16/05/2026
Wiki hii mioyo yetu imebeba maumivu ambayo hayaelezeki kwa maneno kiasi kwamba wengine tumeshindwa hata kulia. Tumempoteza ndugu yetu mpendwa Yohana Edwin (MC Mwakapalila a.k.a Mtumwa Asiye na Faida) kwa ajali. Mwakapalila alikuwa mwanga kwa wengi, sauti ya faraja kwa wenye huzuni, mfano wa kijana bora na nguzo imara kwetu.
Alikuwa mtu mwenye upendo wa kweli. Alipenda watu kwa moyo safi bila ubaguzi. Alikuwa kiongozi ambaye hakutafuta sifa bali alitafuta kuona watu wakisimama, wakitabasamu na wakiamini tena kwenye maisha. Alikuwa sehemu ya vijana waliowasha taa za matumaini kwa watu wengi waliokuwa wameyapoteza. Wapo wengi leo wanalia kimya kimya kwa sababu waliwahi kuguswa na wema wake, ushauri wake, upendo wake, msaada wake na moyo wake wa kipekee sana.
Ni ngumu kuamini kuwa sauti ya Mtumwa Asiye na Faida k**a alivyopenda kuitwa haitasikika tena, ucheshi na tabasamu lake hatutaliona tena na mikono yake haitainuliwa tena kusaidia wengine. Kifo kimetuibia mtu muhimu sana. Jamii ya wana-Mbeya imepoteza shujaa, marafiki tumepoteza rafiki wa kweli, familia ya MIMI NINA WATU na WANA FOUNDATION tumepoteza kipande cha moyo wetu.
Kuna watu huishi miaka mingi lakini hawaachi alama. Lakini MC Mwakapalila katika muda wake mfupi kwenye uso wa dunia ameacha historia ya upendo, utu na matendo makubwa yasiyofutika mioyoni mwa watu. Hakika Mauti imevikwa taji leo.
Pumzika kwa amani my Brother since childhood, Classmate, Mdau wa Matendo Mema na Kiongozi wa kweli. Ninamshukuru Mungu kwaajilili ya maisha yako na mara zote nilikupa maua yako kwa maneno ya kinywa changu kila uliposhiriki Events za WANA CHARITY. Umeondoka kwenye uso wa nchi lakini jina lako, matendo yako na upendo wako vitaendelea kuishi ndani yetu milele.
Safiri salama MC Mwakapalila🕊️😭