16/05/2026
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Albert Chalamila, amewataka Vijana wasiharibu maisha yao kwa Siasa na propaganda za chuki, badala yake wajikite katika jitihada kwa kuwa ndio siri pekee ya mafanikio katika maisha yao.
Chalamila amesisitiza maisha si mepesi k**a wengi wanavyodhani ni magumu na hayako kwenye propaganda ya vinywa na maneno mengi, bali lazima kupitia magumu ili kufanikiwa.
Chalamila ameeleza hayo leo, Mei 16, 2026 wakati akizungumza katika Kongamano la Vijana wa Vyuo Vikuu lililobeba ujumbe wa Never Again, ambapo amesema, "pamoja na kupata elimu mnayoipata leo, mchawi wa kweli ni kujimudu kimaisha na namna pekee ya kujimudu kimaisha ni kuyatafsiri maisha kwa namna ya kipekee," amesema Chalamila.
Pamoja na hayo, Chalamila ameambatanisha maneno yake hayo na nasaha kwa Vijana kuwa, inasikitisha kuona Vijana wanaonyesha chuki dhidi ya Watu sio kwa sababu waliwakosea bali kwa kuwa wamepewa nafasi za Uongozi Serikalini.