04/06/2026
Shirika la INADES-Formation Tanzania leo lilipata fursa ya kumueleza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Hamad Masauni, kuhusu shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na shirika hilo alipofanya ziara katika banda la Shirika hilo wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani yanayoendelea katika Viwanja vya Jakaya Kikwete, Dodoma.
Afisa wa Mafunzo kwa Masafa wa shirika hilo, Daisy Mola, alimueleza Waziri kuhusu kazi za shirika katika utunzaji wa mazingira, kilimo endelevu na matumizi ya mbegu za asili zinazovumilia ukame na magonjwa na mradi wa kuboresha ustawi wa mnyama kazi punda, miradi ikiwa inatekelezwa mikoa ya Dodoma, Iringa na Singida kwa ufadhili wa mashirika ya Bread for the World na Brooke East Africa.
Akizungumza baada ya kutembelea banda hilo, Waziri Masauni alilipongeza shirika kwa mchango wake katika kulinda na kuhifadhi mazingira, akisema juhudi hizo zinaunga mkono Dira ya Taifa ya kuikijanisha Tanzania ifikapo mwaka 2050.
Pia alitambua mchango wa kampeni ya upandaji miti ya “Panda Mti, Tuilinde Kesho” iliyoanzishwa Januari 2026 na Shirika hilo, ambayo inalenga kupanda miti 500,000 ifikapo mwaka 2027, tayari ikiwa imepanda miti 19,758 katika wilaya za Bahi, Chemba na Kondoa