04/06/2026
Leo Tarehe 04/06/2026 Taasisi ya Wasaidizi wa Kisheria Wilaya ya MBOZI ( WSCO) kwa kushirikiana na Polisi Kata ya MAHENJE Inspector NELSON MWINUKA na Afisa Dawati la Msaada wa Kisheria Wilaya ya MBOZI Bi. LILIAN KIKOTI na Wajumbe wa kamati za MTAKUWWA Kata ya MAHENJE,Wamefanikiwa Kutoa Elimu ya Kisheria hususani, Elimu ya Kupinga Vitendo vya Ukatili, Dhidi ya Wanawake na Watoto katika Mkutano Mkuu wa Shule ya Msingi MAHENJE ambapo pamoja na Elimu zilizotolewa na wataalamu hao kikubwa wameweza kuwajengea uwezo wanafunzi kuhusiana na Mbinu mbalimbali za kujilinda Dhidi ya Ukatili kwa kipindi hiki Cha Likizo ambacho watakuwa Majumbani na wawapo maeneo mbalimbali Ambayo si Mazingira ya nyumbani, pamoja na Hilo wameweza kufundishwa Maana ya Ukatili,aina za Ukatili na Mifano yake,Madhara yake na Maeneo ya kutoa Taarifa pindi wanapoona viashiria vya Ukatili,au pindi unatokea,
Kwa upande wa wazazi nao wamejengewa Uwezo,na kuwahamasisha wazazi kujitahidi kuwalinda Watoto Wao Dhidi ya Vitendo vya Ukatili, na kuwa karibu na Watoto na Kupata Muda wa kuongea nao ili kujua changamoto zao na kutafuta ufumbuzi