10/08/2026
Siku ya ijumaa ya tarehe 07/08/2026 tulipokea ugeni maalum wa wadau wa elimu wa mkoa wa Mara na maeneo ya jirani na kushiriki katika warsha jumuishi iliyojenga mahusiano yenye afya na kuongeza uelewa juu ya masuala ya ulemavu na elimu jumuishi.
Tunawapongeza sana kushiriki pamoja nasi katika Warsha na kuona fursa, miundombinu rafiki, uadilifu na umakini wa wanafunzi wetu.
Pichani ni baadhi ya matukio wakati wa warsha ikiwemo mawasilisho/presentation yaliyofanywa na wanafunzi wa fani mbalimbali ndani ya karakana zao.
Lake Victoria Disability Vocational Training Center tupo kukusaidia kufikia ndoto yako.