06/03/2026
Historia ya Shule ya Msingi Vuje
Shule ya Msingi Vuje ni miongoni mwa taasisi za Elimu zenye historia ndefu na thamani kubwa katika eneo la Gonja vuje. Mwanzo wake ulitokana na jitihada na maono ya jamii ya wakati huo, iliyotambua umuhimu wa elimu kwa vizazi vijavyo.
Inasemekana kwamba shule hii ilianzia katika eneo la Mrungu, lililoko katikati ya mlima, mahali palipokuwa na mazingira tulivu na mazuri kwa kujifunza na kukusanyika kwa jamii. Mwanzo wa shule hii ulihusishwa kwa karibu na juhudi za Waislamu wa eneo hilo, hasa baada ya kuwasili kwa Shekh Jabiri kutoka Lamu, (Kenya) aliyelenga kueneza elimu pamoja na maadili mema ya kijamii na kidini.
Kupitia juhudi hizo na mshik**ano wa wakazi wa eneo hilo, wazo la kuanzisha shule lilipata nguvu. Hatimaye, Shule ya Msingi Vuje ikaanzishwa na kujengwa kwa mchango wa Waislamu wa Wilaya ya Same, wakati huo ambapo wilaya hiyo ilikuwa bado ni moja. Katika kipindi hicho, Mar. Mzee Selemani Rashidi Kinenekejo alihudumu kwa heshima kubwa k**a mkaguzi wa shule za Kiislamu Wilaya ya Same, akihakikisha elimu ilitolewa kwa viwango vinavyofaa na kuimarisha mashule ya wakati huo.
Lengo kuu lilikuwa kuwapa watoto wa eneo hilo fursa ya kupata elimu ya msingi, kuwajengea maarifa, nidhamu, na misingi ya maisha bora. Tangu wakati huo, shule hii imekuwa kitovu cha malezi na elimu kwa vizazi vingi vilivyopitia hapo, na baadaye kutoa mchango mkubwa katika jamii na taifa kwa ujumla.
Hadi leo, Shule ya Msingi Vuje inaendelea kubeba kumbukumbu na urithi wa historia hiyo adhimu historia ya mshik**ano, juhudi za jamii, na dhamira ya kuona elimu ikikua na kuendelea katika Gonja Vuje.
Chanzo: Mbaruku Yasini Kinenekejo
-AK
Je, wewe una kumbukumbu gani kuhusu Shule ya Msingi Vuje au historia yake? Karibu ushiriki nasi kwenye maoni.