09/21/2021
We thank African Reflections Foundation for putting on this amazing project for the Kinene Village! We are so very happy to have been a part of this work and cannot wait to visit the rural school in 2022!
TAARIFA KWA UMMAπ
Dar es Salaam, 21/09/2021,
ARF kwa kushirikiana na SKY IS NOT LIMITED (New York), Build A Life Foundation (New York), Gullamhussein Elektra Charitable Trust na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya, Mkuranga, siku ya Jumatano ya Tarehe 29/9 tutazindua Shule ya Msingi Kinene inayopatikana Kata ya Mwarusembe, wilaya ya Mkurunga.
Ni furaha kwetu kufanikisha mradi huu ukiwa na lengo la kuboresha upatikanaji wa elimu bora katika Wilaya ya Mkuranga. Mafanikio ya mradi huu ni jitihada na upendo wa dhati kwa washirika wetu waliotoa mchango wao wa hali na mali.
Mradi huu wa Kinene, ni mradi wa kwanza ambao umetekelezwa na ARF kwa kujenge shule nzima. Tofauti na miradi mingine ya ukarabati au ujenzi wa madarasa tu.
Tunawashukuru wananchi wa Kijiji cha Kinene ambao awali ndio waliomba msaada kwaajili ya ujenzi wa shule ya Msingi Kinene. Kwa uchungu mkubwa watoto walikuwa wanatembea umbali mrefu katika kufuata shule ili kufikia elimu bora. Umbali mrefu uliopelekea watoto kuacha shule lakini pia kuwa katika mazingira hatarishi.
Shule ya Msingi Kinene inatarajia kuwanufaisha Watoto zaidi ya 300 kupata elimu bora katika miundombinu yenye ubora itakayokuza ustawi wa jamii nzima kwa ujumla.
Wasiliana nasi kupitia barua pepe inayopatikana katika tovuti yetu. (Ipo katika Bio) ili kuweza kushirikiana nasi katika kusaidia miradi kwa maendeleo endelevu.
Ahsante sana π