanza mchakato wa uponyaji katika maisha yako. Leo ni siku ambayo unaweza kuokolewa. Leo ni siku ambayo unaweza kuguswa na Mungu. Leo ni siku ambayo unaweza kupata mabadiliko makubwa kabisa katika maisha yako. Sio lazima iwe kesho. Inaweza kuwa leo hii. Yesu si yule wa "Nitakuwa," bali Yeye ndiye "Mimi Niliye."

Zaburi 34:4–5, 8Nilimtafuta Bwana, naye akanijibu, akaniokoa na hofu zangu zote. Wao humtazama Yeye na kung'aa kwa furah...
11/10/2026

Zaburi 34:4–5, 8
Nilimtafuta Bwana, naye akanijibu, akaniokoa na hofu zangu zote. Wao humtazama Yeye na kung'aa kwa furaha, wala nyuso zao hazitaona aibu kamwe. Ee, onjeni mkaone ya kuwa Bwana ni mwema! Heri mtu yule anayemkimbilia Yeye!

Address

Cape Town

Opening Hours

Monday 09:00 - 17:00
Tuesday 09:00 - 17:00
Wednesday 09:00 - 17:00
Thursday 09:00 - 17:00
Friday 09:00 - 17:00

Telephone

+254 711 855 855

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Joyce Meyer Ministries KiSwahili posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to Joyce Meyer Ministries KiSwahili:

Shortcuts

Share