Walter Habari Tanzania.

Walter Habari Tanzania. TUPO KUKUHABARISHA. Karibu mpendwa upate habari na kuchangia mada mbalimbali.

14/08/2026

Karim Foundation yaibua teknolojia ya vyoo vya kisasa vinavyodumu miaka mingi

Mwaka 2018, Shirika la Karim Foundation lilijenga vyoo katika baadhi ya maeneo, lakini changamoto kubwa ilijitokeza baada ya vyoo hivyo kujaa ndani ya kipindi cha miezi sita.

Changamoto hiyo iliwasukuma kutafuta suluhisho la kudumu, hatua iliyowafanya kujifunza kutoka kwa mkandarasi nchini Brazil kuhusu teknolojia ya ujenzi wa vyoo vinavyoweza kudumu kwa muda mrefu bila kujaa.

Teknolojia hiyo sasa imeanza kutumika katika vyoo vinavyojengwa katika shule zinazofadhiliwa na Karim Foundation, huku mfumo huo ukilenga kuongeza muda wa matumizi na kupunguza changamoto ya vyoo kujaa mara kwa mara.

Shao Erro Ae, Mkurugenzi wa Karim Foundation, anaeleza zaidi kuhusu teknolojia hiyo ya kisasa iliyotumika katika ujenzi wa vyoo hivyo.

14/08/2026

Mamia Wajitokeza Kumshuhudia Mama Gift Magugu

Mamia ya wakazi wamejitokeza katika eneo la Mbugani, Kijiji cha Magugu, wilayani Babati, mkoani Manyara, kumshuhudia Mama Gift, mwanamke anayehusishwa na tukio lililozua taharuki baada ya kudaiwa kukutwa akichimbia kitu katika nyumba ya jirani yake.

Tukio hilo limeibua mjadala mkubwa miongoni mwa wakazi wa eneo hilo, huku baadhi yao wakidai kuwa mwanamke huyo alihusika na vitendo vya kishirikina.

Wakazi wa Magugu wamesema Mama Gift ni mtu anayefahamika katika jamii hiyo na amekuwa muimbaji wa kwaya katika moja ya makanisa yaliyopo Magugu, jambo ambalo limeongeza mshangao miongoni mwa waliomfahamu.

πŸŽ“πŸ”₯ **UNATAKA KUJENGA MUSTAKABALI WA KAZI KUPITIA ELIMU YA AFYA?**πŸ“’ **FURSA YA MASOMO HAYDOM INSTITUTE OF HEALTH SCIENCES...
14/08/2026

πŸŽ“πŸ”₯ **UNATAKA KUJENGA MUSTAKABALI WA KAZI KUPITIA ELIMU YA AFYA?**

πŸ“’ **FURSA YA MASOMO HAYDOM INSTITUTE OF HEALTH SCIENCES!**

Usipite tu… **BONYEZA LINK HAPA CHINI** πŸ‘‡πŸ‘‡ na ujue kozi, sifa na namna ya kujiunga.

πŸ“ž **Kwa maelezo zaidi: 0784 598 369**

🎯 **ELIMU LEO, TAALUMA KESHO!**

https://www.instagram.com/reel/DaUbl2_sjCk/?igsh=NWs0dmxuNWRiejdw

13/08/2026

Mapya Yaibuka Tukio la Mama Gift.

Mapya yameibuka kuhusu tukio la mwanamke anayedaiwa kufanya vitendo vya ushirikina katika Kitongoji cha Mbugani, Kijiji cha Magugu, wilayani Babati, mkoani Manyara.

Mwenye nyumba ambako mwanamke huyo, Mama Gift, alidaiwa kukutwa usiku, amesimulia tukio hilo na kusema kuwa Mama Gift ni jirani yake ambaye mara kwa mara alikuwa akimtembelea nyumbani kwake na walikuwa wakishirikiana hata kula pamoja.

*Sillo Awatembelea Vijana Zaidi ya 100 Wanaopata Mafunzo ya Mgambo Ayalagaya* Mbunge wa Jimbo la Babati Vijijini na Naib...
13/08/2026

*Sillo Awatembelea Vijana Zaidi ya 100 Wanaopata Mafunzo ya Mgambo Ayalagaya*

Mbunge wa Jimbo la Babati Vijijini na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Daniel Sillo, amewatembelea vijana zaidi ya 100 wanaopata mafunzo ya Jeshi la Akiba (Mgambo) katika Kata ya Ayalagaya, wilayani Babati.

Akizungumza na vijana hao, Sillo amewataka kuwa watulivu na kutumia vizuri kipindi cha mafunzo wanachopitia, akisisitiza umuhimu wa kuwa wazalendo na kutumia ujuzi watakaoupata katika kulinda amani na usalama katika maeneo yao na Taifa kwa ujumla.

Sillo amesema vijana ni sehemu muhimu katika ulinzi na usalama wa nchi, hivyo amewataka kuzingatia mafunzo, nidhamu na maelekezo wanayopewa na wakufunzi wao.

Aidha, Sillo amekabidhi mipira miwili kwa vijana hao, ambayo watatumia kufanya mazoezi ya michezo baada ya kukamilisha mafunzo yao ya kila siku.

Amesema michezo ni muhimu kwa afya ya mwili na akili, hivyo amewataka vijana hao kutumia muda wao wa mapumziko kufanya shughuli za michezo na kuendeleza mshikamano miongoni mwao.

13/08/2026

TAHARUKI MAGUGU: Mwanamke Akutwa Uchi Nyumbani kwa Jirani.

Sillo Amtembelea Mama Aliyeibiwa Mtoto Mchanga Dareda KatiMbunge wa Jimbo la Babati Vijijini na Naibu Spika wa Bunge la ...
13/08/2026

Sillo Amtembelea Mama Aliyeibiwa Mtoto Mchanga Dareda Kati

Mbunge wa Jimbo la Babati Vijijini na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Daniel Sillo, amemtembelea mama aliyeibiwa mtoto wake mchanga muda mfupi baada ya kujifungua katika Kituo cha Afya Dareda Kati, wilayani Babati, Agosti 8, 2026.

Sillo amempa pole mama huyo na kumfariji katika kipindi hiki kigumu anachopitia, huku akimpa moyo na kumtaka kuendelea kuwa na matumaini wakati juhudi za kumtafuta mtoto huyo zikiendelea.

Aidha, Sillo amewapongeza madaktari pamoja na Mganga Mkuu wa Mkoa na Mganga Mkuu wa Wilaya kwa kuendelea kuwa karibu na familia hiyo na kutoa ushirikiano katika kipindi hiki kigumu.

Amesema ni muhimu familia hiyo kuendelea kupata faraja na msaada kutoka kwa viongozi, wataalamu wa afya pamoja na jamii wakati hatua mbalimbali zikichukuliwa kufuatilia tukio hilo na kuhakikisha mtoto anapatikana.

Mtoto huyo alidaiwa kutoweka muda mfupi baada ya mama yake kujifungua katika kituo hicho cha afya, huku hadi sasa familia ikiendelea kusubiri taarifa za kupatikana kwake.

Sillo Azindua Miradi ya Maendeleo yenye Thamani ya Zaidi ya Milioni 370 Babati VijijiniNaibu Spika wa Bunge la Jamhuri y...
13/08/2026

Sillo Azindua Miradi ya Maendeleo yenye Thamani ya Zaidi ya Milioni 370 Babati Vijijini

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Jimbo la Babati Vijijini, Daniel Sillo, amezindua miradi mbalimbali ya maendeleo katika Kata ya Arri, wilayani Babati, ikiwemo vyoo katika Shule za Msingi Arri na Endasago pamoja na Jengo la Wazazi katika Zahanati ya Kijiji cha Ariitsaayo.

Miradi hiyo imejengwa kwa ushirikiano kati ya wananchi na Karim Foundation International, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuboresha huduma za elimu na afya katika maeneo ya vijijini.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa, miradi hiyo imegharimu zaidi ya Shilingi milioni 370, ambapo Shule ya Msingi Endasago imetumia Shilingi milioni 118.297, Shule ya Msingi Arri takribani Shilingi milioni 129, huku Jengo la Wazazi katika Zahanati ya Ariitsaayo likigharimu Shilingi milioni 123.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa miradi hiyo, Sillo ameipongeza Serikali kwa kuweka mazingira wezeshi yanayowavutia wadau mbalimbali wa maendeleo kushirikiana na Serikali katika kuwekeza kwenye sekta muhimu zikiwemo elimu na afya.

Amesema ushirikiano kati ya Serikali, wananchi na mashirika ya maendeleo ni muhimu katika kuongeza kasi ya utekelezaji wa miradi na kuboresha huduma zinazotolewa kwa wananchi.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkazi wa Karim Foundation International, Shau Erro, amesema shirika hilo litaendelea kushirikiana na Serikali katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo na kuunga mkono utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Naye Diwani wa Kata ya Arri, Paul Masong, amelishukuru Karim Foundation International kwa kuendelea kushirikiana na wananchi na kujenga miradi hiyo muhimu katika Kata ya Arri, akisema miradi hiyo itasaidia kuboresha huduma za kijamii kwa wananchi.

MKURUGENZI MKUU RUWASA AKAGUA MRADI WA MAJI USHETU Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa maji na usafi wa Mazingira Vijijini (RUW...
13/08/2026

MKURUGENZI MKUU RUWASA AKAGUA MRADI WA MAJI USHETU

Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa maji na usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Mhandisi Wolta Kirita amefanya ziara ya kukagua mradi wa maji wa Ushetu - Ulowa uliopo Halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama na kujionea maendeleo ya mradi huo.

Mkurugenzi Mkuu akiambatana na baadhi ya timu ya menejimenti kutoka RUWASA makao makuu,Meneja wa RUWASA Mkoa wa Shinyanga,Meneja wa RUWASA Wilaya ya Kahama pamoja na wasimamizi wa mradi walitembelea mradi huo kutoka Kahama kuelekea Kata ya Mlowa.

Akitoa maelezo kwa Mkurugenzi Mkuu wa RUWASA Meneja mradi Mhandisi John Msengi amesema hadi sasa mradi unaendelea vizuri na kwa sasa mradi upo katika hatua nzuri kwani mabomba na matanki ya vijiji vyote yamekamilika na kazi kazi iliyobaki ni bomba kuu pekee ili wananchi waweze kupata huduma ya maji.

Kwa upande wa Meneja wa RUWASA Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Julieth Payovela amemhakikishia Mkurugenzi Mkuu kuwa mara tu mradi huo kukamilika pamoja na kuhudumia kata ya Mlowa pia utaweza kuhudumia kata nyingine kumi zilizopo njiani kuelekea kata ya Mlowa.

Akihitimisha ziara hiyo Mkurugenzi Mkuu wa RUWASA ameitaka kampuni iliyopewa kazi ya kujenga mradi huo ikamilishe kazi hiyo mapema ili wananchi waweze kupata maji kwani lengo kuu ni kuhakikisha huduma ya maji inapatikana.

"Mambo ambayo tumekubaliana na Mkandarasi wa mradi ni kuhakikisha huduma ya maji inapatikana mapema na itasaidia kulinda miundombinu, na hii itasaidia kijiji cha jirani wakiona wenzao wanapata maji basi na wao wanakuwa na uhakika wa kupata maji" Alisisitiza Mhandisi Kirita.

Akiongea kwa niaba ya Wananchi wa Kata ya Ulowa kijiji cha Ulowa namba mbili Bi.Martha Simon Philipo ametoa shukurani zake kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan kupitia RUWASA kwa kuwaletea maji katika kijiji chao kwani kabla ya ujio wa mradi huo wananchi walisumbuka sana kupata huduma ya maji.

Mradi huo unatekelezwa na Kampuni ya ndani inayoitwa SIHOTECH Engineering Company Limited kwa kushirikiana na Mponela Construction and Company Limited, kwa gharama ya Shilingi 37,518,548,032.35.

12/08/2026

Address

Manyara

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Walter Habari Tanzania. posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to Walter Habari Tanzania.:

Shortcuts

Share