CHECHEReborn Universities Magazine

CHECHEReborn Universities Magazine Lusaglo Attorneys & Consultants Lawfirm; Enhancing Legal Profession_Tz🇹🇿 Deals with Civil&Criminal Imani ya CHECHE Reborn:

Imani kuu ni UKWELI.

“CHECHE Reborn Univeristies Magazine ni makala maalumu, amshi kifikra ambazo zitaanza kubandikwa rasmi katika maeneo ya vyuo vikuu vyote nchini mara baada ya uzinduzi wake. Gazeti hili la makala linakusudia kurudisha vuguvugu zito la wasomi wa vyuo vikuu lililokuepo miaka ya nyuma katika harakati za wanafunzi kulitetea Taifa kinyume na ilivyosasa ambapo kunawimbi kubwa la wasomi waliotawaliwa na u

binafsi, ubepari, ubeberu na ukoloni mambo leo. Makala za gazeti hili zitakuwa zinabandikwa mara Moja kwa wiki katika maeneo ya vyuo vikuu vyote nchini. Misingi ya CHECHE Reborn:

msingi mkuu wa Makala za “CHECHE

REBORN” ni kuheshimu ukweli na kusema ukweli bila kumwogopa au kumhofia kiongozi au mtu yeyote kwa maslahi ya maendeleo ya taifa. Misingi mingineyo ni: Umuhimu wa kujielimisha katika masuala na fikra za kisayansi na ukombozi, Kurudisha hadhi ya taasisi za vyuo vikuu nchini na hadhi ya msomi iliyokwishapotea mbele ya uso wa jamii,
Kutoa taarifa za kitafiti na za kishahidi ili kuendelea kuleta utajiri wa taarifa sahihi kwa wanavyuo, wanazuoni na jamii kwa ujumla wake ili zifanyiwe kazi kwa vitendo katika muhimili wa vyuo vikuu. Kurudisha mwamko wa mijadala ya wasomi yenye maslahi na Taifa katika vyuo vikuu nchini katika maeneo maalumu yaliyotengwa kwa mijadala mathalani REVOLUTION SQUARE ndani ya vyuo vikuu vyote nchini k**a ilivyokuwepo hapo awali. CHECHEReborn haifungamani na Chama chochote cha siasa haswa itajihusisha na kutafuta Ukweli wa mambo k**a kazi kuu ya Elimu inavyojitanabaisha bila kujali itikadi ya chama chochote cha siasa. WanaCHECHEReborn hawanabudi kuuishi na kuuamini ukweli kwa gharama yoyote ile. Inaamini Taasisi za Vyuo vikuu nchini ni muhimili mwingine muhimu na wenye Meno baada ya Bunge, Mahak**a na serikali k**a itatumika ipasavyo. Inaamini kwamba Taifa letu linamihimili mikuu mitatu: Serikali, Bunge na Mahak**a ila muhimili ambao ni muhimu zaidi ya mihimili hii ni taasisi za vyuo vikuu kwani ni Jicho la Taifa, ni mahala penye udongo wa rutuba wa fikra huru na za kitafiti. Ni eneo ambalo wanafunzi wa vyuo vikuu na wanazuoni wanauwezo wa kulisimamia Bunge na Serikali bila kujali itikadi zao za vyama vya siasa. CHECHE Reborn Inaamini pia kazi kubwa ya wasomi ni kutumia taaluma na ujuzi wa wao kuonyesha njia zinaoweza kuleta ukombozi na maendeleo ya watanzania. CHECHE Reborn inashirikiana na Mtandao wa Watetezi wa haki za binadamu ndani na nje ya vyuo vikuu nchini ambao wamejiridhisha kwamba Taifa letu linahitaji vuguvugu jipya la mapinduzi ya taasisi za vyuo vikuu nchini “Universities Revolution- Universities Reborn-dhana kamili”

HITIMISHO:

Hatuna budi kuikumbuka historia ya waasisi wa gazeti la CHECHE na huu ni muendelezo wa fikra zao ndani ya Vyuo vikuu nchini. Gazeti hili liliamsha bongo mgando za wasomi na wanazuoni kutambua wajibu wao kwa Taifa na hatimaye kufungiwa na Serikali katika awamu ya nne. Sisi tumechukua jukumuu la kuendeleza harakati njema zenye maslahi na taifa kwani wapo waasisi wa wazo la gazeti la CHECHE na baada ya gazeti hili kufungiwa, wahariri wa gazeti hili waliamua kuandika Kitabu chenye jina la CHECHE, chenye sura 12 na zaidi ya kurasa 200 ambacho dhana yake kuu ni kuendeleza mawazo ya gazeti la Cheche ya kuendeleza mapambano ya kweli ya ukomboi wa Tanzania na Afrika kwa ujumla wake, kimeandikwa na watu mbalimbali akiwemo Profesa Hirji, Rais Yoweri Museveni wa Uganda. Wengine ni Prof Hajivayanis, Mapolu, Liundi na Zakia Meghji aliyeandika Sura ya Sita ya kitabu hicho.

NANI ATALIA NA KUOMBOLEZA SIKU NIKIFA?  WITO WA MABADILIKO KWA VIJANA        Swali kubwa la kujiuliza ni hili: Umeletwa ...
18/04/2025

NANI ATALIA NA KUOMBOLEZA SIKU NIKIFA? WITO WA MABADILIKO KWA VIJANA

Swali kubwa la kujiuliza ni hili: Umeletwa duniani kwa bahati mbaya k**a mzururaji ili ule ushibe, uposti picha mitandaoni, ubishane kuhusu mpira wa Simba na Yanga, alafu baadae ufe k**a mzoga na kusahaulika, au umeletwa duniani kwa malengo mahsusi ili uwe hadithi na kumbukumbu nzuri kwa familia, jamii na taifa lako?
Tanzania inahitaji kizazi kipya cha watu wanaojiuliza, “Nitaacha alama gani baada ya maisha haya mafupi?” Siyo alama ya picha 1,000 kwenye mitandao, bali alama ya kujitoa, kusimama, na kusema: “Sitakubali taifa langu lijengwe juu ya mifupa ya kizazi kilichonyamaza.”
Yesu Kristo, alizaliwa katika familia maskini ya mafundi Seremala, akiwa kijana mdogo akanza harakati za kuhubiri, kufundisha na kupigania ukombozi wa kiroho, kijamii na kiakili kwa watu waliodhalilishwa na mfumo wa kiimla wa kidini na wa kifalme.
Katika maisha yake ya miaka 33 tu, alijitambulisha na Kujipambanua k**a mwalimu, Mkombozi, na mwanaharakati wa wanyonge – akawafundisha watu thamani ya upendo, haki, na msamaha. Hakuogopa kusema ukweli mbele ya watawala dhalimu. Kwa misimamo hiyo, aliteswa, akasulubiwa – lakini maisha yake yamekuwa hadithi nzuri iliyojaa matumani na yenye kusisimua vizazi hadi vizazi
Haya utasema Yesu alikuwa Mungu aliyejifanya mtu hivyo, huwezi kujilinganisha nae. Patrice Lumumba, kijana kutoka Kongo, alisimama kidete kutetea uhuru na heshima ya watu wake dhidi ya ukoloni. Alitaka Afrika ijitambue, ijiongoze, na ijitegemee. Kwa misimamo yake hiyo thabiti, aliuawa kikatili, lakini jina lake limebaki kuwa mfano wa kizazi cha Afrika kinachojitambua.
Thomas Sankara, akiwa na miaka 33, alipindua utawala wa kifisadi na kuanzisha serikali ya watu nchini Burkina Faso. Alipambana na rushwa, alikata mishahara ya viongozi, alikemea unyonyaji wa kimataifa, na kuwapa wananchi wake matumaini mapya. Alipigwa risasi na kuondolewa madarakani, lakini alama ya uadilifu aliyoacha imeendelea kuhamasisha Afrika nzima.
Steve Biko, kijana wa Afrika Kusini, alianzisha harakati za Black Consciousness – harakati za kuamsha utambuzi wa watu weusi. Aliamini kwamba ukombozi wa mwili huanza na ukombozi wa fikra. Aliteswa hadi kufa akiwa mahabusu kwa sababu ya msimamo wake wa kusema ukweli. Leo hii, jina lake linaheshimiwa kote duniani.
Martin Luther King Jr. alipigania haki za kiraia za watu weusi Marekani. Akiwa mchungaji na mwanaharakati, aliongoza maandamano ya amani, alihubiri dhidi ya ubaguzi, na akaandika historia kupitia hotuba yake maarufu ya "I Have a Dream." Alipigwa risasi na kuuawa akiwa na miaka 39, lakini dunia bado inaimba ndoto yake.
Baba wa Taifa letu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, kijana wa Kitanzania aliyesimama kidete kutetea uhuru wa Tanganyika kutoka kwa wakoloni. Alijitolea kwa elimu na siasa za ujamaa na kujitegemea. Aliamini katika utu, usawa, na mshik**ano wa kitaifa. Hata baada ya kung’atuka madarakani, aliendelea kuwa sauti ya busara kwa bara la Afrika.
Mashujaa hawa hawakuishi maisha marefu sana – lakini waliishi maisha yenye maana, wakiacha alama isiyofutika katika historia ya mataifa yao na dunia.
Tanzania ya sasa inahitaji kizazi kipya cha mashujaa ambao wako tayari kusimama na kuhesabiwa. Ukiachilia Manyanyaso ya Kisiasa yanayowakumba Viongozi k**a Tundu LissuTaifa letu linakumbwa na huduma duni za afya – wagonjwa wanakufa kwa kukosa dawa, vifaa na matibabu stahiki. Sekta ya elimu imepoteza dira; shule nyingi zinazalisha vijana wasioweza kujitegemea wala kuleta suluhisho kwa changamoto zinazolikumba taifa. Wahitimu hawana ujuzi, hawana maarifa ya kujiajiri wala kuchangia maendeleo ya taifa.
Kwa mujibu wa Ripoti ya CAG Uchumi wa nchi unadidimia, Umaskini unaimarika na unaenea mijini na vijijini. Ufisadi umetamalaki, Mashirika ya Umma yamepata Hasara ya Kutisha inayohusishwa na Watu kujichotoa mabilioni ya shilingi, Matumizi mabaya ya fedha k**a Kununua Magari ya kifahari na ya anasa kwaajili ya Viongozi pamoja na kuwajengea nyumba.
Vijana wamelazimishwa kuwa vibaraka wa kisiasa badala ya kuwa viongozi wa mabadiliko. Serikali ya CCM imejikita katika udhibiti wa fikra huru, matumizi ya nguvu, na ukandamizaji wa haki za kiraia. Sheria kandamizi zinawanyima Watanzania uhuru wa kujieleza, kuandamana, na kushiriki kikamilifu katika mchakato wa kidemokrasia.
Tangu mwaka 2010 kumekuwa na Wito kwa Mamlaka za serikali na Bunge kwamba Katiba ya mwaka 1977 ni kikwazo kwa mabadiliko ya kweli imezeeka na kuchakaa mithili ya ajuza lakini Viongozi wetu tuliowapa madaraka wamekuwa wakikataa huku wakivimba kwa kiburi na kutoa majibu mabaya yaliyojaa dharau na dhihaka.
Katiba hii Ilitengenezwa kwa maslahi ya chama kimoja, si kwa manufaa ya wananchi. Lakini watawala wamekataa kwa dharau kusikiliza kilio cha mamilioni ya Watanzania wanaotaka Katiba Mpya. Wananchi wamegeuzwa watazamaji wa mfumo unaowanyonya na kuwanyamazisha.
Katika taifa hili, ambapo vijana wengi hujifungia kwenye mitandao kujadili mapenzi na soka, ni nani atakayesimama na kusema: “Niko tayari kulinda haki, uhuru, na utu wa Mtanzania”?
Ni nani atakayeishi maisha yenye thamani kiasi cha kuwafanya wengine walie siku utakapotoweka?
K**a alivyoandika Robin Sharma katika "Who Will Cry When You Die?", maisha ya maana si yale ya kutafuta starehe, bali ya kutafuta sababu ya kuwepo. Ni maisha yanayoambatana na kusudi, moyo wa kujitolea, na nia ya kuacha dunia ikiwa mahali bora zaidi.
Hatuhitaji vizazi vya kupiga picha na kujitundika mtandaoni. Tunahitaji kizazi cha vijana wanaojua wana kazi ya kuiponya Tanzania. Vijana watakaoandika historia mpya, siyo kuitazama tu.
Huu ndio wakati wakuungana na kuwa sehemu ya mabadiliko tuyatakayo. Sisi ndio kizazi cha Mabadiliko tuamke na Tuwe mfano bora wa kuigwa na hadithi nzuri.
Tuishi maisha ya maana. Tuuache urithi utakaoliliwa kwa heshima, si kudharauliwa kwa aibu.
Tarehe 24 April 2025 Siku ya Alhamisi Tukutane Mahak**a ya Hakimu Mkazi Kisutu Kusikiliza Kesi ya Kutunga inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Wakili na Mwanaharakati wa haki za Kiraia Mh. Tundu Lissu.

Mh. Wasira Makamu Mwenyekiti CCM Tanzania

Address

Dar Es Salam
P.O.BOX3814

Telephone

0765443728

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when CHECHEReborn Universities Magazine posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share