16/09/2024
Mapema leo jumatatu ya tarehe 16 Septemba, 2024 timu ya Pepsi Boyz, Isele FC na wadau mbalimbali wefanikiwa kutembelea kituo cha kulelea watoto yatima, walemavu na wenye mahitaji maalum Mtakatifu Felix no2 na kufanikiwa kukabidhi mahitaji k**a vile Sabuni za unga mifuko 6, miche ya sabuni box 2, mafuta ya kupakaa box 1, unga wa sembe kilo 50, ped box 2, dawa za mswaki box 6, juice carton 6, p**i pc 9, biscuit box 2 na pesa taslimu shilingi elfu arobaini na tano (Tsh 45,000/=) na kukamilisha kiasi cha shilingi laki sita na elfu ishirini na mbili (Tsh 622,000/=) kilichopatikana katika kampeni ya ILULA DERBY
Aidha uongozi wa kituo umeshukuru sana umoja huu wa vijana kupitia michezo ambayo imewezesha ufanikishwaji wa jambo hili, na kuomba kuwa tuwe mabalozi wema wa kituo kwani ni watu wanaohitaji upendo mkubwa sana kutoka kwa jamii
Kipekee tutumie fursa hii kuwashukuru wadau wote walioshirikiana nasi katika zoezi hili kuanzia mwanzo hadi mwisho wa ILULA DERBY
Ikumbukwe zoezi hili limekamilika kwa ushirikiano mkubwa wa PEPSI BOYZ NA JAMII, ISELE FC, ILULA ORPHAN PROGRAM (IOP), THEO AGROCHEMICALS SUPPLY, MKINGANUSU FARM, AMANIE SUPER SEMBE, MTWASIMILE INVESTMENT,UDZUNGWA WATER, MITAA IMETULEA BRAND & SELE AUTO SPARE
๐ธ .purity