22/03/2025
Siku ya Alhamis 20/3/2025 Baraza la Vijana Mkoa Mjini Magharibi limefanya Ziara ya kimasomo katika Dawati la Jinsia na Watoto la Jeshi la Polisi Zanzibar kujifunza kuhusu maswala ya Uzalilishaji. Katika Mafunzo hayo jumla ya Wanachama 32 na Viongozi 2 wa Baraza la Vijana Mjini Magharibi wakiwemo Wanaume 11 na Wanawake 23 wamepatiwa Elimu hio.
Jeshi la Polisi Zanzibar limefurahishwa sana na ujio wa Wanachama hao wa Red Cross kwenda kujifunza Masomo hayo na pia limewataka Vijana hao waliopatiwa Elimu hio kuwa Mabalozi kwa weƱgine na kutoa Mashirikiano pindi wakigundua ishara za Udhalilishaji katika jamii
Akiongea kwa niaba ya Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Mjini Magharibi, Mjumbe wa Tamasha na Michezo kwa upande wa Red Cross amewashukuru Maafisa hao kwa juhudi kubwa wanazochukuwa kutoa Elimu kwa makundi tofauti na kuahid kuwa watukuwa mabalozi wazuri katika jamii na sehemu wanazofanyia kazi, kuimarisha mashirikiano baina ya red cross na Jeshi la Polisi