Umoja wa Mataifa

Umoja wa Mataifa Akaunti rasmi ya Umoja wa Mataifa. Kwa amani, utu & usawa katika ulimwengu wenye ustawi.

Sote tuna jukumu la kukomesha uenezaji wa taarifa za uongo mtandaoni, ambazo zinaweza kuwa na athari mbaya katika maisha...
08/28/2026

Sote tuna jukumu la kukomesha uenezaji wa taarifa za uongo mtandaoni, ambazo zinaweza kuwa na athari mbaya katika maisha.

Kabla ya kusambaza taarifa, tafakari:

Ni NANI aliyeiandaa?
NINI asili yake?
ilitoka WAPI?
KWA NINI unasambaza?
Ilichapishwa LINI?

Afrika ina uwezo mkubwa wa nishati ya jua kuliko sehemu nyingine yoyote duniani, lakini bado inapokea sehemu ndogo sana ...
08/26/2026

Afrika ina uwezo mkubwa wa nishati ya jua kuliko sehemu nyingine yoyote duniani, lakini bado inapokea sehemu ndogo sana ya uwekezaji wa nishati safi.

Haki ya tabianchi haiwezekani bila Afrika kuwa sehemu ya msingi ya suluhisho.

Amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres.

Wahudumu wa misaada ya kibinadamu wanahatarisha maisha yao kila siku ili kuwafikia watu wanaohitaji msaada wa dharura.Ha...
08/24/2026

Wahudumu wa misaada ya kibinadamu wanahatarisha maisha yao kila siku ili kuwafikia watu wanaohitaji msaada wa dharura.

Hata vita vina sheria.

Chini ya sheria ya kimataifa, wahudumu wa misaada, misafara ya kibinadamu na raia lazima walindwe.

📸: Gari la Umoja wa Mataifa liliharibiwa vibaya baada ya kushambuliwa mara mbili na droni wakati ikipeleka misaada kwa raia katika eneo la Ostriv, Kherson nchini Ukraine, moja ya maeneo yaliyoathirika zaidi na vita.

- United Nations OCHA

"Haki za binadamu zinafanya kazi, hata pale zisipopewa vichwa vya habari."Akizungumza mbele ya Baraza la Haki za Binadam...
08/19/2026

"Haki za binadamu zinafanya kazi, hata pale zisipopewa vichwa vya habari."

Akizungumza mbele ya Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa mjini Geneva, Mkuu wa United Nations Human Rights Volker Türk alisema haki za binadamu zinaendelea kubadilisha maisha, kupunguza migawanyiko na kupanua uhuru wa watu duniani.

Hata hivyo, alionya kuhusu "changamoto kubwa za haki za binadamu" na "mashambulizi yasiyo na aibu dhidi ya sheria za kimataifa" yanayosababisha mateso makubwa ya kibinadamu.

"Ni lazima tuyakemee kila wakati na kila mahali, na tufanye kazi ya kuyadhibiti na kuyakomesha."

Leo tunamkumbuka Kofi Annan, Katibu Mkuu wa 7 wa Umoja wa Mataifa, ambaye aliongoza kwa hekima na kuamini katika nguvu y...
08/18/2026

Leo tunamkumbuka Kofi Annan, Katibu Mkuu wa 7 wa Umoja wa Mataifa, ambaye aliongoza kwa hekima na kuamini katika nguvu ya mazungumzo.

"Tunaweza kupenda tulivyo bila kuwachukia wale walio tofauti nasi."

Katika wakati ambapo tofauti mara nyingi hutugawa, maneno yake yanaendelea kutukumbusha kuwa heshima, kuvumiliana na kuelewana ndiyo msingi wa amani.

Katika vita, raia ndio hulipa gharama kubwa zaidi.Lakini hata vita vina sheria.Raia lazima walindwe, wakati wote, kila m...
08/16/2026

Katika vita, raia ndio hulipa gharama kubwa zaidi.

Lakini hata vita vina sheria.

Raia lazima walindwe, wakati wote, kila mahali.

Kamwe hawapaswi kulengwa.

- kupitia United Nations OCHA

Duniani kuna Watu wa Asili milioni 476:- Wanaishi katika nchi 90- Wanawakilisha tamaduni 5,000-Wanazungumza lugha nyingi...
08/11/2026

Duniani kuna Watu wa Asili milioni 476:

- Wanaishi katika nchi 90
- Wanawakilisha tamaduni 5,000
-Wanazungumza lugha nyingi kati ya lugha 7,000 zinazozungumzwa duniani.

Umoja wa Mataifa unaendelea kuhimiza na kulinda haki za Watu wa Asili duniani kote.

Fahamu zaidi: un.org/en/observances/indigenous-day

Wafanyakazi wa misaada mara nyingi wanahitaji uwezo wa kufika katika maeneo ya mbali na yenye changamoto nyingi duniani....
08/09/2026

Wafanyakazi wa misaada mara nyingi wanahitaji uwezo wa kufika katika maeneo ya mbali na yenye changamoto nyingi duniani.

Shukrani kwa Shirika la Umoja wa Mataifa la Huduma ya Anga ya Kibinadamu, inayoongozwa na Mpango wa Chakula Duniani, wanaweza kuleta usaidizi muhimu kwa jamii zilizojitenga.

www1.wfp.org/unhas

World Food Programme

Address

New York, NY
10017

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Umoja wa Mataifa posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share