Makutano ya Wajasiriamali

Makutano ya Wajasiriamali Huu ni ukurasa mubashara wa Asasi (NGO) ya Wajasiriamali. Katika ukurasa huu utajifunza ujasiriamali kwa lugha adhimu ya Kiswahili.

Utapata mafunzo, semina, maonyesho, hadithi na bidhaa zote za kibiashara za kijasiriamali.

Mjasiriamali: Tabia gani isiyofaa ungependa kuwaomba radhi wateja?.....Rafiki yangu, tabia moja ambayo mjasiriamali anap...
08/09/2026

Mjasiriamali: Tabia gani isiyofaa ungependa kuwaomba radhi wateja?.....

Rafiki yangu, tabia moja ambayo mjasiriamali anapaswa kuomba radhi kwa wateja wake ni kuwapuuza baada ya kupata pesa zao.

Mteja hakupaswi kuhisi kwamba ulikuwa unamhitaji mpaka aliponunua, halafu baada ya hapo humjali tena.

Ukimchelewesha, usipomjibu, ukimpa bidhaa isiyo sahihi au ukikosea huduma, kubali kosa na sema “samahani.” Usitafute visingizio.

“Mteja anaweza kusamehe kosa lako, lakini ni vigumu kusahau namna ulivyomtendea ulipokosea.”

Mjasiriamali, jiulize:

Ni tabia gani katika huduma yako ambayo k**a ungekuwa mteja, ungependa muuzaji akuombe radhi?

Mabadiliko ya biashara yanaweza kuanza na “Samahani, nilikosea. Nifanye nini kurekebisha?”

Mimi nafundisha ujasiriamali, karibu tuyajengeeee!

UNAOGOPA KUONGEA NA WATAALAMU WA BIASHARA NA UJASIRIAMALI...... Soma hapa!Rafiki yangu, usiogope kuongea na wataalam wa ...
04/09/2026

UNAOGOPA KUONGEA NA WATAALAMU WA BIASHARA NA UJASIRIAMALI...... Soma hapa!

Rafiki yangu, usiogope kuongea na wataalam wa biashara kwa sababu tu unaona wana uzoefu kuliko wewe. Ukweli ni kwamba, hata wewe una kitu cha kujifunza na wao wana kitu cha kushirikisha. Ushauri na mentorship vinaweza kuongeza uelewa, kujiamini na kukusaidia kuona biashara yako kwa mtazamo mwingine.

Anza kidogo sana:

1. Usianze kwa kutaka kumweleza kila kitu. Muulize swali moja tu, k**a: “Kwa uzoefu wako, ni kosa gani moja unaloliona mara nyingi kwa wajasiriamali wapya?”

2. Andaa swali kabla ya kukutana naye. Hii itakusaidia usipate hofu ya kukosa cha kusema.

3. Jitambulishe kwa sentensi moja: “Nina biashara ya ___, na kwa sasa changamoto yangu kubwa ni ___.”

4. Usijaribu kuonekana unajua kila kitu. Mwambie, “Nataka kujifunza kutoka kwako.” Hilo ni jambo la kawaida kabisa katika networking ya biashara.

5. Anza na mtaalamu mmoja unayemheshimu. Mazoea ya kuzungumza na watu wenye uzoefu yataongeza kujiamini taratibu.

Na kumbuka hili, rafiki yangu:
..“Huwezi kujua kila kitu kabla hujaanza kuuliza.”

Mtaalamu wa biashara si mtu wa kukuogopesha; anaweza kuwa mtu wa kukusaidia kuona kile ambacho wewe hujakiona. Kuomba ushauri si udhaifu—ni hatua ya kujifunza na kukua.

Leo chagua mtaalamu mmoja tu, mtumie ujumbe mfupi: “Nina jambo moja la biashara ningependa kujifunza kutoka kwako. Naweza kukuuliza?”

Karibu tuyajengeeee?

21/08/2026

A BIG MISTAKE ENTREPRENEURS MAKE: POOR PRODUCT PLACEMENT IN THE MARKET....

One of the biggest mistakes I see among entrepreneurs is having a good product but taking it to the market without a clear strategy. Some entrepreneurs produce first and only later start asking: “Where will I find customers?”

The truth is, a good product does not automatically sell itself. You need to understand who your customer is, what problem they have, where they are, what they can afford and why they should choose your product over the competition.

As an Entrepreneurship Coach, my advice is simple: plan the market before scaling production. Conduct simple market research, talk to potential customers, test your product, listen to feedback and adjust your strategy.

Do not produce simply because you can. Produce because the market needs it.

By Simeon Mihinga | Entrepreneurship Coach

ONE BIG MISTAKE ENTREPRENEURS MAKE: “I’LL SELL IT LATER!”....One of the biggest mistakes I see among entrepreneurs is cr...
20/08/2026

ONE BIG MISTAKE ENTREPRENEURS MAKE: “I’LL SELL IT LATER!”....

One of the biggest mistakes I see among entrepreneurs is creating a product or service today while assuming that customers will come later.

The truth is, “later” is not a sales strategy. You can spend time, money and energy creating an excellent product, but if you don't know who will buy it, why they will buy it, and how you will reach them, you may end up with a great product and very few customers.

As an Entrepreneurship Coach, my advice is simple: start looking for the customer before everything is perfect. Talk to potential customers, understand their needs, test your offer, make early sales, listen to feedback and improve.
..Don’t wait to sell later. Learn to sell from today.

Because a business is not built by products alone it is built by customers.

By Simeon Mihinga | Entrepreneurship Coach

19/08/2026

Ben N Huynh most welcome

KOSA KUBWA LA MJASIRIAMALI: “NITAUZA BAADAYE!”....Moja ya makosa ninayoyaona mara nyingi kwa wajasiriamali ni kutengenez...
19/08/2026

KOSA KUBWA LA MJASIRIAMALI: “NITAUZA BAADAYE!”....

Moja ya makosa ninayoyaona mara nyingi kwa wajasiriamali ni kutengeneza bidhaa au huduma leo wakiamini wateja watakuja baadaye.

Ukweli ni kwamba, “baadaye” siyo mkakati wa mauzo. Unaweza kutumia muda, fedha na nguvu nyingi kutengeneza bidhaa nzuri, lakini bila kujua nani atanunua, kwa nini atanunua na utamfikishiaje bidhaa hiyo, unaweza kubaki na bidhaa nyingi bila wateja.

K**a Entrepreneurship Coach, huwa nashauri: anza kumtafuta mteja kabla hujakamilisha kila kitu. Zungumza na watu, waulize mahitaji yao, jaribu kuuza, sikiliza mrejesho na boresha bidhaa yako kulingana na soko.
.. Usisubiri kuuza baadae. Jifunze kuuza tangu leo.

Kwa sababu biashara haijengwi na bidhaa pekee inajengwa na wateja.

Na Simeon Mihinga | Entrepreneurship Coach

Siku moja nilikutana na kijana mmoja.Alikuwa na bidhaa nzuri.  Bei yake ilikuwa sawa.  Hata wateja walikuwa wapo.Lakini ...
16/08/2026

Siku moja nilikutana na kijana mmoja.

Alikuwa na bidhaa nzuri.
Bei yake ilikuwa sawa.
Hata wateja walikuwa wapo.

Lakini kila anapofikiria kupiga simu au kuwaandikia…
moyo wake unapiga kwa nguvu.
Mikono yake inatetemeka.
Anajiambia: “Acha kesho…”

Kesho inakuja.
Kesho nyingine inakuja.
Miezi inapita.

Bidhaa yake inabaki pale pale.

Siku nyingine alinificha uso na kuniambia:
“Simeon… mimi siogopi biashara.
Ninaogopa kuongea na watu.”

Nilinyamaza.

Kwa sababu nimeona hii kitu mara nyingi.

Uoga katika ujasiriamali si hofu ya kushindwa tu.

Ni hofu ya kukataliwa.
Hofu ya kuchekwa.
Hofu ya kuonekana “unahitaji”.
Hofu ya mteja kusema “hapana” kwa sauti kali.

Wengi wetu tunaogopa kuongea na wateja sio kwa sababu hatuna bidhaa…
bali kwa sababu tunaogopa 'hisia' zitakazokuja baada ya majibu yao.

Tunajilinda.
Tunajificha nyuma ya “sijaandaa vizuri”.
Tunajidanganya kwamba “bado si wakati”.

Lakini ukweli ni huu:

Biashara haikui kwa sababu unaogopa kuongea.
Inakua unapoamua kuongea 'hata ukiwa unaogopa'.

Sasa nakuuliza wewe…

Je, wewe unaogopa nini hasa unapofikiria kuongea na mteja?


Address

P. O. Box 2091
Mbeya

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Makutano ya Wajasiriamali posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to Makutano ya Wajasiriamali:

Share