23/02/2025
Siku ya Jumamosi 22/02/2025 Mwenyekiti wa the Green Environmental Organization (GEO) - Go Green Ndg.Ahmedi Haji Mkema ameshiriki katika mahafali ya kwanza ya wahitimu wa mafunzo ya huduma ya kwanza ya msingi na mafunzo ya ngazi ya juu yaliyofanyika ofisi za Tanzania Red Cross Society Tunguu Zanzibar.
Mgeni rasmi aliyehudhuria mahafali hayo ni Mkuu wa Skuli ya Sheria Zanzibar Dkt.Ali Ahmed Uki akimuwakilisha Waziri wa Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala bora Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Ilikuwa ni jambo jema la faraja kwani mafunzo hayo yana manufaa katika kukabiliana na maafa mbalimbali.