Marafiki Wa Elimu

Marafiki Wa Elimu Harakati za Marafiki wa Elimu ni harakati za mashirika, taasisi na watu wenye nia ya kuboresha na ku

Madhumuni ya Harakati za Marafiki wa Elimu ni kutoa fursa kwa watu wanaojali elimu na demokrasia, kubadilishana mawazo na maoni katika masuala ya elimu na kuchukua hatua kwa ajili ya kuleta mabadiliko. Harakati zitachangia kubadili mifumo ya shule ziweze kutoa elimu bora kwa kuzingatia misingi bora ya utawala na haki za binadamu.

27/03/2026

🚨 *MABADILIKO MAPYA YA MITAALA YA ELIMU SHULE ZA MSINGI, SEKONDARI NA VYUO* 2025

MABORESHO YA MITAALA AMBAYO YANAENDA KUBADILISHA MFUMO WETU WA ELIMU:

1. Mtihani wa darasa la Saba utafutwa ifikapo 2027.

2. Mwanafunzi akianza darasa la kwanza lazima amalize Kidato cha nne. Hii itaitwa Elimu ya Msingi.

3. Kutakuwa na Mtihani wa Upimaji wa Kitaifa wa darasa la sita (STANDARD SIX NATIONAL ASSESSMENT) ifikapo 2026.

4. Mwanafunzi atatakiwa asome fani fulani kabla hajamaliza Kidato cha nne ili aweze kujiajiri au kuajiriwa baada ya kumaliza. Hii itaanzia Secondary ambapo kutakuwa na mikondo miwili; Jumla na Amali.

5. Lugha ya kufundishia na kujifunzia itakuwa kiswahili, Kiingereza kitakuwa k**a somo kwa Shule za Kiswahili Medium na lugha ya kufundishia English, kiswahili kitakuwa K**a somo kwa Shule za English Medium.

6. Elimu ya Msingi itakuwa miaka 6. Mwanafunzi ataanza darasa la kwanza akiwa na miaka 6 tofauti na ya sasa miaka 7.

8. Elimu ya Awali mwanafunzi ataanza akiwa na miaka 5. Mwanzoni elimu ya awali haikuwa rasmi na shule za Serikali haikuwepo. Sasa itakuwepo kwa utaratibu huo.

9. Masomo ya Elimu ya Msingi yatakuwa ni KKK(Kusoma, Kuhesabu, Kuandika), Jiografia, kiswahili, Sanaa na Michezo, Hisabati, Sayansi, historia ya TANZANIA na Maadili, Dini na kiingereza na Stadi za Kazi itachomekwa.

10. Kiingereza kitafundishwa kuanzia darasa la kwanza kwa shule za Kiswahili na kiswahili kitafundishwa kuanzia darasa la kwanza kwanza kwa shule za kiingereza.

11. Shule zenye uwezo zitafundisha angalau somo moja la lugha za kigeni k**a Kichina au Kifaransa.

12. Sekondari kutakuwa na mikondo 2, mkondo wa jumla na Amali (Ufundi). Mwanafunzi atachagua kutokana na uwezo, matakwa na malengo yake ya baadaye.

13. Mkondo wa amali (ufundi) utakuwa na fani zifuatazo:-
> Kilimo na Ufugaji.
> Umakenika.
> Biashara na Ujasiriamali.
> Sanaa na Ubunifu.
> Elimu ya Michezo.
> Ufugaji wa Nyuki.
> Uchimbaji wa Madini.
> Urembo.

14. Mwanafunzi wa Mkondo wa Amali atatakiwa kuchukua Masomo manne (4) ya jumla na moja la fani.

15. Masomo ya jumla ya wanafunzi wa Amali ni:-
> Hisabati.
> Elimu ya Biashara.
> Kiingereza.
> Historia ya Tanzania na Maadili.

16. Wahitimu wa Amali watapata vyeti viwili yaani:-
> Cheti cha ujumla cha Elimu ya Sekondari (NECTA) na Cheti cha Amali ( NACTIVET).

17. Kila shule itakuwa na Wakala wa VETA ili kusimamia masuala ya Ufundi.

18. Kila shule haitakuwa na Mikondo zaidi ya miwili ya Ufundi, hii ni kwa ajili ya Ufanisi na fani ziwe zinaendana na fursa za eneo husika.

19. Kutaanzishwa somo jipya la Mawasiliano ya Kitaaluma (ACADEMIC COMMUNICATION) katika A-level na Ualimu.

20. CODING itafundishwa Shule za Msingi.

21. INFORMATION and COMPUTER STUDIES (ICS) itabadilishwa na kuitwa COMPUTER SCIENCE.Somo limesukwa upya.

22. CIVICS itaunganishwa na Historia ya TANZANIA na Maadili kwa O-level.

23. O-level Masomo ya lazima yatakuwa 6 badala 7 ya Sasa.

24. Katika O-level Masomo ya Biology na Geography yatakuwa Masomo ya kuchagua pia kwa sababu Maudhui yake yamekuwa kwenye Masomo ya Jiografia na Sayansi ya Shule ya Msingi kwa mfano Afya ya Jamii, Afya ya Uzazi, Magonjwa ambukizi nk.

25. Civics, Maarifa ya Jamii, Uraia na Maadili yamefutwa, Maudhui yake yameingia katika somo la Historia ya TANZANIA na Maadili.

26. General Studies (GS) katika A-level itafutwa na Maudhui yake yatawekwa katika Somo la Historia ya TANZANIA na Maadili na Mawasiliano ya Kitaaluma.

27. Kufuta baadhi ya Masomo kumefanyika ili kuondoa tatizo la kujirudiarudia kwa Maudhui.

28. Michepuo katika Elimu ya O-level imeongezeka kutoka minne (4) hadi tisa (9).

Michepuo iliyoongezeka ni:-
> Sanaa.
> Lugha.
> Muziki.
> Michezo.
> Tehama.

29. Masomo ya O-level yatakuwa:-
> Biology.
> Physics.
> Chemistry.
> History.
> Geography.
> Historia ya TANZANIA na Maadili.
> Hisabati.
> Kiswahili.
> English.
> Elimu ya Biashara.
> Utunzaji wa _Taarifa za Fedha.
> Computer Science.
> Bible Knowledge.
> Elimu ya Dini ya kiislamu etc.

30. Astashahada ya Ualimu itafutwa kisha itaanzishwa Stashahada (DIPLOMA) ya Elimu ya Awali, Ualimu wa Msingi na Ualimu wa Elimu Maalumu.

> Watakaosoma Stashahada watakuwa waliomaliza Kidato cha Sita na itasomwa kwa miaka miwili.

31. Walimu wa Sekondari wote watakuwa na Shahada (DEGREE). kwa sababu nchi nyingi zinaenda na mwelekeo huu.

32. Vyuo vilivyokuwa vinatoa Stashahada (DIPLOMA) ya Ualimu wa Sekondari vitatumika kutoa continuous Professional Development.

27/03/2026
Siku yetu ya leo Imekuwa ya kipekee kwan ni siku ya kuzaliwa ya Mkurugenzi wetu wa Marafiki Wa Elimu Geita Allah akupe u...
23/07/2025

Siku yetu ya leo Imekuwa ya kipekee kwan ni siku ya kuzaliwa ya Mkurugenzi wetu wa Marafiki Wa Elimu Geita
Allah akupe umri mrefu wenye manufaa,
Hakika wewe ni kijana mdogo Lakin mwenye upeo mkubwa saana mwenye hekima saaana, mwenye uzalendo
Alipwe thawabu mama yako na babako waliokuzaa na kukulea vyema, 🤲
Akutunzie familia yako🤝🤲🤲

09/05/2025

Je, unajua kuwa watoto wa elimu ya awali hujifunza kwa njia tofauti na watu wazima❓

Katika hatua hii muhimu ya ukuaji, watoto hujifunza kupitia 🎲 michezo,🎶 nyimbo, 🎨 michoro, 📚 hadithi, 🗣️ mawasiliano ya kila siku. Mbinu hizi huwasaidia kukuza fikra bunifu, lugha na mawasiliano,💡 ubunifu na ujasiri wa kujifunza na 🌍 uelewa wa mazingira yanayowazunguka.

⚠️ Watoto kujifunza mambo magumu kabla hawajawa tayari kunaweza kuwakatisha tamaa 😔 na kuwafanya waone kujifunza k**a jambo gumu au la kuogopesha 😟.

Je!, Mzazi/Mlezi, unafuatilia anachojifunza mwanao katika darasa la elimu ya awali? Karibu tujadili.

.

Hongera sana Marafiki wa Elimu Katavi
09/05/2025

Hongera sana Marafiki wa Elimu Katavi

31/05/2024

▪️ Hali ya Elimu kwa watoto wanaotoka kwenye familia zenye kipato duni maneneo ya mijini Tanzania iko vipi? Ni utafiti wa kipekee kabisa kufanyika nchini, hivyo weka katika ratiba tukio hili uweze kuungana nasi kidijitali katika uzinduzi wa ripoti hii.

28/05/2024

Leo ni Siku ya Hedhi Salama Duniani.
Serikali, wazazi na jamii kwa ujumla tuwawezeshe wanafunzi wa k**e kujihifadhi wakati wa kipindi cha hedhi.

Je Rafiki wa Elimu umefanya nini ili kuhakikisha watoto wa k**e hawakosi masomo au kwenda shule pindi wanapokuwa hedhi?

Wajumbe wa mtandao wa marafiki wa Elimu Kilwa baada ya uchaguzi wa Timu ya watu 12, Ufuatiliaji wa Mpango wa kurejesha w...
11/05/2024

Wajumbe wa mtandao wa marafiki wa Elimu Kilwa baada ya uchaguzi wa Timu ya watu 12, Ufuatiliaji wa Mpango wa kurejesha watoto shule wale wote waliokatisha Masomo kutokana na changamoto mbalimbali.(Uratibiwa na shirika la HakiElimu Tanzania)

KUTOA NI MOYO NA SI     UTAJIRI Rafiki wa Elimu Kilwa Ndugu Manjesa akiwa anakabidhi msaada wa taa kwa Mh SAIDI KHALIFA ...
11/05/2024

KUTOA NI MOYO NA SI UTAJIRI
Rafiki wa Elimu Kilwa Ndugu Manjesa akiwa anakabidhi msaada wa taa kwa Mh SAIDI KHALIFA (M/mwenyekiti wa mtandao wa marafiki Elimu Kilwa) zitazotumika katika jengo la Maktaba za jamii Kilwa, Kuongeza mwanga wakati wa kujisomea.

12/04/2024
PAMOJA NA KUONGEZA TAALUMA INASAIDIA KUPUNGUZA UTORO KWA WANAFUNZI.Ni utaratibu kwa wanafunzi kuudhuria masomo Asubuhi n...
01/04/2024

PAMOJA NA KUONGEZA TAALUMA INASAIDIA KUPUNGUZA UTORO KWA WANAFUNZI.

Ni utaratibu kwa wanafunzi kuudhuria masomo Asubuhi na jioni, Hapo nyuma Maeneo ya Kata ya Masoko kumekua na changamoto baada ya mapumziko ya mchana baadhi ya wanafunzi kuto rudia tena shule na badala yake kuelekea katika fukwe za bahari kucheza au kuogelea.

Lakini uwepo wa maktaba ya Jamii Kilwa licha ya kuongeza Taaluma imesaidia kuongeza maudhurio, Wanafunzi wengi wamejijengea utamaduni wa wakati wa mapumziko ya mchana kwa idadi kubwa wanaudhuria Maktaba badala ya Kwenda kwenye fukwe za bahari.

Hata hivyo Maktaba inamahitaji Makubwa ya Vitabu kwani vilivyopo ni chakavu.

Address

Geita

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Marafiki Wa Elimu posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share