LEAD Foundation

LEAD Foundation LEAD Foundation is an NGO registered with the Government of Tanzania with offices in Dodoma and Mpwapwa.

LEAD Foundation is an NGO based in Mpwapwa, registered with the Government of Tanzania.

Miezi mitatu. Msimu mmoja wa mvua. Mabadiliko yanaonekana. 🌧️🌱Kwa kuchimba makinga maji ya nusu mwezi, tunavuna maji ya ...
06/03/2026

Miezi mitatu. Msimu mmoja wa mvua. Mabadiliko yanaonekana. 🌧️🌱

Kwa kuchimba makinga maji ya nusu mwezi, tunavuna maji ya mvua na kuyawezesha kupenya ardhini badala ya kutiririka juu ya ardhi. Ndani ya miezi mitatu tu, eneo lililokuwa kavu linaanza kurejea na kuota nyasi.

Maeneo ya malisho yenye afya bora huleta malisho zaidi kwa mifugo, maisha bora kwa wafugaji, na kuimarika kwa bioanuwai.

Kwa kuwa Umoja wa Mataifa umetangaza mwaka 2026 kuwa Mwaka wa Kimataifa wa Maeneo ya Malisho na Wafugaji (International Year of Rangelands and Pastoralists), juhudi za kurejesha ardhi hizi ni muhimu zaidi kuliko wakati mwingine wowote. πŸŒπŸ„πŸŒΎ

Miezi michache iliyopita, eneo hili lilikuwa kavu na limechoka. Hakukuwa na majani. Hakukuwa na uhai. Ilikuwa ni ardhi i...
20/02/2026

Miezi michache iliyopita, eneo hili lilikuwa kavu na limechoka. Hakukuwa na majani. Hakukuwa na uhai. Ilikuwa ni ardhi iliyoharibika.

Kisha tukaanza kazi.

Kwa kuchimba makinga maji aina ya nusu mwezi, tulizuia maji yasitiririke, tukayafanya yabaki ardhini na kuupa uoto wa asili nafasi ya kupona. Leo? ukijani unaanza kurejea. Ardhi inabaki na unyevu kwa muda zaidi. Uhai unarudi taratibu 🌦️🌱

Kurejesha ardhi si tu kuhusu nyasi. Ni kuhusu kuimarisha maisha ya jamii, kuongeza bioanuwai, na kuhakikisha malisho ya kutosha kwa mifugo.

Hatua ndogo. Mabadiliko makubwa. πŸ’š

Kutoka angani, faida ya Kisiki Hai haipingiki.Kwa kutumia mbinu ya Kisiki Hai (FMNR), tunarejesha miti katika maeneo kam...
12/12/2025

Kutoka angani, faida ya Kisiki Hai haipingiki.

Kwa kutumia mbinu ya Kisiki Hai (FMNR), tunarejesha miti katika maeneo kame, kuboresha ardhi, kuboresha maisha ya watu, na kurejesha bioanuai.

Picha hii ya Google Earth kutoka kijiji cha Chipogoro mkoani Dodoma ni mfano tu wa maelfu ya hekta ambazo tumerejesha uhai wake nchini Tanzania.

Kwa kushirikiana na Justdiggit na jamii, tayari tumerejesha miti zaidi ya milioni 23 katika mikoa ya Dodoma na Singida na huu ni mwanzo tu 🌱

Miaka mitatu iliyopita yalikuwa ni machipukizi madogo yanayochipua, leo ni miti iliyosimama wima, imara, kijani na imeja...
07/11/2025

Miaka mitatu iliyopita yalikuwa ni machipukizi madogo yanayochipua, leo ni miti iliyosimama wima, imara, kijani na imejaa uhai.

Hii ndio nguvu ya njia ya Kisiki Hai. Pamoja, tumeweza kurejesha miti million 24, na huu ni mwanzo tu

🀝Mradi unatekelezwa nasi kwa kushirikiana na Justdiggit

Baada ya makinga maji aina ya nusu mwezi kuchimbwa, uoto wa asili huanza kuota ndani ya makinga maji halafu baada miaka ...
12/09/2025

Baada ya makinga maji aina ya nusu mwezi kuchimbwa, uoto wa asili huanza kuota ndani ya makinga maji halafu baada miaka michache uoto huu husambaa katika maeneo jirani ambayo yalikuwa hayajachimbwa makinga maji. Picha hizi zinaonesha jinsi uoto wa asili ulivyoanza kuota ndani ya makinga maji na kuanza kuenea katika maeneo jirani baada ya miaka michache.

πŸ“ Eneo: Kijiji cha Pembamoto , Dodoma, πŸ‡ΉπŸ‡Ώ

🀝 Ushirikiano wa .tz na

Address

Plot 125 Kilimani, Box 1823
Dodoma

Opening Hours

Monday 09:00 - 17:00
Tuesday 09:00 - 17:00
Wednesday 09:00 - 17:00
Thursday 09:00 - 17:00
Friday 09:00 - 17:00

Telephone

+255262322786

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when LEAD Foundation posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share