HBCo - tanzania

HBCo - tanzania Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from HBCo - tanzania, Charitable organisation, Ilemera.

Kura ndio wakati wake, zinawasubiri jamani waheshimiwa; njoooni tu!
17/06/2020

Kura ndio wakati wake, zinawasubiri jamani waheshimiwa; njoooni tu!

15/04/2020

Doforlife

Jiponye kupitia Mambo 10 na mepesi kabisa!!

01. Kumbuka chakula Cha asili kinaongeza Kinga ya Mwili Dhidi ya magonjwa mbalimbali

02. Kuepuka nyama nyekundu hasa unapokuwa mtu mzima (zaidi ya miaka 29) kwa kuwa nyama nyekundu inaongeza mafuta (cholesterols) Mwilini, Sambamba na chakula chenye kiwango kikubwa Cha sukari, ama kilichoondolewa virutubisho vyake vya asili Kisha kuongezewa utamu, K**a vile, soda, wali mweupe, chocolate, burns, keki n.k

03. Kula matunda pekee, kwa utaratibu mfano usile matunda ya ndizi na maziwa kwa pamoja, nzuri zaidi Ni bore utenge mlo ulio na matunda pekee bila chakula mfano unaweza ukala matunda yenye rangi nyeupe, jano, na nyekundu kwa pamoja bila chakula.

04. Zingatia kula mtama, uwele, na kunwya rozera ( maua ya Dodoma).

05. Epuka kuipendelea chakula kilichounguzwa kwa mafuta hasa ya yatokanayo na wanyama ili kupunguza uwezekano wa kuugua kansa

06. Epuka matumizi mabaya ya Dawa za hospital ama kutumia madawa ya kulevya na vichocheo mbalimbali kwa ajili ya kupunguza maumivu ama Msongo wa Mawazo. K**a una Maumivu/ unajihisi kuumwa muoane mtaalamu wa afya aliye na vipimo ili akusaidie, ama fika kituo Cha afya, na hospitalini.

K**a una Msongo wa Mawazo juu ya Mambo fulani ambayo hayajaenda sawa, tujilidhishe kupitia mawasiliano yetu ama fika kwa wataalamu wa ushauri na Saha walio karibu na wewe.

07. Fanya mazoezi ili kurejesha uhai wa afya yako ya Mwili na Akiri, pia unaboresja uwezo wa maamuzi yaliyo sahihi, na hormones zako kufanya Kazi vizuri.

08. Ulevi, uvutaji sigara na tabia zingine zinazoambatana na hayo huzoretesha afya, heshima na uwezo wa kufanya Kazi.

09. Kunywa maji kwa kiasi Cha uzito wako/masaa 24 + nusu Lita kwa siku itakufanya Mwili wako ujisikie shwari kabisa, au pengine inaweza inategemea na Hali ya hewa, na kwa wale walio na Kazi ngumu Sana wanaweza kunywa maji kila Mara na kadri iwezekanavyo

10. Hakuna Mazoea kwenye afya yako, Mwili upe kila kinachohitaji na Sio tamaa ya ajili yako.

Tamaa inauwa haijalishi Ni haraka ama polepole; "Linda afya yako jivunie kuwa halisi"

06/04/2020

Mazoezi Ni msingi wa afya Bora, dhidi ya matatizo mbalimbali ya kimwili, homoni, na uwezo wa kufikiria, utashi wa kufanya maamuzi sahihi n.k.
Mazoezi na nidhamu katika kula kutaifanya Afya yako kuwa maradufu.

21/03/2020

Corona Sio ugonjwa wa watu weupe tu, Bali unaathili mamalia wote, hivyo ewe mtanzania usipotoke na uvumi wa kwamba watu weusi hawapatwi na virusi ama kwamba kwa wale walioathirika na kwa wengine wakafa, hawamjui Mungu la hasha, wanamjua Sana; lakini kwa kuwa ama kwa kupuuza ama kwa kukoswa ufahamu namna ya kujikinga na ugonjwa huo; Ndio kwao umekuwa simanzi;:::

Je, wewe mtanzania utapuuzia tahadhali, na kujitia kichwa ngumu, kwa kujichanganya na hatimaye upate maambukizi?

01. Fikiria ugumu wa huduma kuipata kwa kuwa hata madaktari nao lazima wapende maisha yao kwa kujiwekea tahadhali na wewe uliyeambukizwa.

02. Fikiria uhaba wa Vifaa vya kitaalamu na dawa K**a wangonjwa watakuwa Ni wengi.

03. Fikiria watu kukosa uwepo wako katika ubora wa majukumu ulionayo kwa Sasa.

04. Fikiria namna utakavyowahangaisha ndugu na jamaa, kwa kukosa kutembelewa ukiwa mgonjwa

Mimi naanza Mara moja kujenga tahadhali kwanza nikimuomba MUNGU azibariki tahadhali hizi ili nisije nikapatwa na Virusi Vya Ugonjwa wa korona!!!

Wewe je?

MSONGO WA MAWAZO,sio wengi tunakubwa na tatizo la msongo wa mawazo, lakini ni dhahili kuwa tatizo hili limekuwa changamo...
29/02/2020

MSONGO WA MAWAZO,

sio wengi tunakubwa na tatizo la msongo wa mawazo, lakini ni dhahili kuwa tatizo hili limekuwa changamoto kwa baadhi ya wazee, vijana na kwa kiasi fulani kwa watoto walio na miaka kuanzia 9 hadi 17, kutokana na sababu mbalimbali za kimaisha, mahusiano, wajibu, mifumo ya ukuaji, chakula n.k.

Tatizo hili kwa kiasi kikubwa linawakumba wengi hasa kwa kukosa elimu/uelewa ambao ni mwanga juu ya kutambua uhalisia wa maisha na changamoto zake, mfano hakika k**a mtu ambaye anatapatapa na kukosa kujiamini baada ya mtu kuchelewa kuzaa au hazai kabisa, huyo amekosa kuelewa kuwa, MUNGU mwenyewe katuumba hivo, kwa kutofautiana katika maumnbile ya kibayolojia, kwamba wengine wawe na uzazi na wengine wasiwe nao, na k**a huyu mwenye kutokuzaa akija kubahatika kuzaa, hiyo ni mipango ya MUNGU pia; hivyo hakuna mchawi hapo:

k**a ukiwa na nguvu ya kumshawishi MUNGU akubariki tofauti na mpango wake kwako wa awali; basi udumu kumuomba na kuweka nadhili ya kweli huku ukidumu kuwa mwenye furaha, mchapakazi na kutegemea ahadi zake.

Usitengane wala kufarakana na Mwenza wako kwa sababu tu mmojawapo hazai, labda tu k**a akiwa hataki na anatumia jitihadi kubwa kuhakikisha hkuwa hazai, hapo mwaweza kuamua uamuzi tena uwe uamuzi wa Amani, ili msiruhusu nafasi ya mmojawapo au wote kujuta kwa sababu hiyo.

22/01/2020
22/01/2020

Mwaka 2020, tumejipanga kuwafikiani kwa wingi katika kuhakikisha kuwa jamii yetu ametambua vyema na namna ya kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza na matatizo ambatano k**a vile uzito kubwa au mdogo kuliko kawaida, vitambi, na ........,; hatari mbalimbali katika mazinira yetu ya kila siku kazini na nyumbani
HBCo is enlightening your way, but also strengthening the nation!
this is a campaign of awakening the community of Tanzania from bad lifestyle, to get assurance of health living

22/01/2020

The only way to make people living with stroke is show and support them to fullfil their daily plan through doing physical exercise, in the morning and evening attend with him/her in the ground and make exercise so funny
Doing this will help them to recover and living good life for their time being.

Tusiwanyanyapae na kuwaona mizigo katika familia zetu; na ujue pia matatizo haya hayaji K**a ajali, ninamaanisha mtu kupata kisukari, kupalalaizi, na presha Sio rahisi Wala Sio Jambo la siku moja;

Kulianza na dalili na kwa muda mrefu dalili hizo zikawa zinakusumbua lakini haukuchukua/hamkuchukua tahadhali na kujiepusha na mazingira hatarishi.

Kwa hiyo jiwekee malengo binafsi ya namna utakavyokuwa unafanya ili kuondokana au kuzuia tatizo Hilo lisizidi kukua

Mfano; weka malengo kwa kuzingatia muda (miezi 3, nusu mwaka, mwaka, miaka 2 n.k.), aina ya mazoezi ( ya nguvu, kuvuta, kulainisha viungo, na sawia)

Usiboke na mazoezi kwa kuwa labda unayaridirudia yaleyale, hapana! Elewa kwamba zoezi ambalo umeelekezwa na mtaalam wako was mazoezi linafaida kwa ajili ya Hali yako, wewe unachotakiwa kukifahamu namna gani utayafanya mazoezi hayo kwa usalama:

Ushauri huu unaletwa kwako na HBCo.
💪💪💪💪💪💪💪

16/11/2019
16/11/2019

ISHI MAISHA YALIYO BORA!

16/11/2019

badili mtindo wa maisha yako, kwa kujali afya na usalama wako, upate kutimiza ndoto yako!!

23/09/2019
23/09/2019

Faida tano muhimu juu ya mtindo bora katika maisha yako.
1. hautagua magonjwa yasiyoambukizwa kamwe, na k**a namna moja au nyingine ulipata kurithi toka kwa wazazi wako, ukiwa na mtindo bora wa maisha, hautapata usumbufu wowote utokanayo na mqonjwa hayo.

2. kupunguza wagonjwa mahospitalini, majumbani.

3. kupunguza utegemezi, lawama baina ya jamii.

4. kupunguza matumizi makubwa ya bajeti ya matibabu

5. kurejeshwa na kufanya maradufu kinga ya mwili hadi dhidi ya magonjwa yanayoambukizwa

23/09/2019

Karibuni katika semina zetu, kwa ajili ya Afya zetu, kwa mawasiliano zaidi piga simu namba 0757787880, email; [email protected].
au k**a unapenda kukoment, Fanya hivo katika ukurasa juu wa Facebook; kwa sasa tuko SENGEREMA mjini na tuko na semina katika WATATUBU GYM kila siku ya alhamisi SAA 11:00 jioni

13/09/2019

kwa miaka kadhaa na kwa watu wengi wamekuwa wakifanya mazoezi k**a hobby na wengine kwa ajili ya lengo la kupendeza au kuvutia, na kwa hali hiyo wengi wamekumbana na matatizo mbalimbali baadhi yake ni hizi
1. kufanya mazoezi bila kuzingatia usalama wa afya kisa awe mwenye mvuto.
2. kwa kuwa walitamani kuwa wenye guvu na stamina, umahili huo wakautumia kufanikisha matukio mabaya. n.k.


HBCo ni shirika linalokuelimisha na kutambua kuwa mazoezi ni chanzo cha kuimarisha afya yako, pamoja na kuzingatia lishe bora hasa chakula cha asili.
mazoezi hayana madhara lakini mtu atafanya bila kuzingatia hatua anaweza kupata matokeo ambayo hakutegemea.

mazoezi yanaumhimu wa kuimarisha afya ya akili na mwili
kwa kuufanya mwili wako uwe wa msawazo, furaha na mwenye kuvutia.
zaidi na zaidi yanatokomeza magonjwa yasiyoambukizwa/ magonjwa na matatizo yatokanayo na mtindo mbaya wa maisha.
k**a vila kisukari, presha, kansa, kupalalaizi, moyo kushindwa kufanya kazi vizuri na kwa ufanisi, kitambi n.k.

mtindo mbaya wa maisha ni pamoja na;-
1. kutozingatia mlo kamili,( kupendelea vyakula vya sukari nyingi hasa ya viwandani k**a vile tomato, chipsi, keki soda, wali mweupe n.k)

2. kutofanya mazoezi na kutojishughulisha
jamii ya tanzania tunaisa kubadili mtindo mbaya wa maisha ili kupunguza gharama za matibau, utegemezi, vifo, na wagonjwa mahospitali.

Address

Ilemera

Telephone

+255757787880

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when HBCo - tanzania posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to HBCo - tanzania:

Share