16/05/2026
Katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya Familia, CDI tulipata fursa ya kushiriki maadhimisho yaliyofanyika katika viwanja vya Kitangiri, Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza yaliyoandaliwa na Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela chini ya kauli mbiu: “Mtoto ni malezi; msingi wa familia bora na taifa imara.”
Kupitia maadhimisho hayo, CDI tuliwasilisha mada kuhusu “Uhusiano wa afya ya akili na familia bora” tukisisitiza umuhimu wa malezi chanya, ustawi wa afya ya akili, na mshikamano wa kifamilia katika kujenga jamii salama na taifa lenye nguvu.
Tunathamini ushirikiano wa wadau wote walioendelea kuhamasisha ustawi wa familia na maendeleo ya jamii.
Maadhimisho haya hufanyika tarehe 15 May kila mwaka.