Embassy of Peace Association

Embassy of Peace Association We are the one who deal with peace making

UNAPOENDESHA GARI MAMBO MATATU YANAWEZA KUKUTOKEA NA KUSABABISHA AJALIMambo hayo ni:1. KUONDOA MACHO BARABARANIYaani kua...
26/02/2023

UNAPOENDESHA GARI MAMBO MATATU YANAWEZA KUKUTOKEA NA KUSABABISHA AJALI

Mambo hayo ni:
1. KUONDOA MACHO BARABARANI
Yaani kuangalia upande mwingine kandoni au nje ya barabara au nyuma kwa muda fulani. Mfano, kugeuka kusemezana na abiria, kumwangalia msichana fulani mrembo nje ya gari, kumwangalia abiria wa k**e aliyevaa nguo fupi na kukaa siti ya upande wa kushoto mwa dereva, kushangaa jambo fulani nje ya gari kwa sekunde kadhaa.

2. KUONDOA MIKONO KWENYE USUKANI
Inaweza kutokea ukawa unaongea na mtu kwa mikono ukiirusha, kuongea na simu, kushangilia au kuhamaki kwa hasira, nk

3. KUHAMISHA AKILI/MAWAZO YAKO BARABARANI.
Yaani unaendesha gari upo pale kimwili lakini kiakili ni k**a upo ndotoni. Haupo pale kabisaa, sababu ya msongo wa mawazo au kuwaza jambo lolote nje ya pale ulipo. Mfano, unaenda kwenye usaili wa kazi, akili yako inawaza sijui maswali yatakuwaje, sijui watanikubali kweli, sijui ntakumbuka nilivyosoma nk. Unaweza pia ukawa unamuwazia mtu fulani hadi unajikuta unatabasamu peke yako au kuongea peke yako. Unaweza kuwa unawazia aibu au fedheha fulani iliyokupata huko nyuma. Hali hii inaweza kufanya uendeshe gari kilomita nyingi tu bila kujitambua. Mwili utaendesha gari k**a kawaida lakini akili haipo pale, kinachoongoza pale ni kumbukumbu iliyohifadhiwa (reflex memory) tu.

Haya yote ndo yanaunda kitu kinachoitwa DISTRACTED DRIVING, ikitokea dharura unashindwa kabisa kukabiliana nayo kwa haraka, yaani reaction time inachelewa. Hadi uzinduke huko usingizini ndo uweze kuchukua hatua. Au unakumbwa na kigugumizi uache simu idondoke ipasuke unag'ang'ania usukani au uokoe vyote kwa pamoja.

Ndio sababu unaambiwa unapoendesha gari usiruhusu bughudha zinazoweza kukuondolea umakini barabarani.

RSAadmin1
RSA Tanzania
Usalama Barabarani ni Jukumu Letu Sote

Address

Magomeni

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Embassy of Peace Association posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to Embassy of Peace Association:

Share