16/12/2025
*Wapendwa Katika Bwana* .
Ninapenda niwashukuru sana wote
1. Mliofika kwa kikao Cha leo na
2. Mliotoa taarifa ya kutofika kwa sababu mbalimbali
Mambo yaliyojadiliwa ni:-
1. *Barua ya kuwaomba ufadhili wa vifaa*
🤝Wajumbe walipokea na kukubaliana na bajeti iliyoandaliwa na wakakubaliana kuwa *MAJINA YA WATU* watakaotusaidia kupata hivyo vifaa yawasilishwe kwa Mkurugenzi ili waandikiwe barua rasmi kuombwa kusaidia.
2. *Bajeti ya vifaa*
🌻Bajeti hii Wajumbe walikubaliana kuwa ndio iwe mwongozo kwa ajili ya kukusanya vifaa vya shule.
3. *Sherehe ya pamoja na watu wenye Ualbino*
🙏 Mkurugenzi aliwasilisha mada hii kwamba inahitajika bajeti ya chakula na nauli kwa watu wenye Ualbino Wilaya ya Iramba na kusema tayari amewasilisha ombi kwa Mkuu wa Mkoa la kuomba ufadhili wa bajeti hiyo.
4. *Vikao vya kawaida.*
👍Wajumbe waliomba tuwe na vikao, sio mpaka kusubiri matukio. Na kwa hili tumekubaliana kuwa tutakuwa na Kikao *Kila weekend ya mwisho ya mwezi*
5. *Uongozi wa Shirika*
Wajumbe waliuliza k**a Kuna Uongozi wa Shirika ama la. Mkurugenzi aliwahabarisha Wajumbe kuwa ni kweli Shirika Lina Uongozi.
Ambae ni:-
1. *Mkurugenzi Mkuu*
2. *Katibu Mkuu* na
3. *Mhasibu*
Ingawaje kiukweli kwenye kipengele Cha mhasibu tunatakiwa tufanye namna.
Pia Mkurugenzi aliwaomba Wajumbe kwamba wajiandae kwa uchaguzi kwani tunatakiwa tuwe na MWENYEKITI ambae yeye atahusika kusimamia na kuendesha vikao vyote vya shirika hata k**a Mkurugenzi hayupo. Hivyo tujiandae.
6. Kiingilio Cha Shirika
Wajumbe waliuliza namna ya kujiunga na shirika. Mkurugenzi aliwaeleza Wajumbe kuwa kwa kuwa hili ni Shirika la kusaidia wenye uhitaji na sio biashara, hivyo *HAKUNA KIINGILIO* . Sifa kuu ya mwanachama wa Shirika hili ni *MOYO WAKE WA KUJITOA NA KUJITOLEA* Kwa hiari yake. Na alisema " *Shirika hili si la Kidini, si la kisiasa Wala la kikabila* " Na tunafanye ama kuhudumia Tanzania Bara
7. Namna ya kushiriki kwenye bajeti hii.
Mkurugenzi aliwaeleza wajumbe kwa kuwa Kila mmoja aliyepo hapa ni mwanachama na aliingia hapa kwa moyo wake wa kupenda kusaidia Yatima basi *KILA MTU ATOE KADRI MUNGU ATAKAVYOMGUSA* .
Namna ya kuwasilisha mchango wako....
Kwa vitu wasiliana nami ama Katibu Miriam.
Kwa fedha tumia njia hii:-
1. LIPA namba M-PESA *37416286* Jina: SAMSON BENARD MPINGA
2. N.M.B A/C NO. *50610026325*
JINA: *SABE HELPING FOUNDATION*
MUNGU ibariki TANZANIA
MUNGU ibariki SAHEFO
MUNGU atubariki Sisi sote amen...
Ndimi,
*EV. Samson B Mpinga*
MKURUGENZI WA SHIRIKA
Samson Benard Mpinga Agnes Jacob Janeth Tullo Tuseme Ukweli Juu Ya Mambo Yote Evangelist Samson Ugula