Dodoma YOUTH Development Organization -doyodo

Dodoma YOUTH Development Organization -doyodo Youth Led org. that's empower young people in health, education, leadership and economically .

TANZANIA YOUTH DEVELOPMENT FORUM TYDF 2026
20/01/2026

TANZANIA YOUTH DEVELOPMENT FORUM
TYDF 2026

📌 DOYODO YASHIRIKI TATHMINI YA UTEKELEZAJI WA NAIA–AHWDOYODO Tanzania imeshiriki kikamilifu katika kikao cha tathmini ya...
08/01/2026

📌 DOYODO YASHIRIKI TATHMINI YA UTEKELEZAJI WA NAIA–AHW

DOYODO Tanzania imeshiriki kikamilifu katika kikao cha tathmini ya utekelezaji wa Ajenda ya Kitaifa ya Kuwekeza katika Afya na Maendeleo ya Vijana Balehe (NAIA–AHW) kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2021/22 hadi 2024/25, kilichoandaliwa na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum.

Kikao hiki muhimu kilifanyika tarehe 22–23 Desemba 2025, kikilenga kutathmini mafanikio, changamoto na masomo muhimu katika utekelezaji wa nguzo sita za NAIA–AHW, zikiwemo:
✔️ Kuzuia maambukizi ya VVU
✔️ Kutokomeza mimba za utotoni
✔️ Kupambana na ukatili wa kijinsia na dhidi ya watoto
✔️ Kuboresha hali ya lishe
✔️ Kuhakikisha wasichana na wavulana wanabaki shuleni
✔️ Kuwezesha vijana kupata ujuzi na fursa za kiuchumi

Ushiriki wa DOYODO unaonesha dhamira yetu ya kuendelea kuwa mdau hai katika juhudi za kitaifa za kuwezesha vijana, kuchangia ushahidi wa utekelezaji, na kusukuma mbele ajenda za maendeleo jumuishi na endelevu kwa vijana wa Tanzania.

📢 Pamoja tunajenga kizazi chenye afya, ujuzi na fursa!

*25/11/2025*Mkurugenzi Mtendaji wa DOYODO na Mwenyekiti wa Jukwaa la Maendeleo ya Vijana Tanzania (TYDF), Ndg. Rajabu Ju...
07/12/2025

*25/11/2025*

Mkurugenzi Mtendaji wa DOYODO na Mwenyekiti wa Jukwaa la Maendeleo ya Vijana Tanzania (TYDF), Ndg. Rajabu Juma Suleiman, ameongoza kikao cha robo ya tatu cha mwaka cha Wadau wa Kamati Tendaji ya TYDF.

Kikao hiki kimefanyika kwenye ofisi za Plan International Tanzania, jijini Dar es Salaam, kikiwakutanisha wadau wa maendeleo ya vijana pamoja na wajumbe wa Kamati Tendaji ya TYDF kwa mwaka 2025/2026. Ajenda kuu ya kikao ilikuwa kujadili mpango na utekelezaji wa TYDF kwa mwaka 2026, pamoja na mikakati madhubuti ya kuhakikisha jukwaa linafikia na kugusa kundi kubwa zaidi la vijana nchini.

Kikao kimeendelea kutoa mwelekeo thabiti wa kuimarisha ushirikiano na mshik**ano miongoni mwa wadau, kwa lengo la kufanya TYDF kuwa jukwaa jumuishi, linalosikiliza sauti za vijana na kutekeleza mipango yenye tija. DOYODO inaendelea kuthibitisha nafasi yake katika kusukuma mbele ushiriki wa vijana kwenye maendeleo ya taifa kupitia majukwaa shirikishi na yenye matokeo chanya.

03/09/2025  Mkurugenzi Mtendaji wa DOYODO na Mwenyekiti wa Jukwaa la Maendeleo ya Vijana Tanzania (TYDF), Ndg. Rajabu Ju...
04/09/2025

03/09/2025 Mkurugenzi Mtendaji wa DOYODO na Mwenyekiti wa Jukwaa la Maendeleo ya Vijana Tanzania (TYDF), Ndg. Rajabu Juma Suleiman, ameongoza kikao cha robo ya pili ya mwaka cha Wadau na Kamati Tendaji cha TYDF kilichofanyika katika ofisi za Marie Stopes, jijini Dar es Salaam. Kikao hiki kiliangazia uwasilishaji wa mpango na bajeti ya TYDF 2026.

Kikao kilitoa mwelekeo mpya na kuimarisha mshik**ano wa pamoja kati ya wadau kwa lengo la kuhakikisha TYDF linaendelea kuwa jukwaa shirikishi, lenye manufaa makubwa kwa vijana na lenye utekelezaji wenye ufanisi. TYDF linaendelea kuthibitisha nafasi yake k**a chombo muhimu cha kuwakutanisha vijana na wadau mbalimbali katika kuendeleza ustawi na maendeleo ya vijana nchini.

DOYODO had the honor of hosting Amref Health Africa Country Director  Dr. Florence Temu, who was welcomed by our Executi...
31/08/2025

DOYODO had the honor of hosting Amref Health Africa Country Director Dr. Florence Temu, who was welcomed by our Executive Director, Mr. Rajabu Juma Suleiman.

We shared our journey and vision through the TYDF Youth Empowerment Center, the TYDF Digital Hub, and the upcoming Tanzania Youth Development Forum 2026, all platforms designed to amplify young people’s voices and unlock their potential.

Dr. Florence Temu celebrated 10 years of DOYODO’s impact and pledged to stand with us in driving forward youth development in Tanzania.

This milestone reminds us that when partners unite, young people rise, communities grow, and nations transform.

*Taasisi ya Dodoma Youth Development Organization (DOYODO)* imetambuliwa na kutunukiwa *cheti cha heshima* kwa mchango w...
25/08/2025

*Taasisi ya Dodoma Youth Development Organization (DOYODO)* imetambuliwa na kutunukiwa *cheti cha heshima* kwa mchango wake thabiti katika kuinua ustawi wa jamii kupitia programu shirikishi za vijana, elimu ya uongozi, afya, uchumi na teknolojia.

Cheti hicho kilipokelewa na *Mkurugenzi Mtendaji wa DOYODO na Mwenyekiti wa Jukwaa la Maendeleo ya Vijana Tanzania (TYDF), Ndg. Rajabu Juma Suleiman*, na kukabidhiwa na *Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima*, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, *kwa niaba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango*, wakati wa Kongamano la Mwaka la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGOs).

Heshima hii inaonesha uthibitisho wa dhamira ya DOYODO kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa taifa kupitia sauti na nguvu kazi ya vijana.

Mkurugenzi Mtendaji wa Ladies Joint Forum na Mwakilishi wa Vijana katika Baraza la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali, Bi. F...
26/07/2025

Mkurugenzi Mtendaji wa Ladies Joint Forum na Mwakilishi wa Vijana katika Baraza la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali, Bi. Francisca Damian Mboya, akifanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa DOYODO na Mwenyekiti wa TYDF, Ndg. Rajabu Juma Suleiman, kuhusu maandalizi ya Jukwaa la Kitaifa la NGOs litakalofanyika tarehe 11-13 Agosti 2025, likilenga kutathmini mchango wa mashirika katika maendeleo ya taifa kwa kipindi cha miaka mitano.

Aidha, Bi. Francisca aliipongeza DOYODO kwa kutimiza miaka 10 ya mafanikio, na kuweka sahihi yake kwenye bango la maadhimisho.


Address

Dodoma

Opening Hours

Monday 08:00 - 16:00
Tuesday 08:00 - 16:00
Wednesday 08:00 - 16:00
Thursday 08:00 - 16:00
Friday 08:00 - 16:00

Telephone

+255677066490

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Dodoma YOUTH Development Organization -doyodo posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to Dodoma YOUTH Development Organization -doyodo:

Share