Kigoma Elimu Foundation

Kigoma Elimu Foundation Kigoma Elimu Foundation Ni mfuko wa Elimu wa Hiari unaondeshwa na wenyeji wa Kigoma Ujiji kusaidia Elimu kwa wanafunzi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji

KIEF Joins Over 70 TEN/MET Members to Advance Gender Equality in EducationDar es Salaam | August 19, 2026KIEF was proud ...
21/08/2026

KIEF Joins Over 70 TEN/MET Members to Advance Gender Equality in Education

Dar es Salaam | August 19, 2026

KIEF was proud to join more than 70 TEN/MET members in Dar es Salaam on Wednesday for a training on Gender Awareness, Sensitivity and Responsiveness.

The session provided practical tools to better understand gender issues, address barriers to equality, and integrate gender-responsive approaches into programs, advocacy, and daily work.

This strong turnout shows a growing commitment among education stakeholders to move beyond discussion and take concrete steps toward a more inclusive and equitable education system in Tanzania.

In line with our commitment to inclusive education, KIEF will use the insights from this training to strengthen gender responsiveness in our own programs and support our partners to do the same.

We join TEN/MET and fellow members in turning the commitment to gender equality into action, in schools, in communities, and across the education system.

Leo Shirika la KIEF kwa kushirikiana na Kamati ya Ushauri wa Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano - TCRA CCC Mkoa wa Kigom...
05/08/2026

Leo Shirika la KIEF kwa kushirikiana na Kamati ya Ushauri wa Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano - TCRA CCC Mkoa wa Kigoma, tumetoa semina ya Stadi za Maisha katika Shule ya Msingi Kagera kwa Walimu na Wanafunzi.

Semina ililenga kujiepusha na matumizi ya vifaa vya mawasiliano vinavyoathiri maendeleo ya watoto, ikiwemo kutazama movie na tamthilia zisizo na maadili. Tulijadili athari zake kielimu na kimaadili, pamoja na njia za kutumia teknolojia kwa njia chanya.

Tunashukuru Uongozi wa Shule ya Msingi Kagera, Walimu na Wanafunzi wote kwa ushiriki wenu. Pamoja tuendelee kujenga vizazi vyenye maadili, nidhamu na matumizi sahihi ya teknolojia kwa maendeleo ya Taifa letu.

Shirika la   tumeshiriki mafunzo ya Ushiriki na Ushirikishwaji katika Michakato ya Kisera yanayofanyika hapa Dodoma na w...
16/06/2026

Shirika la tumeshiriki mafunzo ya Ushiriki na Ushirikishwaji katika Michakato ya Kisera yanayofanyika hapa Dodoma na wawakilishi 21 wa asasi mbalimbali za kiraia kutoka Tanzania Bara na Visiwani. Mafunzo haya yanaratibiwa kupitia programu ya Safeguarding Young People na yana lengo la kuangalia Michakato ya Sera hasa zinazowahusu vijana

Mafunzo haya yanalenga kuwajengea uwezo vijana na asasi za kiraia ili waweze kushiriki kikamilifu katika mchakato wa uundaji, utekelezaji na usimamizi wa sera zinazogusa maisha yao moja kwa moja hususan katika maeneo ya elimu, ajira, afya, mazingira, uongozi na usawa wa kijinsia

• Ushiriki wa vijana katika michakato ya kisera ni muhimu kwa sababu:
• Unatoa nafasi kwao kushiriki katika maamuzi yanayowahusu.
• Unachochea uwajibikaji na uwazi kwa viongozi na watoa maamuzi.
• Unawajengea vijana uelewa wa mifumo ya utawala na haki zao za kiraia.
• Unachangia kupatikana kwa sera jumuishi zinazozingatia mahitaji ya makundi yote, mijini na vijijini.
• Unaimarisha ushirikiano kati ya vijana, asasi za kiraia na serikali katika kufanikisha dira ya maendeleo ya taifa.

Vijana ni wabia wakubwa wa maendeleo na Tunaamini kuwa kuwezesha vijana kushiriki kikamilifu katika mchakato wa sera ni msingi wa kujenga jamii yenye haki, usawa na maendeleo

We don’t just attend sessions. We absorb, we question, we apply.  This photo is what the building looks like before the ...
11/06/2026

We don’t just attend sessions. We absorb, we question, we apply.
This photo is what the building looks like before the world sees the results.

At Kigoma Elimu Foundation, we believe real change starts in rooms like this. Young minds, open notebooks, full focus. Because policy, education, and community development are not built by accident. They are written, debated, and shaped by the people who show up.

Every pen moving here is a future policy drafted. Every idea shared here is a life that could change tomorrow.

This is the work. This is the movement. And this is only the beginning.

To every youth reading this: the tables are open. Will you pull up a chair?

Drop a comment if you believe in learning that leads to action.

Leo tarehe 26 Mei 2026, KIEF kwa kushirikiana na wanachama wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TeNMeT) tumekutana Sea Shells H...
27/05/2026

Leo tarehe 26 Mei 2026, KIEF kwa kushirikiana na wanachama wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TeNMeT) tumekutana Sea Shells Hotel, Millennium Tower, Dar es Salaam kwa kikao cha Community of Practice (CoP).

Mada Kuu ilikuwa ni: Changamoto za Mabadiliko ya Tabia ya Nchi katika Sekta ya Elimu nchini Tanzania.

Kikao hiki cha CoP kimewaleta pamoja wataalamu na wadau wa elimu kujadili kwa kina jinsi mabadiliko ya tabia ya nchi yanavyoathiri upatikanaji wa elimu bora miundombinu kuharibiwa na mafuriko, ratiba za masomo kuvurugika, na usalama wa chakula mashuleni.

Hatua zinazofuata: Kukamilisha ripoti ya research na kuandaa mapendekezo ya Action Plan kwa ajili ya wadau wa elimu nchini.

Elimu himilivu dhidi ya mabadiliko ya tabia ya nchi inawezekana kupitia ushirikiano.

DarEsSalaam

Tumeshiriki Kikao cha Robo Mwaka cha NGOs KigomaLeo KIEF tumeshiriki kikao cha robo mwaka cha NGOs kilichofanyika katika...
20/05/2026

Tumeshiriki Kikao cha Robo Mwaka cha NGOs Kigoma

Leo KIEF tumeshiriki kikao cha robo mwaka cha NGOs kilichofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma, kata ya Mahembe.

Kikao hiki kimejikita kutathmini mchango wa NGOs katika maendeleo ya jamii kwa kipindi cha Januari hadi Machi 2026.

Tumejifunza, tumeshirikishana uzoefu, na kuweka mikakati ya kuongeza matokeo ya kazi zetu kwa jamii tunazozihudumia.

Tunashukuru Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma na wadau wote kwa ushirikiano. Tunaendelea kushirikiana kwa maendeleo ya Kigoma.

Education is not a privilege. It is a right.  I see it every day. When a child drops out because there’s no money for fe...
06/05/2026

Education is not a privilege. It is a right.
I see it every day. When a child drops out because there’s no money for fees, or the school is too far, or someone says “education is not for girls”, we all lose something. We lose a future doctor, a teacher, an engineer, a leader from our own community.
That is why I speak up. For classrooms with enough books. For teachers who get the support they deserve. For decisions that keep our children in school, not on the streets.
When we fight for education, we are fighting for the future we will all share.


27/04/2026

NI KWA 📚

Mwalimu Julius K. Nyerere aliwahi kusema, "Elimu si njia ya kupata pesa, bali ni njia ya kumkomboa mtu kiakili, kiutu, na kijamii." Maneno haya yanatukumbusha kuwa darasa si jengo tu; ni kiwanda cha kutengeneza raia wanaojitambua. Leo, bado kuna watoto wanaobaki nyumbani kwa sababu ya ulemavu, umaskini, au imani potofu kwamba “hawawezi”. Tukikubali hali hiyo, tunazima taa za kesho. Kila mtoto anayeandikishwa shuleni ni mwenge unaowashwa wa maarifa, wa ujasiri, na wa maendeleo ya familia na taifa zima.

Hivyo k**a jamii tukiwa na nia ya dhati, tunaweza kubomoa vikwazo vyote. Tuwahimize wazazi wawasajili watoto wote bila ubaguzi, tuhakikishe shule zina walimu wa elimu maalum na miundombinu rafiki, na tuache kauli zinazodhoofisha ndoto za watoto. Uandikishaji si takwimu tu; ni ahadi ya maisha bora. Mtoto mmoja anayesoma leo ni daktari, mwalimu, au kiongozi anayepunguza umaskini wa kizazi kijacho. Tusimwachie yeyote nyuma tuwaandikishe, tuwalee, tuwaamini.



Ngolelwa Enos Masanja Daniel
Green Community Initiatives - GCI Mbaruku Makuka Kigoma Elimu Foundation NGO Forum for Public Health Friends KigomaUjiji Mc



  JUMUISHI NI  , SI  ✨Kila mtoto ana ndoto. Kila mtoto ana uwezo. Haijalishi k**a ana ulemavu wa kusikia, ulemavu wa mac...
27/04/2026

JUMUISHI NI , SI ✨

Kila mtoto ana ndoto. Kila mtoto ana uwezo. Haijalishi k**a ana ulemavu wa kusikia, ulemavu wa macho, changamoto za ujifunzaji, au anatoka katika mazingira magumu darasa linapaswa kuwa mahali pa kila mmoja. Elimu jumuishi si kuhusu "kuwasamehe" watoto wenye mahitaji maalum waingie darasani. Ni kuhusu kubadilisha mifumo, miundombinu, na mitazamo yetu ili kila mwanafunzi apate kushiriki, kujifunza, na kung’ara kwa njia yake. Tunapowajenga walimu, kutoa vifaa wezeshi, na kukuza utamaduni wa kukubali tofauti, tunajenga Tanzania yenye usawa.

Tuanze nyumbani, tuendelee shuleni. Zungumza na mwalimu wa mwanao kuhusu ujumuishaji. Muunge mkono mwenzako mzazi mwenye mtoto mwenye ulemavu. Shiriki posti hii ili ujumbe ufike mbali. Tukikataa kuwatenga, tunawapa nafasi ya kutuonyesha dunia wanayoweza kuijenga. Kwa sababu darasa moja lenye watoto tofauti ndilo maabara halisi ya jamii yetu ya kesho.




Address

Address: P. O Box 2405, Ramboni Street, Matofalini Road, Opposite Kasingirima Ward Office, Ujiji
Kigoma
47108

Opening Hours

Monday 08:00 - 17:00
Tuesday 08:00 - 17:00
Wednesday 08:00 - 17:00
Thursday 08:00 - 17:00
Friday 08:00 - 13:30

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Kigoma Elimu Foundation posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to Kigoma Elimu Foundation:

Shortcuts

Share