Youth Peace Makers Tanzania

Youth Peace Makers  Tanzania The Lushoto based subsector of Y Global with motto "Stop Poverty" aiming to empower, advocate and lobby for citizen participation.

10/06/2026
MAADHIMISHO YA SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI LUSHOTO YAIBUA WITO WA TANZANIA YA KIJANI IFIKAPO 2050Maadhimisho ya Siku ya Ma...
08/06/2026

MAADHIMISHO YA SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI LUSHOTO YAIBUA WITO WA TANZANIA YA KIJANI IFIKAPO 2050

Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani yaliyofanyika katika eneo la Manolo, Wilaya ya Lushoto, yamebeba ujumbe mzito wa kuwajibika katika uhifadhi wa mazingira kupitia kaulimbiu isemayo “Dira 2050: Tuwajibike Kukijanisha Tanzania.”

Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Lushoto aliyewakilishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto, Bi. Ikupa Mwasyoge. Maadhimisho hayo yaliwakutanisha wanafunzi kutoka Shule za Sekondari Nywelo na Shume, vikundi vya afya na mazingira, wananchi, wadau wa mazingira pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali za mitaa.

Kwa kipindi cha tarehe 2 hadi 5 Juni, shughuli mbalimbali zilifanyika ikiwa ni sehemu ya Wiki ya Mazingira. Tarehe 3 Juni wananchi walishiriki zoezi la usafi katika maeneo ya Maguzoni na Halmashauri, huku tarehe 4 Juni elimu kuhusu uhifadhi wa mazingira na matumizi ya nishati safi ikitolewa kwa wananchi na washiriki mbalimbali.

Kilele cha maadhimisho kilifanyika tarehe 5 Juni ambapo shughuli mbalimbali zilifanyika ikiwemo gwaride, igizo lenye ujumbe wa utunzaji wa mazingira, upandaji wa miti, usomaji wa risala pamoja na hotuba kutoka kwa viongozi mbalimbali.

Akizungumza katika maadhimisho hayo, Bi. Ikupa Mwasyoge alipongeza juhudi zinazofanywa na Halmashauri, vikundi vya mazingira, wadau pamoja na wananchi katika kuhamasisha utunzaji wa mazingira na matumizi ya nishati safi.

“Jukumu la kutunza mazingira ni la kila mwananchi. Ni muhimu kuendelea kuzingatia kauli mbiu ya ‘Kata mti, panda mti’ ili kuhakikisha tunalinda mazingira yetu kwa kizazi cha sasa na kijacho,” alisema Bi. Ikupa.

Aidha, aliwataka wakulima na wafugaji kulinda vyanzo vya maji kwa kuepuka shughuli zinazoweza kuharibu mazingira, huku akisisitiza kuwa kila Halmashauri inapaswa kuhakikisha inapanda miti milioni 1.5 k**a sehemu ya juhudi za kitaifa za uhifadhi wa mazingira.

Katika maadhimisho hayo pia ilielezwa kuwa taasisi 15 tayari zimehamia katika matumizi ya nishati safi, hatua inayotajwa kuwa sehemu muhimu ya kupunguza uharibifu wa mazingira na matumizi ya nishati zisizo rafiki kwa mazingira.

Mbali na elimu na hamasa zilizotolewa, maadhimisho hayo yalihusisha ugawaji wa mitungi ya gesi kwa vikundi vya mazingira, vyeti vya kutambua mchango wa wadau mbalimbali pamoja na miche ya miti kwa taasisi na vikundi mbalimbali. Miongoni mwa walionufaika ni Yogoi, Nywelo Sekondari, Mkuki, Kutoja pamoja na wadau kutoka TFS.

Washiriki wa maadhimisho hayo walikubaliana kuendelea kushirikiana katika kutunza mazingira, kuongeza matumizi ya nishati safi, kupunguza matumizi ya plastiki na kuhamasisha matumizi ya mbadala zake ili kuhakikisha Tanzania inakuwa ya kijani na salama zaidi kuelekea Dira ya 2050.

Kwa pamoja walisisitiza ujumbe wa maendeleo endelevu unaosema, “Tushik**ane kwa pamoja kuleta maendeleo; Tanzania ni yetu sote.”

Kwa siku tatu mfululizo, kuanzia tarehe 21–23 Mei 2026, vijana, viongozi wa jamii, wadau wa michezo na wanajamii walikut...
25/05/2026

Kwa siku tatu mfululizo, kuanzia tarehe 21–23 Mei 2026, vijana, viongozi wa jamii, wadau wa michezo na wanajamii walikutana katika programu ya michezo kwa maendeleo iliyoandaliwa na YPM kwa kushirikiana na Legal Vision Organisation (LEVO) pamoja na Deutsche Gesellschaft für Internationale Zusammenarbeit (GIZ) Tanzania, ikiwa na lengo la kupaza sauti dhidi ya ukatili wa kijinsia kupitia nguvu ya michezo.
Safari hiyo ilianza siku ya kwanza kwa semina na mijadala iliyogusa maisha ya wengi, ambapo washiriki walijadili kwa kina kuhusu ukatili wa kijinsia, athari zake na namna jamii inaweza kushirikiana kuutokomeza.
Siku ya pili, nguvu ya michezo ilichukua nafasi yake kupitia semina ya michezo kwa maendeleo. Washiriki walijifunza kuwa michezo si ushindani pekee, bali pia ni darasa la maisha. Walijadili namna sessions za michezo zinaweza kutumika kufundisha usalama, heshima, usawa na kuhamasisha jamii kupinga ukatili wa kijinsia.
Aidha moja ya matukio yaliyowagusa wengi zaidi ilikuwa ni igizo lililoonesha namna rushwa na matumizi mabaya ya mamlaka yanavyoweza kupindisha haki za waathirika wa ukatili wa kijinsia. Kupitia igizo hilo, washiriki waliona namna vitendo hivyo vinavyorudisha nyuma harakati za jamii katika mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia na kuathiri imani ya waathirika katika mifumo ya haki. Wanajamii walijawa na hisia, tafakari na mazungumzo ya kina juu ya wajibu wa jamii katika kuhakikisha haki inapatikana kwa usawa.
Katika kuthamini mchango wa michezo kuileta pamoja jamii, bonanza lenye lengo la kufikisha ujumbe wa kupinga ukatili wa kijinsia lilifanyika na timu kumi nan ne (14) zilishiriki na kutazamwa na watu zaidi ya 500 ambao walipata mafunzo ya namna ya kukabili ukatili wa kijinsia kabla ya bonanza kuanza
Kupitia michezo, elimu na mazungumzo ya wazi, YPM, LEVO na GIZ Tanzania wanaendelea kuthibitisha kuwa mabadiliko ya kweli yanaanza pale jamii inapoungana na kuchukua hatua.

Youth voices belong in spaces where decisions are made.Youth Peacemakers Tanzania (YPM) is proud to have supported 5 you...
22/05/2026

Youth voices belong in spaces where decisions are made.

Youth Peacemakers Tanzania (YPM) is proud to have supported 5 young leaders to participate in the Tanzania International Model United Nations (TIMUN), a platform that brings together youth to discuss global challenges, diplomacy, leadership, and sustainable solutions.

As part of this experience, one of our delegates also had the opportunity to visit the Parliament of Zanzibar, gaining first-hand exposure to governance, policy making, and leadership processes.

At YPM, we believe that exposing young people to conferences, summits, and leadership platforms is essential in shaping informed, confident, and active citizens. These opportunities allow youth to:
🔹 Build leadership and diplomacy skills
🔹 Exchange ideas with fellow young leaders
🔹 Gain global and national perspectives
🔹 Strengthen confidence and public speaking
🔹 Become changemakers within their communities

Investing in youth participation today means building stronger leaders for tomorrow. 🌱

As part of bringing mental health awareness closer to the community, today our SRHE Advisory, Debora Kamitanjin, held an...
15/05/2026

As part of bringing mental health awareness closer to the community, today our SRHE Advisory, Debora Kamitanjin, held an engaging session at Prince Claus, focusing on the importance of mental well-being, open conversations, and creating supportive spaces for young people. 🧠💚

Together, we continue to break the stigma around mental health and encourage communities to prioritize emotional and psychological well-being.

Kuelekea maadhimisho ya Siku ya Hedhi Duniani, YPM tumepata wasaa wa kuungana na shirika la  kwa kutembelea Shule ya Sek...
14/05/2026

Kuelekea maadhimisho ya Siku ya Hedhi Duniani, YPM tumepata wasaa wa kuungana na shirika la kwa kutembelea Shule ya Sekondari Masange Juu kwa ajili ya zoezi la ugawaji wa pedi zinazoweza kutumika zaidi ya mara moja kwa wanafunzi 301.

Lakini pia wanafunzi wamepata elimu kuhusu matumizi ya njia mbalimbali za kujisitiri kipindi cha hedhi ikiwemo tampon, kikombe cha hedhi pamoja na pedi za kutumia mara moja, ikiwa ni sehemu ya kuongeza uelewa na kuwajengea uwezo wa kufanya uchaguzi sahihi kuhusu afya ya hedhi.

Zoezi hili limeendelea kuhamasisha afya ya hedhi, kuondoa unyanyapaa na kuhakikisha wasichana wanapata mazingira bora ya kujifunzia kwa kujiamini zaidi. 💜

Katika kuendelea kuhamasisha afya bora kwa jamii, leo tumepata nafasi ya kushirikiana na Dr. Omary kutoka Hospitali ya W...
14/05/2026

Katika kuendelea kuhamasisha afya bora kwa jamii, leo tumepata nafasi ya kushirikiana na Dr. Omary kutoka Hospitali ya Wilaya ya Lushoto ambaye ametoa elimu ya afya kwa vijana wa Chuo cha KOTETI kuhusu kujikinga na magonjwa ya zinaa.

Kupitia elimu hii, vijana wamepata maarifa muhimu yatakayowasaidia kulinda afya zao na kujenga maisha bora ya baadaye.

Tumepata bahati ya kutembelewa na wawakilishi kutoka Wizara ya Afya kupitia Idara ya Kutokomeza Malaria kwa ajili ya kuj...
14/05/2026

Tumepata bahati ya kutembelewa na wawakilishi kutoka Wizara ya Afya kupitia Idara ya Kutokomeza Malaria kwa ajili ya kujadili na kuimarisha mpango mkakati wa kutokomeza mazalia ya mbu katika jamii.

Ziara hii imekuwa fursa muhimu ya kubadilishana uzoefu, kujenga ushirikiano na kuendelea kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa mazingira safi katika mapambano dhidi ya malaria.

Pamoja tunaweza kutokomeza malaria! 🦟💚

"Wapendwa Wafanyakazi YPM Hongereni kwa siku kubwa ya Wafanyakazi Jitihada na muda wenu ni mchango mkubwa wa thamani na ...
01/05/2026

"Wapendwa Wafanyakazi YPM
Hongereni kwa siku kubwa ya Wafanyakazi
Jitihada na muda wenu ni mchango mkubwa wa thamani na kuheshimika kwa YPM, Jamii ya wadau wa ndani na nje na Taifa letu.

Daima kwa Umoja tutafika mbali.

Happy Workers Day 2026."
Rev. Godfrey T Walalaze
Director YPM

Address

Peacemakers Road
Lushoto
21701

Opening Hours

Monday 08:30 - 17:00
Tuesday 08:30 - 17:00
Wednesday 08:30 - 17:00
Thursday 08:30 - 17:00
Friday 09:00 - 17:00

Telephone

+255272660017

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Youth Peace Makers Tanzania posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share