09/04/2022
Kwanza niwashukuru wote mlioshiriki kumchangia dada ambaye anaendelea na matibabu katika hospitali ya Manipal, Bangalore, India. Kwa siku chache tulizofanya challenge yetu alipata 42M kati ya 65M alizokua akihitaji. Hivyo bado 23M ambazo tutazimalizia mwisho wa mwezi huu.
Nililazimika kukatisha challenge ya Mishy na kumuomba tuendelee mwisho wa mwezi, kwa ajili ya ndugu yangu Joseph Massawe ambaye ni mgonjwa sana. Joseph alianza kuugua 2020 kwa kuvimba mwili na kupata michubuko kwenye ngozi. Alitibiwa Agha Khan na Rabinisia lakini hali yake haikutengemaa. Aliendelea kupata changamoyo ya mapafu na moyo kushindwa kufanya kazi vizuri.
Baadae alichukuliwa sampuli (biopsy) na majibu yakaonesha ana "auto immune syndrome" yani mfumo wake wa kinga kushambulia mwili wake badala ya kumlinda (immune system attacking your body instead of protecting it). Magonjwa haya kwa ujumla huitwa Rhaematological disease.
Matibabu yake ni kupandikizwa seli kinga nyingine (immunoglobulin replacement therapy) ambayo hufanyika nje ya nchi. Familia ikampeleka Medicana international Hospital iliyopo mjini Izmir, Uturuki.
Alipofika ikaonekana ana maji kwenye chamber moja ya moyo (pedicarium) na infection kwenye mapafu. Madaktari wakashauri kabla ya upandikizaji wa seli, atibiwe kwanza magonjwa yanayomsumbua. Ametibiwa na hali yake imetengemaa kidogo hivyo kwa sasa anaweza kupandikizwa seli.
Gharama za upandikizaji ni $19,000 lakini pia ana deni la $6,000 na hivyo kufanya jumla kuwa $25,000 sawa na TZS 60M.
Bahati mbaya kipindi hiki ambacho yupo tayari kupandikizwa seli, familia imeishiwa nguvu. Kwa zaidi ya miaka miwili familia imetumia gharama kubwa kumtibia, hivyo kwa sasa pumzi imekata.
Hivyo ndugu, jamaa na marafiki tumejipigapiga ili kuokoa maisha yake na kupata 20M, bado 40M. Kwa unyenyekevu naomba tuwe na challenge ya masaa 72 kuokoa maisha ya ndugu yetu huyu. Kumbuka bila kufanya upandikizaji wa seli Joseph hataweza kuendelea kuishi.
Tuma mchango wako kwenda (Tigopesa) 0714-049556 AU (MPESA) 0745-777112 Martina Desdery Massawe. Huyu ni dada mkubwa wa Joseph. Asante na Mungu akubariki.
Nihurumie foundation TZ