GT Mission Ministry

GT Mission Ministry We Preach and Proclaim the Gospel of Jesus Christ to the World, We undertake this as a Purpose of Salvation

04/08/2026

Kwa maana ikiwa Mungu hakuwaachilia malaika waliokosa, bali aliwatupa shimoni, akawatia katika vifungo vya giza, walindwe hata ije hukumu; wala hakuuachilia ulimwengu wa kale, bali alimhifadhi Nuhu, Mjumbe wa haki na watu wengine saba, hapo alipoleta Gharika juu ya ulimwengu wa wasiomcha Mungu.

Mistari hii; Petro alifunuliwa jambo kubwa sana Jinsi Mungu anavyoutazama uasi na ukengeufu wa mtu, hana hasara kukuondoa na ufe katika dhambi yako haijalishi nafasi yako.

Wale malaika walioasi mbinguni, aliwatupa shimoni akawatia katika vifungo vya giza hadi siku ya kutupwa Jehanamu, unaoneje? Angewahurumia wabaki labda wangebadilika huko mbinguni, labda watubu! Akawatupilia mbali!
Unaoneje wale wa kipindi cha Nuhu, walivyoanza ukengeufu, uzinzi ulitamalaki, ikazariwa mijitu isiyomithilika ya hovyo, michafu hadi Mungu alihuzunika kwanini aliwaumba wanadamu, akapunguza hata miaka ya kuishi hadi miaka 120, lakini wapi hayakukoma ! Multiplication ya uzao muovu ilizidi sana, akaamua kuifuta dunia kwa gharika! Mijitu miovu, michafu, mizinzi, ilifutiliwa haikuoneka tena! Ni watu 8 tu wenye haki waliokolewa.

Unaoneje? kule Sodoma na Gomora, akiipindua na kuifanya majivu, akaifanya iwe ishara kwa watu watakaokuwa hawamchi Mungu baada ya haya: akamwokoa Lutu yule mwwnye haki aliyehuzunishiwa na wale walawiti, wafilaji, wahalifu. Aliwauwa wote hakusaza mtu kule.

Unaoneje wewe, una thamani kuzidi wale katika kuumbwa kwako, Mungu hana hasara, anaweza kukuondoa na uchafu wako usipotubu na Kuiamini Injili na Kuokoka.

Unatuona k**a wajinga fulani hivi tunapokutahadharisha na ukengeufu wako, acha uzinzi huo, acha ulawiti, acha ushoga huo, usagaji, ufisadi,na uchafu wako uthiomithilika, kumbuka miaka yako ya kuishi hapa duniani is so limited, una miaka mingi ya kuishi baada ya kufa hapa duniani utateseka milele baada ya hukumu.

Ningekupa na mfano mwingine wa watu karibu 600,000 au zaidi waliofia jangwani, walipomuasi Mungu kwa sheria ya Musa, unaoneje? Aliwaokoa kwa Pharao, akawaua wote Jangwani kwa kukengeuka kwao, akawaacha wana wao tu kuingia Kaanani na wale wawili tu Joshua na Karebu.

Nakutahadhalisha; Okoka sasa, la! Mungu hana hasara.

2Pet.2:4-7.

JM Mwakalebela.

01/08/2026
01/08/2026

Hii ndiyo Kweli: Haitabadilika!
1Tim.6:6-11
"Walakini utauwa pamoja na kuridhika ni faida kubwa"

"Kwa maana hatukuja na kitu duniani, tena hatuwezi kutoka na kitu" ila tukiwa na chakula na nguo tutaridhika na vitu hivyo"

" Lakini hao watakao kuwa na Mali huanguka katika majaribu na tanzi, na tamaa nyingi zisizo na maana, zenye kudhuru, ziwatosazo wanadamu katika upotevu na uharibifu"

"Maana shina moja la mabaya ya kila namna ni kupenda fedha; ambayo wengine hali wakiitamani hiyo wamefarakana na imani, na kujichoma kwa maumivu mengi".

" Bali wewe, mtu wa Mungu, uyakimbie mambo hayo; ukafuate haki, utauwa, imani, upendo, saburi, upole".

Kwanza:hatukuja na kitu duniani! Na hatutaondoka na kitu duniani! Mali tulizonazo hatutaondoka nazo! Zitabaki hapa duniani ama ziharibike au ziliwe na watakaoziwahi!

Pili: Mali na vitu vikiwa mikononi mwetu ni chanzo kikubwa cha kujaribiwa ama kwa kiburi, ama kwa dharau ama Kujiona wewe ni wewe! Ukamsahau aliyekupa!

Tatu;fedha ina nguvu, fedha inapenda ijulikane, fedha inapenda itumike huwa haipendi ikae tu! Fedha ni ukuta huwa inajilinda isiingiliwe, inanua chochote ikitaka! Fedha inapenda ukubwa! Fedha inapenda ukuu! Isipoidhibitiwa na mdhibiti fedha itakupeleka Jehanamu!

Nne; Wengi wamepotea! Walianza vizuri na Mungu! Walipoanza kuongezeka Mali na fedha, wakapofuka! Wakajichoma huko na huko! Ni wakali hawashauriki Kiroho wala hawataki kukemewa! Mali na fedha zimekuwa miungu yao! wanatengeneza injili za kuwalinda wasikemewe!

Tano;Ndugu! Hivi vyote Utaviacha hapa duniani! Chunga roho yako! Uilinde imani hii uliyoipokea! Hata ukiwa navyo vimpe Mungu utukufu na ukuu! siyo vimshushe chini! Usijaribiwe navyo!

Mwisho;Hakikisha Jina lako halifutwi kwenye Kitabu cha uzima kwasababu ya Mali na fedha! Ufu.21:27..

Mungu akukumbuke.

Hii ndiyo Kweli...

JM Mwakalebela.

Bwana Yesu Asifiwe,Mungu ametupa Nafasi tena, The Village Gospel Campaign inakwenda tena Tabora, Wilaya ya Uyui, Tutakuw...
28/07/2026

Bwana Yesu Asifiwe,
Mungu ametupa Nafasi tena, The Village Gospel Campaign inakwenda tena Tabora, Wilaya ya Uyui, Tutakuwa na Mkutano wa Injili kuanzia tarehe 9-13 Septemba 2026 utakaofanyika kwenye Kijiji cha Mlangale. Tutashirikiana na Makanisa wenyeji toka Vijiji jirani vya vya Sawewe, Ndobha, Makomba, Sala, Ugowola, Ufuluma, Makazi, Kakuni, Jionee na Kichangani.
Watu wa Maeneo hayo mnakaribishwa.

15/07/2026

Naaam.

HOW GOD CAME INTO THE BONNKE-FAMILY (Testimony)The Bonnke-Clan from East-Germany did not know Jesus. This was my family....
09/03/2026

HOW GOD CAME INTO THE BONNKE-FAMILY (Testimony)
The Bonnke-Clan from East-Germany did not know Jesus. This was my family. My grandfather August Bonnke was very sick indeed. A mysterious disease had knocked him down, which doctors could not diagnose. He suffered excruciating pains and screamed day and night for years. But then a miracle happened. An American missionary of the “Assembly of God” lost in 1922 his way in the enormous forests, where my people lived. His name was Louis Graf. These missionaries were full of the Holy Spirit. Wherever they went they prayed for the sick and saw mighty miracles. When Louis Graf got lost in the forest and came to our village, the first question was “Is there anybody sick here?” O yes! It was my very own grandfather.
Louis Graf entered August Bonnke’s household like a blazing lantern in a dismal cavern. Cobwebs of religious doubt and stagnation were swept aside as he moved toward the bed where August lay writhing in agony. He proclaimed liberty to the downtrodden, healing to the sick, and salvation to the poor needy sinner. He announced that the Holy Spirit had been sent for a demonstration of the power of God that could make all things new. He took the sick man by the hand and commanded that he rise and be made whole in the name of Jesus. August felt a jolt of heaven’s power surge through his body. He leapt from his sickbed and stood trembling like a criminal around whom the walls of a prison had just fallen. He looked at his arms and legs as if iron chains had just been struck from them. He felt his once swollen and inflamed joints, and they were renewed to a supple and youthful state. His wife, Marie, who had been at his bedside for years, began to weep. He began to walk, then to run, then to leap, then to shout. He grabbed his wife and embraced her with tears running freely down his face. A moment ago, he had been unable to endure the slightest touch on his skin. Now, he was a man set free of pain. He was free indeed.
I, Reinhard Bonnke, was born 18 years later. My father Hermann Bonnke had become a pastor. The fire of the Holy Spirit had transferred to him and later to me. God called me to be an Evangelist in Africa. I saw almost 80 million souls receive Jesus as their Savior. May the same holy flame jump into your heart and get you going for God; and may many a “lawnmower” be exchanged for a “combine harvester” in the ripe harvest fields of souls. Blessed?

Hii ndiyo Kweli: Ufu:14:13, 'Ukifa katika dhambi unakwenda moja kwa moja kwenye mateso kuzimu' Ukifa katika Bwana unakwe...
24/02/2026

Hii ndiyo Kweli: Ufu:14:13,
'Ukifa katika dhambi unakwenda moja kwa moja kwenye mateso kuzimu' Ukifa katika Bwana unakwenda moja kwa moja kupumzika peponi. Huwezi kumpangia mtu aende ambako hakuchagua!

Hakuna sehemu ya pamoja wote wafao. Kila mmoja ataongoza kule alikochagua aende na atamkuta aliyemchagua amkute! K**a Kristo ni Bwana uwe na uhakika atakupokea ukifa! Ikiwa shetani ni bwana wako uwe na uhakika atakupokea na kipondo kitaendelea huko aliko !.

Tunaweza kubembelezana sasa tungali hai usitende dhambi, lakini hatuwezi kubembeleza ukifa usiende kuzimu ! Kugeuka kutokwenda kuzimu kunafanyika ungali hai!

Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; Kwa kuwa matendo yao yafuatana nao.

Nimekumbusha tu na Hii ndiyo Kweli.

JM Mwakalebela

13/02/2026
03/01/2026

Not a single word from Abel is recorded in Scripture. Cain murders him, and Cain has something to say. But the victim of violence? the recipient of hate? the righteous one? Not a syllable.

Cain has words, Abel none.

But Abel does speak in a different language. He utters crimson eloquence, red rhetoric so profound his speech pierces heaven's veil to lodge in the ears of God.

How so? The Lord says, "The voice of your brother's blood is crying to me from the ground" (Gen. 4:10).

You see what's happening?

1. Blood has a voice.
2. Blood cries out to God.
3. Blood is heard by heaven.

Far, far later, the author of Hebrews wrote about another crimson eloquence, about more red rhetoric. He says that the blood of Jesus "speaks better than the blood of Abel" (12:24).

Whatever Abel's blood said to God, Christ's blood said it better.

The voice of Jesus's blood, crying out from the ground beneath the cross, piercing the heavens, lodging in the ears of God, speaks one and only one message: "Father, forgive them."

That eloquent blood pronounces the absolution of the world, you included.

Believe it. It is for you.

Address

Mail Moja
Kibaha

Opening Hours

Monday 05:00 - 22:00
Tuesday 05:00 - 22:00
Wednesday 05:00 - 22:00
Thursday 05:00 - 22:00
Friday 05:00 - 22:00
Saturday 05:00 - 22:00
Sunday 05:00 - 12:00

Telephone

255752154790

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when GT Mission Ministry posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to GT Mission Ministry:

Shortcuts

Share