Himaya ya wana Qurashiyyah

Himaya ya wana Qurashiyyah to educate ummah from locally to globally "YUKHRIJUNNAS MINADDHHULUMATI ILA NOUR"

25/02/2019

Je tushajiandaa siku ya kufufuliwa

08/02/2019

NA HIZI NDIZO FADHILA ZA QUR'AAN...
➡️ Watu wa Qur'aan ni watu bora kwa Allaah سبحانه وتعالى.
➡️ Mwenye kuhifadhi Qur'aan Hutangulia Kaburini kwa ajili ya mwanga anaojaaliwa nao.
➡️ Mtu bora kabisa ni Mwenye kuisoma na akaifundisha.
➡️ Mwenye kuhifadhi Qur'aan huvalishwa Taji Siku ya Qiyama.
➡️ Qur'aan Humnyanyua mtu na humdhalilisha mwengine.
Imetoka kwa 'Umar رضي الله عنه kwamba Mtume صلى الله عليه وسلم amesema :
" Mtume wenu amesema ; Allaah Atawanyanyua baadhi ya watu kwa kitabu hiki, na Atawadhalilisha wengine kwa kitabu hiki. (Qur'aan)"
( Muslim )
➡️ Thawabu mara mbili kwa mwenye kuisoma kwa mashaka.
Imetoka kwa 'Aisha رضي الله عنها Kwamba Mtume صلى الله عليه وسلم amesema :
" Yule aliyekuwa hodari wa kusoma Qur'aan atakuwa pamoja na Malaika Waandishi wa Allaah watukufu Wacha Mungu, na yule ambaye anaisoma Qur'aan kwa mashaka na huku anajitahidi kwa kudodosa atapata ujira mara mbili ".
{ Al-Bukhariy na Muslim }
➡️ Kiombezi siku ya Qiyama.
Imetoka kwa Abuu Umaamah رضي الله عنه kwamba Mtume صلى الله عليه وسلم amesema ;
" Someni Qur'aan kwani itakuja Siku ya Qiyama ikimuombea mwenye kuisoma "
( Muslim )
➡️ Qur'aan humpandisha mtu daraja ya Pepo.
➡️ Kuteremka Malaika wa utulivu na Rahmah kwa wanaosoma Qur'aan.
➡️ Thawabu kwa kila herufi moja.
Ya ALLAH Tujaalie tuwe wenye kuisoma na kuiandama

04/02/2019

Jitibu kwa majina ya Allah

بسم الله الرحمن الرحيم

Kwa Jina La Mwenyezi Mungu Mwingi Wa Rehema Mwenye Kurehemu

Mwenyezi Mungu anasema katika Quran Tukufu;

وَلِلَّهِ الأَسْمَاءُ الْحُسْنَى فَادْعُوهُ بِهَا وَذَرُوا الَّذِينَ يُلْحِدُونَ فِي أَسْمَائِهِ…

Maana yake, “Na Mwenyezi Mungu ana majina mazuri mazuri; muombeni kwayo. Na waache wale wanaoharibu utakatifu wa majina Yake…”

Baada ya utafiti wa miaka 3, Dokta Ibrahim Karim (ambaye ni mwanzishi wa elimu ya Biogemitry) amegundua kwamba majina mazuri ya Mwenyezi Mungu yana nguvu ya kuponya idadi kubwa ya maradhi na kwa njia ya sahihi kwa tofauti ya kipimo cha nguvu ndani ya mwili wa mtu. Na amegundua kwamba kila jina mojawapo ya majina mazuri ya Mola ipo nguvu inayochochea immune system kufanya kazi kwa uwezo mkubwa katika kiungo kimojawapo cha mtu. Na aliweza dokta Ibrahimu kutumia kanuni ya sauti kugundua kwa kutaja tu jina mojawapo ya majina mazuri ya Mola inapelekea kuendeleza vizuri njia za nguvu muhimu ndani ya mwili wa mtu.

Ameashiria Dokta Ibrahim kwamba hakika yeye ni mtu wa kwanza kufanyiwa uchunguzi ambapo amejitibu macho yake kutokana na maambukizo, na kuishia kutaja majina ya Mola Annuur, Al-Baswiir na Al-Wahhaab (النور والبصير والوهاب). Na kwa muda wa dakika 10 amepata shifaa na kuondokewa na wekundu wa macho. Na ameendelea kusema kwamba majina hayo hayo matukufu ya Mola yanatumika kwa ajili ya kujikinga pia. Na imegunduliwa kwamba nguvu ya shifaa inaongezeka/inazidi ukisoma aya za shifaa baada ya kutaja majina mazuri ya Mola. Hizi aya za shifaa:

وننزل من القرآن ما هو شفاء ورحمة للمؤمنين ولا يزيد الظالمين إلا خسارا

Maana yake, "Na tunateremsha katika Qur'ani yaliyo ni matibabu na rehema kwa Waumini. Wala hayawazidishii madhaalimu ila khasara."

ياأيها الناس قد جاءتكم موعظة من ربكم وشفاء لما في الصدور وهدى ورحمة للمؤمنين

Maana yake, "Enyi watu! Yamekujieni mawaidha kutoka kwa Mola wenu Mlezi, na poza kuponyesha yaliyomo vifuani, na uwongofu, na rehema kwa Waumini."

وإذا مرضت فهو يشفين

Maana yake, Na ninapo ugua ni Yeye ndiye anaye niponesha.

Njia ya kujitubu: Weka mkono wako wa kuume mahali unapohisi maumivu kisha taja jina/majina la/ya Mola kwa kurudia rudia mpaka utakapohisi nafuu kwa idhini ya Mola.

Hapa chini ni uchunguzi wake aliofikia k**a ifuatavyo:

1 - Maradhi ya sikio الأذن
السمـــــــــيع
(Taja jina la Mola ASSAMII`I)

2 - Maradhi ya mfupa العظـــــــــام
النـــــــــــــــافع
(Taja jina la Mola ANNAAFA`U)

3 - Maradhi ya uti wa mgongo العمود الفقري
الجبـــــــــــــار
(Taja jina la Mola ALJABAAR)

4 - Maradhi ya goti الركبــــــــة
الــــــــــــرؤوف
(Taja jina la Mola ARAUUF)

5 - Maradhi ya nywele الشعـــر
البديــــــــــــــع
(Taja jina la Mola ALBADIIU)

6 - Maradhi ya moyo القـــــــــــلب
النــــــــــــــــور
(Taja jina la Mola ALNUUR)

7 - Maradhi ya misuli العضلات
القـــــــــــــــوي
(Taja jina la Mola ALQAWII)

8 - Maradhi ya mshipa wa moyo أوردة القلب
الوهـــــــــــاب
(Taja jina la Mola ALWAHAAB)

9 - Maradhi ya myocardial عضلة القلب
الـــــــــــــرزاق
(Taja jina la Mola A'RAZAAQ)

10 - Maradhi ya mishipa الأعصــاب
المغنـــــــــــى
(Taja jina la Mola ALMUGHNIY)

11 - Maradhi ya mshipa mkubwa wa damu الشريــــــان
الجبــــــــــــــــار
(Taja jina la Mola ALJABAAR)

12 - Maradhi ya tumbo المعــــــــــده
الــــــــــرزاق
(Taja jina la Mola A'RAZAAQ)

13 - Maradhi ya kensa السرطـــــان
جل جلالــــــــــه
(Taja jina la Mola JALA JALALUH)

14 - Maradhi ya thyroid الغدة الدرقية
الجبــــــــــــار
(Taja jina la Mola ALJABAAR)

15 - Maradhi ya paja الفخــــــــــذ
الــــــــــــرافع
(Taja jina la Mola ALRAAFA'A)

16 - Maradhi ya kuumwa nusu kichwa الصداع النصفي
الغنــــــــــــي
(Taja jina la Mola ALGHANIY)

17 - Maradhi ya mishipa ya jicho الشرايين بالعين
المتعـــــــــــال
(Taja jina la Mola ALMUTA'AL)

18 - Maradhi ya figo الكـــــــــــلى
الحـــــــــــــي
(Taja jina la Mola ALHAY)

19 - Maradhi ya colon القـــولـــون
الـــــــــــــرؤوف
(Taja jina la Mola ALRAU'UF)

20 - Maradhi ya utumbo الأمعــــــــاء
الــــــــــــرزاق
(Taja jina la Mola ALRAZAAQ)

21 - Maradhi ya ini الكبـــــــــــد
النافـــــــــــــــــع
(Taja jina la Mola A'NAAFA'A)

22 - Maradhi ya pancreas البنكريـــــاس
البــــــــــــارئ
(Taja jina la Mola ALBAARI'Y)

23 - Maradhi ya fat bags اكياس دهنية
النافـــــــــــــــــع
(Taja jina la Mola A'NAAFA'A)

24 - Maradhi ya kizazi الرحــــــــم
الخالــــــــــــق
(Taja jina la Mola ALKHAALIQ)

25 - Maradhi ya kibofu المثانــــــــه
الهـــــــــــــــادي
(Taja jina la Mola ALHAADIY)

26 - Maradhi ya arthritis الروماتيزم
المهيـمــــــــن
(Taja jina la Mola ALMUHAY'MIN)

27 - Maradhi ya prostate البروستاتـــة
الرشيــــــــــــــد
(Taja jina la Mola ARASHEED)

28 - Maradhi ya backbone of the eye. عصب العين
الظاهـــــــــــر
(Taja jina la Mola ADHAAHER)

29 - Maradhi ya pineal gland. الغدة الصنوبرية
الهــــــــــــــادي
(Taja jina la Mola ALHAADI)

30 - Maradhi ya blood pressure. ضغط الدم
الخافـــــــــض
(Taja jina la Mola ALKHAAFEDH)

31 - Maradhi ya pafu. الرئـــــــــــة
الــــــــــــــرزاق
(Taja jina la Mola ARAZAAQ)

32 - Maradhi ya gland lemusip. الغدة الثيموسية
القـــــــــــــوي
(Taja jina la Mola ALQAWI)

33 - Maradhi ya gland juu ya figo الغدة فوق الكلوية
البــــــــــــــــارئ
(Taja jina la Mola ALBAARI'Y)

34 - Maradhi ya mba. قشر الشعر
جل جلالــــــــــــه
(Taja jina la Mola JALA JALALUH)

35-Maradhi ya sinuses. الجيوب الأنفية
اللطيف – الغني - الرحيم
(Taja MAjina ya Mola ALATIIF - ALGHANIY - ARAHIIM)

36-Maradhi ya jicho. العين
النور – البصير – الوهاب
(Taja MAjina ya Mola ALNUUR - ALBASIIR - ALWAHAAB

04/02/2019

Wajue Mitume wako na umri walioishi duniani:
1-ADAM (930)
2-IDRIS (356)
4-NUOH (950)
5-HOUD (265)
6-SWALEKH (586)
7-LUTT (155)
8-IBRAHIM (195)
9-ISMAIL (137)
10-IS-GHAQA (120)
11-YAAKOUB (136)
12-ELYASAW (109)
13-YUSSOUF (110)
14-SHUAIB (882)
15-MUSSA (125)
16-HAROUN (119)
17-DAUWD (149)
18-SULEIMAN (150)
19-AYOUB (146)
20-ZULKIFLIY (43)
21-YUNUOS (51)
22-ZAKARIA (207)
23-YAHYA (95)
24-ISSA (40)
25-MUHAMMAD (63)
Wape na wenzako Elimu hii wanufaike. Yani ukipuuza hii nitakuona mtu waajabu kweli, wakati msg za kipuuzi unakuwa wa kwanza kushare

27/01/2019

🔻NINI HUKMU YA ANAASHIDI NA QASWIDA⏬
----------------------------------------------------------
Swali:
Ni ipi hukumu ya anashidi pia naomba kujua tofauti katika anashidi na qaswaida
🎩JAWABU✅:
الحمد لله رب العالمين والصلاة والسلام على أشرف الأنبياء وإمام المرسلين
وبعد.
Katika mambo ambayo tunamshukuru ALLAAH kwa uwazi wa hukumu yake katika Shari’ah yetu ya Kiislamu na fatawa za Wanazuoni wetu waliosoma wakabobea katika ‘Ulamaa wa Ahlus-Sunnah wal-jamaa (ALLAAH Awarehemu waliotangulia na kuwahifadhi waliobakia) Ni hili suala ambalo fitna yake imekithiri sana katika jamii ya Kiislam. Wakazeeka juu yake vijana, na kukongorojoka juu yake wazee, Ila wachache katika waliorehemewa na ALLAAH.
Ila -walillaah al-hamd- Wanazuoni wamelitolea kauli nyingi zinazokurubia kuwa ni Ijmaa k**a hazijakuwa ni ijmaa.
Ntataja hapa baadhi ya kauli za baadhi yao, Na kukhitimisha kwa kauli nzito ya Baqiyyatus-Salaf (Al-Imaam Swaaleh Al-Fawzaan -ALLAAH Amhifadhi).
1⃣. Al-Imaam Al-Albaaniy (Allaah Amraham!):
Yeye hakulikubali jambo hilo la anaashiid bali amelipiga vita na kutoa tamko la kutofaa kwake.
Na miongoni mwa hoja zake juu ya hilo alisema:
“Ni vyema kujenga hoja juu ya hilo kwa mambo mawili:
1. Kwamba hizi anaashiid hazikuwa katika uongofu wa Wema wetu waliotutangulia (Radhi za ALLAAH ziwe juu yao!).
2. Hali halisi inayoshuhudiwa na kujulikana ni ya khatari pia.
Na hilo ni kwasababu tumeanza kuona kwa baadhi ya vijana wa Kiislam wanapumbazika kwa hizi anaashiidi za kidini. Na huwa wanazighanni daima. Jambo ambalo limepelekea wengi wao waache kujishughulisha na kisomo cha Qur’an na kumdhukuru ALLAAH na kumswalia Mtume (swalla LLAAHU ‘alayhi wasallam) na kusikiliza mawaidha…” .
“👈🏼البيان المفيد عن حكم التمثيل والأناشيد📚📚”.
2⃣. Al-Imaam Al-‘Uthaymiin (ALLAAH Amrehem) Anasema:
“Anaashiid ziitwazo za Kiislamu ni Anaashiid za Kizushi (za kibidaa), zinafanana na zilizozuliwa na Masufi. Na kwa hali hiyo inapasa watu waachane nazo na waelekeze jitihada zao kwenye mawaidha ya Kitabu na Sunnah.
Ama ikiwa ni tungo ambazo zitatumika kwenye vita kusaidia kupandisha mori katika Jihadi ni jambo zuri”.
3⃣. Imaam Ahmad shaakir katika kitabu chake ummda tafsir: aliulizwa ni ipi hukmu ya anaashiid za kidini?
Akajibu: Hizi zote ni katika mambo ya bidaa yenye kuchukiza, hayamzidishii mfanyaji ispokuwa anakuwa mbali (yanamuweka mbali muimbaji na msikilizaji na kheri),
Muulizaji akasema: laakin Allah anasema "nikumbukeni nami nitakukumbeni" na hawa wanaoimba wanamtaja Allah hasa hasa katika wakat wa mwisho wa usiku (wale waimbaji wa usiku).
Shekh akasema: jee mimi nimeipinga hiyo aya? Wao wanamtaja Allah kwa maasia naye Allah anawakumbuka kwa kuwachukia,
Wao pia wanamtaja Allah kwa njia ya bidaa nayeye Allah anawakumbuka kwakuwachukia".
4⃣. Imam Ahmad aliulizwa: Unawazungumziaje watu wanaoimbaimba?
Akasema: Wanachokifanya ni bidaa na haifai kukaa nawatu wanamna hiyo".
5⃣Imaam Shaafiy anasema: "nimeacha katika mji wa baghadaad (iraqi) kitu ambacho azanaadiqa (kundi miongon mwa wanaafiq) wameanzisha (wamekizusha) wanakiita anashid wanataka kuwazuia watu na quraan".
👉🏽Anaashid zinawazuia watu na kusikiliza quran kupata uhuzin na majonzi, wangap katika waislam wanaposikiliza baadhi ya anaashiid wanatokwa na machozi na wanakaribia kulia?
Wangap katika wapenz wa anashid kwenye sim zao wamedownload ma anashiid kuliko quran na mawaidha? Wangap?
Angalia watoto, wanawake na wanaume ambao majumba yao mara kwa mara wamezoea kuweka maanaashiid na maqaswida, angalia walivyohifadh kichwani mwao, ni manyimbo tu
Imefikia mtu huyo ukimuwekea quran anakwambia zima, zima, anajiskia vibaya
Mtu akisikiliza quran ahisi km ina mchoma choma nakuwatia kizungu zungu, laakin akisiliza anaashid moyo wake unaburudiika na anajisikia raaha kabisa. Subhaana Allah. Jee hizi sio athari za anaashidi
6⃣. Al-‘Allaamah Al-Fawzaan (ALLAAH Amhifadhi) Anasema:
“Na miongoni mwa yanayohitaji uzinduzi juu yake ni yale mambo yaliyoenea kwa wengi miongoni mwa vijana wa Dini kuhusu kanda ambazo zina sauti za watu waimbao kwa pamoja Wanaziita kanda za anaashiid za Kiislamu, na kwa uhakika ni miongoni mwa nyimbo tu. Na huenda zikawa na sauti za kufitini (kabisa). Na huuzwa kwenye maduka ya studio pamoja na kanda za Qur’aan na mihadhara ya Kidini.
Na kuziita hizi nashidi kuwa ni anaashiid Islaamiyyah ni jina la kimakosa (kabisa!), Kwa sababu Uislamu haujatuwekea anaashiid, bali umetuwekea Dhikrillaah na Kisomo cha Qur’aaan na Ilmu yenye manufaa. Ama anaashiid (ziitwazo) Islaamiyyah, hizo ni katika Dini za Masufi wazushi. Ambao wameijaalia Dini yao kuwa ni mambo ya kipuuzi puuzi na mchezo mchezo. Na kuzifanya anaashiid kuwa ni sehemu ya Dini, ni kujishabihisha na manaswara WAKRISTO….”
“👉🏽AL-KHUTWAB AL-MIMBARIYYAH 3/-184-185📓📓”
Ama qaswiidah:
Ni mkusanyiko wa beti za kishairi ambazo zimeafikiana kwa wizani na vina.
Na tofauti ambayo ipo ni kuwa qaswidah inaweza kusomwa na mtu mmoja tu kwa lengo la kufikisha ujumbe fulani bila ya kujikalifisha kuiremba na kuipamba na kujitutumua. Ama anaashiid ni mkusanyiko wa sauti za watu wanaozipamba sauti zao na kuziremba wakiwa na naghma huku wakiimba anaashiid zao.
Na zote hizi hazifai nimambo ya kizushi yapumbao
Wallahu aalam.

Address

Stone Town

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Himaya ya wana Qurashiyyah posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share