Zanzibar Maisha Bora Foundation

Zanzibar Maisha Bora Foundation Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Zanzibar Maisha Bora Foundation, Nonprofit Organization, Migombani, Zanzibar.

Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF), founded in 2021 by the First Lady of Zanzibar, is dedicated to improving the quality of life for women, youth, and children across Zanzibar.

03/06/2026
Leo tumefanikisha zoezi la ugawaji wa mifuko ya pedi kwa wanafunzi 360 wa k**e wa Kidato cha Nne katika Skuli ya Sekonda...
03/06/2026

Leo tumefanikisha zoezi la ugawaji wa mifuko ya pedi kwa wanafunzi 360 wa k**e wa Kidato cha Nne katika Skuli ya Sekondari Kidoti, iliyopo Wilaya ya Kaskazini A, Mkoa wa Kaskazini.

Lengo la ugawaji huo ni kusaidia kukabiliana na changamoto ya upatikanaji wa hedhi salama kwa wanafunzi wa k**e, ili isiwe sababu ya wanafunzi hao kukosa siku za masomo, jambo ambalo linaweza kuathiri mahudhurio yao shuleni, ushiriki darasani na hatimaye ufaulu wao wa kitaaluma kushuka.

Sambamba na ugawaji huo, wanafunzi walipatiwa elimu kuhusu hedhi salama hedhi pamoja na ukatili wa kijinsia, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuwawezesha wasichana kufanya maamuzi sahihi kuhusu afya, ustawi na maendeleo yao kwa ujumla.

Kupitia mpango huu, ZMBF inaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wa elimu na maendeleo kuhakikisha wasichana wanapata fursa sawa ya kujifunza katika mazingira salama, yenye staha na yanayowawezesha kufikia ndoto zao na kuchangia kikamilifu katika maendeleo ya jamii na taifa.

A healthy future starts with menstrual dignity.Let’s create a world where no girl misses opportunities because of her pe...
28/05/2026

A healthy future starts with menstrual dignity.

Let’s create a world where no girl misses opportunities because of her period.

Mapema wiki hii ZMBF imeshiriki katika kikao muhimu cha wadau wa sekta ya mwani Zanzibar. Kikao cha Zanzibar Seaweed Mul...
23/05/2026

Mapema wiki hii ZMBF imeshiriki katika kikao muhimu cha wadau wa sekta ya mwani Zanzibar. Kikao cha Zanzibar Seaweed Multi-Stakeholder Action Group (ZSMAG) kiliandaliwa na Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi, na kuongozwa na Naibu Katibu Mkuu, Ndg. Zahour Kassim Al-Kharous.

ZMBF iliwakilishwa na Mtaalamu wa Kilimo cha Mwani, Bi. Joice Denis.

Kikao hicho kilikuwa ni muendelezo wa vikao vya kila robo mwaka, ambapo wadau mbalimbali hukutana na kujadili maendeleo ya sekta ya mwani, kuimarisha ushirikiano na kutafuta fursa mpya za kukuza Uchumi wa Buluu wa Zanzibar.

Kupitia mradi wa Joint Programme on Rural Women’s Economic Empowerment tunaoutekeleza kwa kushirikiana na International ...
21/05/2026

Kupitia mradi wa Joint Programme on Rural Women’s Economic Empowerment tunaoutekeleza kwa kushirikiana na International Fund for Agricultural Development, tunaendelea kutoa mafunzo ya uongezaji thamani wa mwani kwa wanawake kutoka shehia 7 za Wilaya za Kusini na Kati Unguja.

Kupitia mafunzo hayo, wanawake 78 kutoka vikundi 39 wamejengewa uwezo kupitia mafunzo ya nadharia na vitendo katika maeneo mbalimbali ikiwemo uongezaji thamani wa mwani, utengenezaji wa mbolea, unga lishe wa mwani, scrub, faida na matumizi ya mwani, masoko na ujasiriamali, pamoja na afya na usalama wakati wa uchakataji.

Kwa upande wa vitendo, washiriki wamepata fursa ya kutengeneza bidhaa mbalimbali zinazotokana na mwani ikiwemo sabuni, lotion, cream, vidonge vya mwani, pamoja na mafuta ya nywele na mwili.

Mafunzo haya yanalenga kukabiliana na changamoto ya utegemezi wa soko moja la mwani ghafi, bei ndogo ya mazao, pamoja na ukosefu wa ujuzi wa kuongeza thamani ya zao hilo — hali inayosababisha wakulima wengi, hususan wanawake, kuendelea kupata kipato kidogo licha ya kazi kubwa wanayoifanya.

Kupitia ujuzi huu, wanawake wanafunguliwa fursa za kujenga biashara endelevu, kuongeza kipato, na kuimarisha mchango wao katika Uchumi wa Buluu Zanzibar.

   with .repost・・・Ahead of the 79th World Health Assembly in Geneva, Commonwealth Health Ministers and officials will co...
17/05/2026

with .repost
・・・
Ahead of the 79th World Health Assembly in Geneva, Commonwealth Health Ministers and officials will convene to discuss the future of cancer care.

Cervical cancer is at the heart of that conversation.

The Commonwealth accounts for 40% of new cervical cancer cases and 43% of global deaths, despite representing just 30% of the world’s population. By 2030, cases are projected to rise by 55% – the equivalent of one woman dying every three minutes.

Across the Commonwealth, First Ladies and Spouses of Heads of Government are emerging as champions of change in the fight against cervical cancer.

👉 Swipe to see how they are leading national efforts to drive progress and save lives.

|

Leo, Zanzibar Maisha Bora Foundation tumepokea ujumbe kutoka Singapore katika ziara ya kazi iliyolenga kujifunza kwa kin...
13/05/2026

Leo, Zanzibar Maisha Bora Foundation tumepokea ujumbe kutoka Singapore katika ziara ya kazi iliyolenga kujifunza kwa kina kuhusu miradi na programu mbalimbali zinazotekelezwa na taasisi yetu.

Ujumbe huo ulipata fursa ya kujionea moja kwa moja utekelezaji wa programu za uwezeshaji wa wanawake na vijana katika sekta ya mwani, afya, pamoja na maendeleo ya jamii. Hadi sasa, taasisi imefikia wanufaika zaidi ya 250,000 kupitia afua mbalimbali zinazolenga kuboresha maisha ya jamii.

Ziara hiyo imeendelea kufungua fursa za ushirikiano, kubadilishana uzoefu, na kuonesha mchango wa programu mbalimbali katika kuimarisha maendeleo jumuishi ya jamii ya Zanzibar.

Kupitia mradi wa Mpango wa Pamoja wa Uwezeshaji wa Kiuchumi kwa Wanawake wa Vijijini (JP-RWEE), wanawake 78 kutoka Mkoa ...
11/05/2026

Kupitia mradi wa Mpango wa Pamoja wa Uwezeshaji wa Kiuchumi kwa Wanawake wa Vijijini (JP-RWEE), wanawake 78 kutoka Mkoa wa Kusini wamepatiwa mafunzo ya biashara na uongezaji thamani wa zao la mwani.

Kupitia mafunzo hayo ya siku tano, vikundi 39 vya ushirika viliwakilishwa na wanawake hao ambao wamejengewa uwezo wa kugeuza mwani kuwa bidhaa zenye thamani, pamoja na kujifunza kuhusu uthibitishaji na uimarishaji wa bidhaa k**a sabuni, mafuta na bidhaa nyingine kupitia ushirikiano na Shear Illusions Industries, mfanyabiashara mkubwa wa bidhaa za urembo.

Moja ya changamoto kubwa inayoikabili sekta ya mwani ni ukosefu wa soko la uhakika, hali inayosababisha hasara kubwa pale wanunuzi wanaposhindwa kujitokeza kununua mwani. Hali hii huathiri moja kwa moja wanawake wengi wanaotegemea zao hili kukidhi mahitaji muhimu ya kila siku ya familia zao.

Mafunzo haya yanafungua fursa za kipato endelevu, kukuza ujasiriamali wa wanawake, na kuimarisha mchango wao katika Uchumi wa Buluu Zanzibar pamoja na pato la taifa.

Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF) inaungana na wananchi wa Zanzibar, Watanzania wote pamoja na jumuiya ya kimataifa...
10/05/2026

Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF) inaungana na wananchi wa Zanzibar, Watanzania wote pamoja na jumuiya ya kimataifa kuadhimisha Siku ya Mama Duniani, leo tarehe 10 Mei 2026.

Siku hii ni fursa ya kutambua mchango mkubwa wa mama katika malezi ya familia na maendeleo ya jamii. ZMBF inaendelea kuamini kuwa kumwezesha mama ni kuijenga familia na jamii yenye ustawi zaidi.

ZMBF inawatakia kina mama wote Heri ya Siku ya Mama Duniani.

Address

Migombani
Zanzibar

Opening Hours

Monday 08:00 - 16:00
Tuesday 08:00 - 16:00
Wednesday 08:00 - 16:00
Thursday 08:00 - 16:00
Friday 08:00 - 16:00

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Zanzibar Maisha Bora Foundation posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to Zanzibar Maisha Bora Foundation:

Share