23/04/2026
Katika muendelezo wa maadhimisho ya Wiki ya Uhasibu nchini, Chama cha Wahasibu Tanzania (TAA) kimepata fursa ya kutoa elimu ya uhasibu na usimamizi wa fedha kwa wafanyabiashara wa Kariakoo (maarufu k**a βMatycoonβ), hatua iliyolenga kuongeza uelewa na kuboresha uendeshaji wa biashara zao.
Kupitia mpango huo, TAA pia kipo katika hatua za utekelezaji wa Mkataba wa Makubaliano kati yake na vyama vya wafanyabiashara wa Kariakoo. Lengo kuu la ushirikiano huu ni kuhakikisha wafanyabiashara wanapata huduma sahihi, za kitaalamu na kwa wakati kutoka kwa wahasibu waliobobea.
Huduma zitakazotolewa ni pamoja na ushauri wa biashara, uandaaji wa taarifa za fedha, ushauri wa kikodi, usajili na urasimishaji wa biashara, huduma za ukaguzi wa hesabu, pamoja na ushauri kuhusu upatikanaji wa mitaji. Aidha, TAA itaendelea kutoa elimu ya sheria na kuhamasisha uelewa wa masuala ya kisheria yanayohusu biashara.
Hatua hii inatarajiwa kuleta tija kwa wafanyabiashara wa Kariakoo kwa kuwawezesha kufanya maamuzi sahihi ya kifedha na kuendesha biashara zao kwa ufanisi zaidi.
TAA inaendelea kusisitiza kaulimbiu yake ya βSahihi na Hakiβ katika kutoa huduma zake kwa jamii.