thedi.or.tz

thedi.or.tz We are non-profit Organisation to promoting health, environmental sustainability and development.

 : Katika picha ni mtaalamu wa afya ya kinywa na meno kutoka shirika la   akitoa ufafanuzi wa hatua za kufuata wakati wa...
11/05/2024

: Katika picha ni mtaalamu wa afya ya kinywa na meno kutoka shirika la akitoa ufafanuzi wa hatua za kufuata wakati wa kusafisha kinywa.

Ufafanuzi huo umetolewa kwa waalimu wa afya shule za msingi na wahudumu wa afya ngazi ya jamii wakati wa kilele cha mafunzo ya mradi wa kuboresha huduma za afya ya kinywa na meno wilayani Misungwi, ambapo mafunzo hayo yamehitimishwa tarehe tisa mwezi Mei.

Aidha, mradi huu umelenga kuboresha upatikanaji wa huduma bora za kinywa na meno wilayani Misungwi hususani maeneo yasiyo na huduma hizo kwa Sasa. Pia, mradi huu utatekelezwa kwa kipindi cha miaka mitatu mpaka kufikia mwezi Disemba mwaka 2026.

📸.dom

11/05/2024

. Kutoka katika video hapo juu, ni mtaalamu wa kinywa na meno Caroline Smith kutoka Shirika la alipokuwa akitoa ufafanuzi wa hatua zinazotakiwa kufuatwa wakati wa kusafisha kinywa.

Ufafanuzi huo ulitolewa kwa wakazi wa Wilaya ya Misungwi wakati wa kutoa mafunzo kwa waalimu wa afya shule za msingi na wahudumu wa afya ngazi ya jamii yaliyofanyika kuanzia Mei sita na kuhitimishwa Mei tisa katika viwanja vya shule ya sekondari Kolomije Wilayani humo.

Pia, mafunzo hayo yametolewa k**a hatua za mwanzo za utekelezwaji wa mradi wa kuboresha huduma za afya ya kinywa na meno wilayani Misungwi ambapo mradi huo unatekelezwa kwa ushirikiano wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi, Shirika la Tanzania Health Environment and Development Initiatives (THEDI) na Bridge2Aid (B2A) kutoka nchini Uingereza.

Sanjari na hayo, malengo mahsusi ya mradi huo ni kurahisisha upatikanaji wa huduma bora za kinywa na meno kwa wakazi wilayani humo.

THEDI NA B2A KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA YA KINYWA NA MENO MISUNGWI. Shirika la Tanzania Health Environment and Development...
10/05/2024

THEDI NA B2A KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA YA KINYWA NA MENO MISUNGWI.

Shirika la Tanzania Health Environment and Development Initiatives limetoa mafunzo kwa waalimu wa afya shule za msingi na wahudumu wa afya ngazi ya jamii yaliyofanyika kuanzia tarehe sita na kuhitimishwa tarehe tisa mwezi mei k**a sehemu ya utekelezaji wa mradi wa kuboresha huduma za afya ya kinywa na meno wilayani Misungwi.

Mradi huo umetoa mafunzo kwa jumla ya walimu 265 kutoka shule 83 na wahudumu wa afya ngazi ya jamii 166 kutoka katika vituo vya afya 38 wilayani Misungwi.

Pia, mradi huo umelenga kuwarahisishia wananchi kuzifikia huduma bora za kinywa na meno kwa kutumia mikakati mbalimbali ikiwemo kuanzisha huduma za mikoba, kuwezesha upatikanaji wa vifaa na wataalamu katika ngazi ya hospitali na vituo vya afya, kutoa mafunzo kwa wataalamu wa afya ya kinywa na meno ngazi ya Afisa Tabibu pamoja na kutoa elimu ya afya ya kinywa na meno kwa wanafunzi mashuleni na jamii kwa ujumla.

Kwa upande wake mgeni rasmi katika mafunzo hayo alikuwa ni Afisa tabibu-meno, Dokta. Casmir Richard amelishukuru shirika la THEDI na wadau wengine kwa kuendelea kuunga mkono juhudi za serikali katika kuboresha huduma za afya nchini.

Tunawatakia Wafanyakazi wote Nchini na kote Duniani Maadhimisho mema ya Siku ya Wafanyakazi.
01/05/2024

Tunawatakia Wafanyakazi wote Nchini na kote Duniani Maadhimisho mema ya Siku ya Wafanyakazi.

THEDI and B2A Led the Commemoration of the 2024 World Oral Health Day (WOHD) Event in Misungwi District - Mwanza, Tanzan...
28/04/2024

THEDI and B2A Led the Commemoration of the 2024 World Oral Health Day (WOHD) Event in Misungwi District - Mwanza, Tanzania

Maintaining good oral hygiene habits, such as brushing twice a day, visiting the dentist every six months, flossing, and limiting sugar intake, is crucial to ensuring healthy gums, preventing costly dental procedures, and mitigating long-term health concerns. Tanzania Health Environment and Development Initiatives (THEDI) and Bridge2Aid (B2A) are committed to improving access to quality oral healthcare services in six district councils of the Mwanza region, Tanzania. The initiative aims to address barriers such as low coverage, poor accessibility, lack of awareness, and limited resources, thereby enhancing the oral health outcomes of underserved populations.

The project is designed to enhance coverage and access to quality oral healthcare services through outreach programs and capacity-building training for Dental Therapists. Additionally, it aims to promote positive oral health behaviors and practices through school-based oral health promotion and the utilization of Community Health Workers (CHWs) to disseminate relevant oral health Information, Education, and Communication (IEC) materials within the community.

As part of the project activities, from March 19th to 20th, 2024, THEDI and B2A collaborated with the Misungwi District Council to lead the commemoration of the 2024 World Oral Health Day (WOHD) events. The event was held at Usagara Health Center and over the course of two days, the project registered a total of 118 clients (47 males and 71 females) with various oral health conditions. Oral health services were provided jointly by experts from THEDI, Chicco Specialized Dental Clinic, Hope Dental Center, and the Misungwi District Council.

The WOHD event was presided over by Hon. Kashinje Machibya, the Councilor of Usagara Ward and Chairperson of the Misungwi District. In his address, he expressed gratitude for selecting Misungwi as a project implementation site, highlighting its relevance and the community's need for such services. He also pledged his commitment to ensuring the project achieves its objectives.

Taasisi ya Tanzania Health Environment and Development Initiatives (THEDI) inawatakia Watanzania wote heri ya miaka 60 y...
26/04/2024

Taasisi ya Tanzania Health Environment and Development Initiatives (THEDI) inawatakia Watanzania wote heri ya miaka 60 ya Muungano.

25/04/2024

•AFYA YA KINYWA NA MENO.
-
THEDI ni moja kati ya mashirika yasiyo ya kiserikali yaliyoshiriki kikamilifu katika maadhimisho ya siku ya Afya ya Kinywa na Meno yaliyofanyika tar 17 Machi 2024 katika wilaya ya Misungwi, mkoani Mwanza.
-
THEDI imekuwa mdau mkubwa wa Afya ya Kinywa na Meno na imeendelea kutoa huduma bora za afya ya kinywa na meno ikiwemo elimu na matibabu katika wilaya ya Misungwi.
-

  Wakazi wapatao 118 wa kata ya Usagara wilayani Misungwi walikuwa wakipatiwa huduma za afya ya kinywa na meno bure na s...
25/04/2024

Wakazi wapatao 118 wa kata ya Usagara wilayani Misungwi walikuwa wakipatiwa huduma za afya ya kinywa na meno bure na shirika lisilokuwa la kiserikali la .or.tz kwa kushirikiana na pamoja na wakati wa maadhimisho ya siku ya afya ya kinywa na meno yaliyofanyika tarehe 20 mwezi machi wilayani humo.
-
Sanjari na hayo Mratibu wa afya ya kinywa na meno wilaya, Dokta. Jacob Ngorobi amesema kuwa zaidi ya 80% ya wananchi wilayani humo wanatatizo la afya ya kinywa na meno.
-
Nao Wananchi waliofika katika kituo cha afya cha Usagara kupata huduma hizo za afya waliendelea kuomba wataalamu wa afya ya meno na kinywa na wadau wengine wa afya kuendelea kutoa huduma hiyo kwa jamii.
-
Kwa upande wake Mkurugenzu Mtendaji wa Shirika lisilokuwa la kiserikali la .or.tz Bwana. Joshua Rubona alisema kuwa zipo mila na desturi potofu kuhusu afya ya kinywa na meno k**a vile, baadhi ya maeneo au makabila wanaamini kuwa watoto wadogo wanapopata homa au kuharisha wanaamini kuwa wana meno ya plastiki na mwisho wake huishia kuwapeleka kwa waganga wa kienyeji.
-
Pia, Bwana Rubona aliongezea kwa kusema kuwa wameweka malengo ya kufikia vituo vya afya vijijini ambavyo huduma hizi hazipatikani na watahakikisha upatikanaji wa vifaa, upatikanaji wa wataalamu na mafunzo ya vitendo kwa wataalamu wa afya na upande wa wananchi watahakikisha wanafika mashuleni hususani katika shule za msingi kwa lengo la kufanya uhamasishaji mashuleni kupitia kwa waalimu wa afya wa shule za msingi na jamii kwa ujumla kupitia wahudumu wa afya.

.or.tz

 . Katika picha ni wananchi wa kata ya Usagara wilayani Misungwi mkoani Mwanza walipokuwa wakipatiwa elimu ya usafi wa k...
25/04/2024

. Katika picha ni wananchi wa kata ya Usagara wilayani Misungwi mkoani Mwanza walipokuwa wakipatiwa elimu ya usafi wa kinywa na meno katika kituo cha afya cha Usagara
-
Shughuli hiyo ilifanyika wakati wa maadhimisho ya siku ya afya ya kinywa na meno duniani yaliyofanyika tarehe 20 mwezi machi, ambapo shirika lisilokuwa la kiserikali la "Tanzania Health Environment and Development Initiatives-THEDI" .or.tz pamoja na wadau wengine wa afya ambao ni na walishirikiana kufikisha elimu ya afya ya kinywa na meno kwa wakazi wa kata ya Usagara wilayani Misungwi.
-
Ikumbukwe kuwa maadhimisho haya hufanyika mara moja kila mwaka na wilayani Misungwi yalihudhiriwa na mgeni rasmi ambaye ni Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Misungwi na Diwani wa kata ya Usagara Mh. Kashinje Machibya.
-
Sanjari na hayo, wataalamu na wadau wa afya mbalimbali wanaendelea kuwahimiza wananchi wote kuwa ni muhimu kuchua hatua stahiki za kujali afya ya kinywa na meno na kuhakikisha wanazingatia usafi wa kinywa, lishe bora na kuwaona wataalamu wa kinywa na meno angalau kila baada ya miezi sita ili kudumisha afya bora ya kinywa na meno.
-

Official Logo of Tanzania Health Environment and Development Initiatives (THEDI) -ABOUT US Tanzania Health Environment a...
25/04/2024

Official Logo of Tanzania Health Environment and Development Initiatives (THEDI)

-

ABOUT US

Tanzania Health Environment and Development Initiatives (THEDI) was founded in October 2022 by a group of energetic specialists in public health, environment, finance and administration, monitoring and evaluation, and information technology. They came together with the mission to partner with communities, and stakeholders to protect, promote, and improve people’s health and well-being. They also realized the necessity of this establishment as a driving force in contributing to sustainable community development in Tanzania.

THEDI like other Non-Governmental Organizations and international humanitarian institutions, aims at achieving sustainable results from developmental where health promotion is seen as a core driving force. The multisectoral approach will lead to the success of the organization and the focus will be on strengthening the participation and involvement of communities and different stakeholders for impactful.

-

For more information visit our website at thedi.or.tz

-

Address

Mwanza

Opening Hours

Monday 09:00 - 17:00
Tuesday 08:00 - 16:00
Wednesday 08:00 - 16:00
Thursday 08:00 - 16:00
Friday 08:00 - 16:00

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when thedi.or.tz posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to thedi.or.tz:

Share