MARAFIKI WA KWELI TANZANIA

MARAFIKI WA KWELI TANZANIA JAMBO MARAFIKI WA KWELI TANZANIA? hii ni page ya kuwaweka marafiki karibu na kuwapa news of daily life and advices,please like it NOW. MUNGU akubariki sana

Abeid Karume aliuawa kwa kipigwa Risasi Tarehe 7/4/1972Risasi nane zilitolewa mwilini kwake mwili wake ulipofikishwa kwe...
26/05/2026

Abeid Karume aliuawa kwa kipigwa Risasi Tarehe 7/4/1972

Risasi nane zilitolewa mwilini kwake mwili wake ulipofikishwa kwenye Hospitali ya V. I. Lemin, mjini Unguja kwa uchunguzi,
Sawa na idadi ya miaka minane ya utawala wake tangu 1964 hadi kifo chake.

TUKIO LENYEWE LILIKUA HIVI;-

Rais Karume na Makomredi wenzake wa Chama cha Afro-Shirazi (ASP) alikuwa na mazoea ya kucheza karata, dama au dhumuna kwenye ukumbi wa ofisi za makao makuu ya Chama hicho Kisiwandui, kila jioni k**a sehemu ya mapumziko.

Siku hiyo alifika saa 11.00 jioni akiwa na walinzi wake, akaingia ndani nao wakabaki nje kulinda.

Ikafika zamu yake kucheza;-akawa anacheza na Mzee Maalim Shaha Kombo ambaye alionekana kulemewa.

Ndipo Karume akamwita Mzee Mtoro Rehani ajitayarishe baada ya Kombo, naye akaitikia kwa kuaga kwanza aende msalani kujisaidia.
Sekunde chache baada ya hapo na kabla Mzee Mtoro Rehani hajarejea kutoka msalani, ghafla watu wawili wenye silaha walivamia chumba alimokuwa Karume na wenzake na kumimina risasi wakimlenga mzee karume.

Kufumba na kufumbua mzee karume akawa katika dimbwi la damu kimya, amepoteza uhai.

Hakuna mtu mwingine aliyeuawa mbali na kujeruhiwa tu, mmoja wao akiwa Katibu Mkuu wa ASP, (sasa) Hayati Thabit Kombo Jecha.
Risasi uaji (the fatal bullet), mbali ya risasi zote, iliyochukua uhai wa Karume ilitoka kwenye bunduki ya Luteni Hamoud Mohammed Hamoud wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWT), ambaye ndiye alikuwa kiongozi wa uvamizi huu na aliyefyatua risasi ya kwanza wakati Karume akicheza na wenzake.

Inasemekana, Hamoud aliuawa papo hapo na mlinzi wa Karume.

Wauaji wengine waliofuatana na Hamoud katika uvamizi huo ni Kapteni Ahmada Mohamed, Koplo mmoja wa jeshi ambaye jina lake halijafahamika hadi leo, na raia mmoja aliyetambulika kwa jina la Ali Khatibu Chwaya, ambao inaelezwa wote hao waliuawa kwenye mapambano ya silaha nje ya eneo la tukio.

Dakika chache baada ya mauaji kutokea, alifika Kanali Ali Mahfoudhi na askari mwingine, Kapteni Makame Hamis, wakauchukua mwili wa Karume na kuukimbiza hospitali.

Kanali Mahfoudhi alikua ni mmoja wa vijana wa Umma Party (UP) cha Abdulrahman Mohamed Babu, kilichoungana na ASP baada ya Mapinduzi ya Januari 12, 1964 na kuunda Serikali ya mseto.

Ni kati ya vijana waliopelekwa Cuba kwa mafunzo ya kijeshi, na ni mmoja wa wapiganaji walioendesha mapambano ya kisayansi usiku wa Mapinduzi na kuk**ata uwanja wa ndege mchana Aprili, 1972.

Ni mmoja wa wanaharakati wa siasa za mrengo wa Kikomunisti ambao hawakutakiwa Zanzibar wakati wa utawala wa Karume,
kufuatia Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Aprili 26, 1964, Karume alishinikiza kwa Nyerere wapewe kazi Tanzania Bara aweze “kupumua” ambapo Mahfoudhi alipewa cheo cha Mkurugenzi wa Operesheni katika JWT.

Wengine ambao hawakutakiwa ni pamoja na Babu mwenyewe aliyepewa Uwaziri wa Mipango ya Uchumi, hasimu mwingine wa Karume, Othman Sharrif, ambaye alifanywa Afisa Mifugo wa Mkoa, Mtwara, na Balozi Salim Ahmed Salim wakati huo Balozi wa Zanzibar nchini Misri ikaridhiwa aendelee kuwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano nchini humo.

Kuna dhana mbili kinzani kuhusu jinsi Karume alivyouawa na hatima ya wauaji.

Dhana moja inadai kwamba, watu wanne walivamia mahali alipokuwa Karume na wenzake, wakamimina risasi mara nne au mara tano hivi, risasi ya kifo ikampata Karume shingoni akafa, huku zingine zikiendelea kumiminwa kulenga meza walipokuwa.

Inadaiwa kuwa Hamoud aliuawa kwenye eneo la tukio, ambapo wawili waliuawa baadaye na vyombo vya usalama (kwa mapambano?) na mmoja alijiua.

Dhana ya pili inadai kwamba Hamoud alikufa kwenye eneo la tukio katika mazingira ya kutatanisha, ama kwa kujipiga risasi kuepuka kuk**atwa hai na kuteswa baada ya kuona asingeweza kutoroka, au alijeruhiwa vibaya na walinzi wa Karume, kisha Ahmada akampiga risasi na kumuua kumwepusha kuteswa na kutoa siri k**a angek**atwa hai, kisha (Ahmada) akaweza kutoroka kwenye eneo la tukio.

Kufuatia mauaji hayo, watu 1,100 walik**atwa na kuhojiwa juu ya kuhusika au kutohusika kwao na mauaji, wengi wakiwa viongozi na wanachama wa zamani wa Umma Party. Chama cha Babu na wanachama mashuhuri wa ASP wenye siasa za mrengo wa kikomunist.
Mungu ailaze roho ya marehemu mpendwa wetu Muheshimiwa Abeid Karume Mahala pema peponi. Amina.

21/05/2026
21/05/2026

MZEE ASIMULIA MAMBO MUHIMU

TOGO YAONDOA VIZA KWA WAAFRIKA WOTESerikali ya Togo imetangaza kuwa kuanzia Jumatatu, raia wote wa Afrika wenye pasi hal...
20/05/2026

TOGO YAONDOA VIZA KWA WAAFRIKA WOTE

Serikali ya Togo imetangaza kuwa kuanzia Jumatatu, raia wote wa Afrika wenye pasi halali hawatahitajika tena kuwa na viza ili kuingia nchini humo.

Kwa mujibu wa taarifa ya Wizara ya Usalama, Waafrika wataweza kuingia Togo bila viza na kukaa kwa muda wa hadi siku 30.

Serikali ya Togo imesema hatua hiyo inalenga kufungua zaidi nchi hiyo kwa wawekezaji na wageni, kukuza maendeleo ya kiuchumi, pamoja na kuifanya Togo kuwa kitovu cha kikanda cha huduma, biashara, utamaduni na mahusiano ya watu.

Wizara hiyo pia imeeleza kuwa uamuzi huo unaendana na maadili ya mshik**ano wa Kiafrika na kurahisisha usafiri wa Waafrika ndani ya bara lao.

Hata hivyo, Waafrika wanaopanga kusafiri kwenda Togo watalazimika kujisajili kwenye tovuti ya Serikali inayohusika na safari angalau saa 24 kabla ya kuwasili nchini humo ili wapatiwe kibali cha kusafiri.

Togo sasa imejiunga na Mataifa mengine ya Afrika yaliyokwisha kuondoa viza kwa Waafrika, yakiwemo Rwanda, Ghana, Benin, Seychelles na Gambia.

Balthazar Egonga ameachiwa huru kutoka gerezani baada ya miaka 2. Wanawake nchini Equatorial Guinea na sehemu mbalimbali...
20/05/2026

Balthazar Egonga
ameachiwa huru kutoka gerezani baada ya miaka 2. Wanawake nchini Equatorial Guinea na sehemu mbalimbali za Afrika wanaonekana kusherehekea kuachiliwa kwake.

Balthazar alipata umaarufu mkubwa mtandaoni baada ya zaidi ya video 400 zake za “kula wanawake ” kusambaa kwa kasi. Wanawake wengi walivutiwa na “ustadi” wake wa kula noodles na wengine walikuwa tayari kumpa noodles zaidi. Leo ameachiwa rasmi na sasa ni mtu huru.

Address

Kinondoni

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when MARAFIKI WA KWELI TANZANIA posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share