Kigoma Region Tanzania

Kigoma Region Tanzania 'Jumuiya Ya Watu wa Kigoma'
Watu kutoka Mkoa wa Kigoma hukusanyika hapa ili kushiriki habari na kuungana na marafiki.
(2)

Kigoma inapatikana Magharibi mwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ukurasa wa Kijamii kwa watu wa Mkoa wa Kigoma ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mtandao wa kudhibiti Ujinga, Maradhi, Umasikini, kuinua Uchumi, Elimu, Vipaji, Fursa, Ajira, Kushiriki Habari na matukio, Haki na Usawa kwa watu wa mkoa wa Kigoma. Inajumuisha watu wote wanaoishi Kigoma na wenye asili ya mkoa wa Kigoma popote pale walipo.

02/06/2026

Video inaonyesha zoezi la kuinua na kuweka mashine ya kubebea Nanga ndani ya meli ya MV Liemba tayari kwa hatua za ufungaji na usanifu.

-Dar es Salaam Merchant Group

Kazi za ukarabati wa MV Liemba zinaendelea ambapo sasa zimehusisha ufungaji wa window wipers (vipangusa vioo). Vipangusa...
02/06/2026

Kazi za ukarabati wa MV Liemba zinaendelea ambapo sasa zimehusisha ufungaji wa window wipers (vipangusa vioo). Vipangusa vioo vya meli hutumika kusafisha maji ya mvua, mawimbi na ukungu kwenye vioo ili kuboresha mwonekano wakati wa safari.

-dmgfamily

Kazi za ukarabati wa meli zinaendelea, ikiwa ni pamoja na kufunga na kusanifu mashine ya kuvuta na kushusha nanga (windl...
02/06/2026

Kazi za ukarabati wa meli zinaendelea, ikiwa ni pamoja na kufunga na kusanifu mashine ya kuvuta na kushusha nanga (windlass winch). Kwenye meli, mnyororo wa nanga hupitia kwenye gurudumu maalum linaloitwa wildcat, ambalo hushika na kuongoza mnyororo huo kwa usalama wakati wa kuvuta au kushusha nanga nzito.

-dmgfamily

Baadhi ya wakazi wa kijiji cha Mganza wilayani Uvinza wameeleza wasiwasi kuhusu hali ya ofisi ya CCM inayodaiwa kutotumi...
02/06/2026

Baadhi ya wakazi wa kijiji cha Mganza wilayani Uvinza wameeleza wasiwasi kuhusu hali ya ofisi ya CCM inayodaiwa kutotumika kwa muda mrefu, hali iliyochangia kuharibika kwa jengo hilo. Wananchi wamezitaka mamlaka na viongozi wa chama kuchukua hatua za kulifufua au kulipatia matumizi yenye manufaa kwa jamii. Hata hivyo, madai ya kuwa jengo hilo limetelekezwa kutokana na ukosefu wa wanachama au kutumiwa na wahalifu hayajathibitishwa na mamlaka husika.
-Omary Maranda

01/06/2026

Watu wa Kasulu waahidi kuibwaga CCM kwenye uchaguzi ujao, Katibu wa k**ati ya mafunzo wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kanda ya Magharibi Mwalimu Rubibi Idrisa Kassim, jana tarehe 30 Mei 2026, amehutubia mkutano wa hadhara katika mji wa Kasulu mkoani Kigoma.

Wananchi wa mji wa Kasulu, walijitokeza kuchangia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) baada ya kumalizika kwa mkutano wa hadhara, uliyofanyika tarehe 30 Mei 2026, katika uwanja wa Kiganamo. Kiasi cha fedha kilicho patikana ni Tsh 353,000.

Shirika la Nature Tanzania kwa kushirikiana na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) limeendesha usiku wa ...
01/06/2026

Shirika la Nature Tanzania kwa kushirikiana na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) limeendesha usiku wa filamu za uhifadhi katika vijiji vya Kasisi na Chagu, wilayani Uvinza, mkoani Kigoma.

Tukio hilo lililenga kuongeza uelewa kuhusu umuhimu wa kulinda Eneo la Ramsar la Malagarasi-Moyowosi (MMRS). Kupitia filamu iliyoonesha mfano wa eneo la ardhioevu linalosimamiwa vizuri, wananchi na wadau walijifunza faida za mifumo hiyo ya ikolojia ikiwemo uhifadhi wa bioanuwai, usafishaji wa maji, kudhibiti mabadiliko ya tabianchi na kuimarisha maisha endelevu ya jamii.

Kwa kutumia filamu k**a nyenzo ya elimu ya mazingira, tukio hilo limehamasisha ushiriki wa jamii na kuimarisha dhamira ya kuhifadhi mazingira kwa muda mrefu, kwa kutambua kuwa mafanikio ya uhifadhi huanza pale jamii inapokuwa mstari wa mbele.

Bata mwenye mabawa yenye miiba (Spur-winged Goose) aonekana katika Eneo la Ramsar hapa Malagarasi-Moyowosi, Nguruka, Kig...
01/06/2026

Bata mwenye mabawa yenye miiba (Spur-winged Goose) aonekana katika Eneo la Ramsar hapa Malagarasi-Moyowosi, Nguruka, Kigoma.

Halmashauri ya Mji Kasulu imeibuka bingwa wa mpira wa miguu wavulana katika mashindano ya UMITASHUMTA 2026 ngazi ya Mkoa...
01/06/2026

Halmashauri ya Mji Kasulu imeibuka bingwa wa mpira wa miguu wavulana katika mashindano ya UMITASHUMTA 2026 ngazi ya Mkoa wa Kigoma.

-Simbeye

Mwanaume mwenye umri wa miaka 53, mkazi wa Kitahana Kibondo, amefariki dunia baada ya kujinyonga kwa kutumia kamba ya ch...
31/05/2026

Mwanaume mwenye umri wa miaka 53, mkazi wa Kitahana Kibondo, amefariki dunia baada ya kujinyonga kwa kutumia kamba ya chandarua. Mwili wake ulikutwa kwenye mti wa mwembe na watoto waliogundua tukio hilo. Viongozi wametoa wito kwa jamii kutoa taarifa za changamoto badala ya kuchukua uamuzi wa kujidhuru.
Omary Maranda

Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Buhigwe, Ndugu Laurenti Melkiory Kapimpiti, amewaapisha Makarani Waongozaji Wapiga Kura k...
31/05/2026

Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Buhigwe, Ndugu Laurenti Melkiory Kapimpiti, amewaapisha Makarani Waongozaji Wapiga Kura kiapo cha kutunza siri na kujitoa uanachama, huku akiwataka kuzingatia sheria, kanuni na maelekezo ya uchaguzi kuelekea uchaguzi mdogo wa Udiwani Kata ya Nyamugali utakaofanyika Juni 1, 2026.
Omary Maranda

Address

P. O. BOX 734, Kigoma District, Kigoma Town Ward, Shede Street, Bangwe & Stanley Road, House No: 02
Kigoma
47101

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Kigoma Region Tanzania posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to Kigoma Region Tanzania:

Share