20/05/2026
Elimu ya uhifadhi mashuleni ni uwekezaji wa Taifa la kesho.
Kuelimisha watoto kuhusu umuhimu wa uhifadhi wa mazingira na wanyamapori ni hatua muhimu ya kujenga jamii yenye uelewa, uwajibikaji na uwezo wa kuishi kwa amani na tembo pamoja na viumbe wengine wa porini.
Kupitia elimu hii, tunakuza kizazi kinachotambua thamani ya urithi wa asili na wajibu wa kuulinda kwa manufaa ya sasa na ya vizazi vijavyo.