Tanzania Childfind Foundation

Tanzania Childfind Foundation Tanzania ChildFind Foundation is a based non-profit dedicated to upholding child rights and promoting child welfare across Tanzania.

We work tirelessly to protect vulnerable children, ensure their safety, and empower them to thrive in a caring society.

27/04/2026

Celebrating my 5th year on Facebook. Thank you for your continuing support. I could never have made it without you. 🙏🤗🎉

TALAKA AU KUACHANA KUNAWAATHIRI ZAIDI WATOTO.Sehemu Ya 3Tukiwa tunaelekea mwishoni mwa mada hii napenda tumalizie Kwa ku...
14/08/2024

TALAKA AU KUACHANA KUNAWAATHIRI ZAIDI WATOTO.

Sehemu Ya 3

Tukiwa tunaelekea mwishoni mwa mada hii napenda tumalizie Kwa kuangalia mambo tunayopaswa kufanya baada ya kuachana au kutalikiana.

Unaweza ukajiuliza kwanini natumia maneno haya kuachana na kutalikiana. Talaka ni Kwa watu walioona na kuachana namaanisha watu walioishi pamoja bila kufunga ndoa.

I think hapo tunaelewana.

K**a ilivyo imani yangu siku zote ni kwamba kuachana sio vita. Hivyo kuachana kwa wazazi hakupaswi kuwa ndio mwisho wa ushirikiano wao katika malezi ya watoto wao.

Hata baada ya kuachana au kutalikiana wazazi wanapaswa kushirikiana katika majukumu ya kuwalea watoto wao kana kwamba bado wanaishi pamoja, japo ni kweli kwamba sio rahisi k**a tunavyoweza kutamka.

Sio rahisi kwasababu wazazi walioachana au kutalikiana hawatumii muda wao pamoja. Kila mtu anakuwa na harakati zake.

Na wazazi wengine wanataka kuwashirikisha watoto ugomvi wao. Wanawaeleza watoto wao juu ya ubaya wa baba au juu ya ubaya wa mama. Kosa hili maranyingi linafanywa na wazazi wa k**e, yaani kina mama.

Hii inaweza kupelekea mtoto akawa na chuki au dharau dhidi ya mzazi wake mwingine baada ya kulishwa sumu kuhusu madhaifu ya huyo mzazi.

Natoa rai yangu kwa wazazi, tusifanye ujinga huo. Tuwaache watoto wafurahie upendo wa pande zote mbili hata baada ya sisi kuachana au kutalikiana.

Kutalikiana kunaruhusiwa hata katika maandiko matakatifu lakini, tutalikiane kwa sababu za msingi na sio kwasababu ya fashion au kuchokana tu.

Maandiko yaasema...
MATHAYO 19:7,9
"Wakamwambia, Jinsi gani basi Musa aliamuru kumpa hati ya talaka, na kumwacha?

Nami nawaambia ninyi, Kila mtu atakayemwacha mkewe, isipokuwa ni kwa sababu ya uasherati, akaoa mwingine, azini; naye amwoaye yule aliyeachwa azini."

Bila shaka, huenda mengi zaidi yakahitajika kuliko kuvumilia tu katika ndoa ambayo haina furaha.

Muhimu tusiwatese watoto hata mara baada ya sisi wazazi kuachana au kutalikiana na maisha yetu yasiwe ya magomvi na uhasama usio na maana yoyote.

Tusiendeane kwa waganga ili kuharibiana maisha wala tusifanyiane visa ili kutuondoa kwenye njia sahihi za mafanikio tena ikiwezekana tusaidiane ili kila mmoja afanikiwe katika maisha yake.

Mafanikio ya wazazi ndio mafanikio ya watoto wetu.

Ahsante kwa kufuatilia mada hii na sina shaka k**a utaielewa mada hii basi utaenda kuwa mzazi ambaye ni mfano wa kuigwa katika jamii zetu.

Mungu awabariki sana.

A Dream By George G Francis

Join us 👇
Tanzania ChildFind Foundation

TALAKA AU KUACHANA KUNAWAATHIRI ZAIDI WATOTO.Sehemu Ya 2Matatizo ambayo watoto hupata baada ya wazazi wao kutalikiana ya...
14/08/2024

TALAKA AU KUACHANA KUNAWAATHIRI ZAIDI WATOTO.

Sehemu Ya 2

Matatizo ambayo watoto hupata baada ya wazazi wao kutalikiana yanaendelea kuwaathiri hata wanapokuwa watu wazima.

Hapa tafiti nyingi zinaonesha kuwa kuna uwezekano mkubwa hata wao pia wakashindwa kudumu kwenye ndoa zao au mahusiano yao. Suala la kuacha au kuachika kwao wanaona ni kawaida tu.

Hivyo ushauri ni kwamba wazazi inapofikia point imeshindikana kuendelea kuishi pamoja basi tufikirie namna bora zaidi ya malezi kwa watoto wetu.

WAFILIPI 2:4,5
"Kila mtu asiangalie mambo yake mwenyewe, bali kila mtu aangalie mambo ya wengine.

Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu"

Hivyo tusiangalie masrahi yetu peke yake bali na masrahi ya watoto wetu.

Siku zote ni lazima tukumbuke kuwa mahitaji ya mzazi na mahitaji ya mtoto yanatofautiana. Mzazi anayefukiria kuhusu kuachana na mzazi mwenzake ni kwamba anataka kuanza maisha mapya peke yake au na mtu mwingine.

Lakini kwa kawaida hasingependa maisha yake yabadilike, eti akaishi na baba bila mama au akaishi na mama bila baba. Yeye anapenda aendelee kuishi na wazazi wake wote wawili kwa amani na upendo.

Hata leo ukifanya uchunguzi na kuwauliza watoto waliopitia malezi ya upande mmoja vipi k**a walipata furaha baada ya wazazi wao kuachana jibu litakuwa ni 'HAPANA.'

Binafsi nimelelewa na ndugu zangu tangu nikiwa mdogo naelewa jinsi maisha ya kuishi mbali na wazazi wazazi wako iwe wamefariki au wameachana haifurahishi hata kidogo.

Lakini kila kwenye mabaya mengi, mazuri hayakosekani. Kuna uwezekano mdogo sana wa watoto kuwa na furaha baada ya wazazi wao kutalikiana. Inawezekana pia akapata furaha japo hizi ni case chache sana.

Muhimu, k**a sio salama kwa maisha yenu na kwa usalama wa watoto wenu basi hapo hakuna namna itabidi wazazi waachane kwa amani ili iwe rahisi kuendelea kushirikiana kwa ukaribu katika malezi ya watoto wao.

Inaendelea....

A Dream By George G Francis

Join us 👇
Tanzania ChildFind Foundation

TALAKA AU KUACHANA  KUNAWAATHIRI ZAIDI WATOTO.Sehemu Ya 1Miaka ya hivi karibuni kumekuwa na changamoto nyingi sana katik...
14/08/2024

TALAKA AU KUACHANA KUNAWAATHIRI ZAIDI WATOTO.

Sehemu Ya 1

Miaka ya hivi karibuni kumekuwa na changamoto nyingi sana katika ndoa na mahusiano hali inayopelekea ndoa nyingi na mahusiano mengi kuvunjika.

Mbaya zaidi kuvunjika kwa ndoa na mahusiano ambayo teyari kuna watoto ndani yake, wazazi hawaangalii kabisa madhara ambayo yanaweza kuwapata watoto mara baada ya wao kushindwa kuendelea kuishi pamoja.

Lengo kuu la kuanzisha mahusiano au ndoa ni kuishi maisha ya pamoja k**a mume na mke katika siku zote za uhai lakini inapotokea imeshindikana kuendelea kuishi pamoja k**a kuna watoto ni muhimu kwanza kuagalia ustawi na ukuaji bora wa watoto hao.

Tafiti nyingi zinaonesha kwamba watoto huathirika sana wazazi wanapoachana. Na tukiaangalia ndoa nyingi au mahusiano mengi yanavunjika kwa ugomvi hivyo kupelekea wazazi kushindwa kufikiria kuhusu usalama wa watoto baada ya wao kuachana.

Miongoni mwa athari zinazoweza kuwapata watoto baada ya wazazi kuachana ni k**a hizi zifuatazo.

1. Kukosa huduma na mahitaji muhimu ya mtoto. Mfano, chakula, sehemu nzuri ya kulala, mavazi, mahitaji ya shule na afya. Mtoto anakosa huduma hizi kwasababu ya kuvunjika kwa ushirikiano mzuri kati ya baba na mama katika malezi.

2. Mtoto kuwa na mfadhaiko na kupoteza hali ya uchangamfu. Hii inatokana na upweke unaosababishwa na mazoea ya kuwaona wazazi wakiwa pamoja na kuwafurahia.

3. Mtoto kuwa na hasira za marakwamara pamoja na chuki. Hii inatokana na kuathirika kisaikolojia hasa k**a ameshuhudia ugomvi wa baba na mama kabla ya kuachana.
MFANO: k**a aliona baba akimpiga mama au mama akimfanyia baba ubaya fulani. Hivyo hii kitu inamuingia na kumuathiri mojakwamoja.

4. Kushuka kwa uwezo wao wa kufanya vizuri katika masomo. Hii wakati mwingine kunaweza kumfaya mtoto akaacha hata shule mojakwamoja. Hii inatokana na kukosekana kwa usimamizi mzuri kutoka kwa wazazi wote wawili baada ya kuachana.

5. Watoto kupata hofu na wasiwasi au kujiamini kupitiliza Mtoto aliyelelewa na wazazi wote wawili na yule aliyelelewa na mzazi mmoja wanatofautiana sana kwenye eneo hili.
Hapa kuna mawili; mtoto anaweza kuwa mwoga sana au k**a kujiamini basi anjiamini kupitiliza. Vyote hivi vina madhara makubwa linapokuja suala la uhusiano wake na watu wengine. Akiwa na hofu basi ataogopa sana watu na k**a akijiamini kupitiliza basi atakuwa na dharau sana kwa watu.

Inaendelea.....

A Dream By George G Francis

Join us 👇
Tanzania ChildFind Foundation

Address

Morogoro

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Tanzania Childfind Foundation posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share