21/04/2026
Mwaka 2024, TSO ilifanikiwa kuwawezesha vijana 6 wanaoishi katika mazingira magumu ya ukosefu wa kipato kukamilisha mafunzo ya stadi za maisha katika afya ya akili, maadili na tabia, elimu ya fedha, ujuzi wa kidijitali na ujasiriamali pamoja na kuwaunganisha na wadau wa maendeleo iliyowawesha kupata ujuzi wa vitendo na fursa za ajira. Aidha, TSO iliwawezesha vijana 40 (wasichana 26 na wavulana 14) wa Shule ya Sekondari Mikocheni, kuongeza uwezo wa kujiamini, kutambua kusudi la maisha na kuweka malengo, jambo lililowasaidia kuboresha ufaulu wao wa masomo na maisha yao binafsi. (Tazama picha zaidi za mafunzo na ajira hapa chini).