Tanzania Houston Community - THC

Tanzania Houston Community - THC THC official Blog

Tanzania Houston Community (THC) Leaders with UTT AMIS Representatives
08/10/2026

Tanzania Houston Community (THC) Leaders with UTT AMIS Representatives

🇹🇿 TANZANIA HOUSTON COMMUNITY (THC) 🇹🇿OFFICIAL STATEMENT – SHUKRANI KWA UTT-AMISUongozi wa Tanzania Houston Community (T...
08/09/2026

🇹🇿 TANZANIA HOUSTON COMMUNITY (THC) 🇹🇿

OFFICIAL STATEMENT – SHUKRANI KWA UTT-AMIS

Uongozi wa Tanzania Houston Community (THC), kwa niaba ya wanajumuiya, wazazi na watoto wote walioshiriki katika shughuli yetu ya BACK2SCHOOL 2026, unapenda kutoa shukrani za dhati kwa UTT-AMIS kwa kuwa mdhamini na mshirika muhimu katika kufanikisha shughuli hii.

Kupitia udhamini na msaada wa UTT-AMIS, tulifanikiwa kugawa school supplies kwa zaidi ya wanafunzi 250, ikiwa ni sehemu ya juhudi zetu za kuwaandaa watoto wetu kwa mwaka mpya wa masomo na kuwapa moyo wa kuendelea kufanya vizuri katika elimu.

Mchango huu haukuwa tu msaada wa vifaa vya shule, bali ulikuwa ni uwekezaji katika elimu, ndoto na mustakabali wa watoto wetu.

THC inathamini sana moyo wa UTT-AMIS wa kurudisha kwa jamii na kushirikiana nasi katika shughuli zenye kuleta maendeleo na mshikamano ndani ya jamii yetu.

Kwa wazazi, watoto, volunteers, viongozi na wanajumuiya wote waliojitokeza na kufanikisha BACK2SCHOOL 2026, tunasema ASANTENI SANA!

Na kwa namna ya pekee:

THANK YOU UTT-AMIS FOR SUPPORTING OUR CHILDREN AND OUR COMMUNITY! ❤️🇹🇿

Tunatarajia kuendelea kushirikiana katika shughuli nyingine zijazo kwa manufaa ya jamii yetu.

Pamoja Tunaweza. Pamoja Tunajenga Jamii Yetu.

Kwa heshima,

UONGOZI THC

07/02/2026
Happy Father's Day
06/21/2026

Happy Father's Day

Address

Houston, TX

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Tanzania Houston Community - THC posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to Tanzania Houston Community - THC:

Shortcuts

Share