Single Parent Family Foundation - SPFF

Single Parent Family Foundation - SPFF We are truly blessed to have a growing base of volunteers who selflessly and passionately possess the desire to help single parent families in need.

Single Parent Children Foundation, “SPCF” is a non-profit organization committed to educating, growth-based training, equipping and empowering single parent families with resources, practical assistance, emotional encouragement and social networking to better their lives, and those of their children; based in Tanzania and the surrounding areas. For my research, I come to realized that, children fr

om single parent families are more prone to su***de, teen pregnancy, behavioral disorders, criminal activity and school avoidance. They also suffer from parental tension, abandonment, effects of moving, fear of change and losing attachment to their parents. To help single parent families navigate through life, SPCF, a non-profit organization, aims to provide access to information and resources, and create online and offline programs. Single Parent Children Foundation hosts a resource directory, a social platform, and serves as an advocate in private, public and the non-profit sector for single parents. The information, resources, and social platform equips and empowers single parent families and helps them do more than they could alone. The three keywords for SPCF are Help, Heal, and Hope. SPCF is committed to breaking this cycle and to help build resource connections for families that help them to become more productive, more resourceful and more informed on how to be the best parent they can be for their children. We focus to continue making a profound difference in the lives of single parent children and their families in the years to come.

19/06/2024

TOFAUTI YA MWANAMKE NA MWANAUME
A. Tofauti za Tabia.�1. Utafiti umegundua kuwa wanaume wanapenda ushindani na wanawake ushirika; Kwa kweli si tu kwamba wanaume hupenda ushindani kuliko wanawake bali pia hufanya vizuri mahali penye mazingira ya ki-ushindani. Tabia hii huonekana hata katika uchaguzi wa aina tofauti ya ucheshi—wanawake hupenda kucheka na wengine na kutumia utani k**a njia ya kufanya wengine wajisikie vizuri; wanaume huwasiliana kwa mizaha, kebehi na vijembe.�2. Kwa ujumla wanaume ni jasiri, huweza kukabili hatari zaidi, na hujihusisha na tabia hatarishi zaidi ya wanawake. Kuna sababu za kibaiolijia kwa jambo hili, ambazo huhusishwa na testosteroni za mwanamume ndani ya mimba, pamoja na kiwango haba cha serotonin kwa wanaume wakilinganishwa na wanawake, na tofauti ya muundo wa ubongo kati ya wanume na wanawake. Kwa upande mwingine, wanawake kwa ujumla ni wapole na wapenda amani wakilinganishwa na wanaume kwa sababu ya tofauti zao za kihomoni (kiwango kikubwa cha serotonin, oxytocin, na estrogen wakilinganishwa na wanaume).�3. Kutokea utotoni hadi uzeeni wanawake wanapenda watoto kuliko walivyo wanaume, na wana uwezo wa kuhisi maono ya mwingine, wapole, wenye uwezo wa kulea kuliko wanaume. Wanawake wana uwezo wa kulea/kutunza kuliko wanaume. Hizi ndizo sababu za kibaiolijia zisababishazo hayo. “Uwezo huo husabishwa na homoni iitwayo peptide oxytocin. Kwa wanaume na kwa wanawake, oxytocin huchochea muunganiko na hisia kuwa katika hali tulivu. Kwa wanaume hii huachiliwa kwa kiwango kikubwa wanapofikia kileleni katika kujamiiana. Kwa wanawake, oxytocin inaachiliwa kwa kiwango kikubwa katika kipindi cha mimba na kunyonyesha.” (Rhoads 2004: 198) Wanawake na wamama wanapenda watoto wadogo kuliko wanaume na wababa. Tafiti zimeonyesha kuwa wanawake wamama wana uwezo mkubwa wa kusoma lugha za mwili kuliko wanaume wababa, kutambua hisia za watoto, kusoma nyuso za watoto, na kutofautisha sauti za vilio za watoto na kelele; watoto wanaonekana kupendelea zaidi sauti za mama zao.�4. Tofauti hizo hapo juu zaweza kuweka msingi wa “pambana-au-kimbia” mwitikio unaojitokeza katika mazingira yanye msongo mkubwa kwa wanaume; kwa upende mwingine, tafiti huonyesha ya kuwa mmwitikio wa wanawake katika mazingira yenye msongo mkubwa huwa ni kwa namna ya “tenda-na- uwe rafiki” kuliko kwa ku“pambana-au-kimbia.” Kutenda kunahusisha kujilinda kibinafsi na uzao dhidi ya madhara; kufanya rafiki huendeleza wazo la kujilinda kwa makundi ambayo hutoa msaada wa pamoja wakati mwanamke anaposhindwa kujihudumia na watoto wake (tazama pia Brizendine 2006: 41-42). Kwa hiyo, wanawake ni wepesi kutumia masaada wa kijamii wawapo katika hali ya matatizo/msongo kuliko walivyo wanaume. Wanaume kitabia hujiunga katika kundi kwa lengo la kushambulia, wanawake kwa lengo la kujikinga.�5. Wanaume na wanawake kwa kawaida wana miitiko tofauti na namna tofauti za kutendea kazi matatizo ya kihisia. Wanaume na wanawake, wote wanapenda na hujisikia vizuri kuwa karibu na watu wenye furaha, lakini ni wanawake peke yao wameripoti ya kuwa wanajisikia vizuri pia wakiwa karibu na mtu mwenye huzuni. Wanaume wanapopitia wakati mgumu kihisia hukwepa kuonana na wengine �6. Ingawaje wanaume na wanawake huripotiwa kuwa huhisi kiwango sawa cha hasira, wanatofautiana katika mchakato wa jinsi wanavyoshughlikia hasira zao. Wanaume, hasa wanaume vijana wana kiwango kikubwa cha testosteroni, hupata hasira haraka, na huonyesha hasira kwa ukali zaidi. Kwa kawaida wanawake hawadhihirishi hasira yao; namna wanavyoonyesha hasira na ukali ni kwa jinsi isiyo wazi ingawaje ni halisi
B. Tofauti za Haiba na Mtazamo.
�1. Ipo tofauti kati ya wanawake na wanaume katika kupendelea na mtazamo kuhusu, kujamiiana na tofauti hiyo huongezeka kadiri wakuavyo.
- Katika ubongo wa wanaume kitovu kinachahusika na swala la kujamiiana ni kikubwa mara 2-21⁄2 zaidi ya kile cha wanawake (Ibid.: 5, 91). Tafiti zinaonyesha kuwa idadi iliyo mara saba zaidi ya wanaume kulinganisha na wanawake, wameripotiwa husikia hamu ya kufanya ngono zaidi ya mara moja kwa siku, na wanawake mara nne zaidi ya wanaume wamesema hawajahisi “chochote kabisa.” Kwa wastani wanaume husema hufikiri kuhusu mapenzi (ngono) kati ya mara tatu hadi tano kwa siku; wanawake husema mara kadhaa kwa wiki au mwezi.
- Katika umri wa miaka 20-30 wanaume hufikiri kuhusu kufanya mapenzi (ngono) zaidi ya mara moja kwa dakika, wakati ambapo wanawake hufikiri mara moja kwa siku, au mara tatu au nne kwa siku katika siku zao za rutuba zaidi (Ibid., 91).
- Kwa wanaume wengi kuliko ilivyo kwa wanawake, kufanya mapenzi ya mara kwa mara na ipendezayo yahusianishwa kwa karibu na furaha katika ndoa. Ndani na nje ya ndoa wanawake husema hujihusisha na ngono ili kushirikiana hisia na mapenzi; wanaume hutoa sababu ambazo ni za kimwili zaidi, k**a vile hitaji la kuridhishwa kingono. Hali kadhalika wanaume wanaofanya uasherati kwa sehemu kubwa hufanya hivyo kwa sababu ya kutafuta ladha na misisimko tofauti katika ngono, wakati ambapo wanawake waweza kufanya hivyo kwa kutafuta utoshelevu wa kihisia wanaoukosa kwa waume wao.
- Wanaponyimwa ngono, wanaume kimsingi watachukia au kukasirika kuliko wanawake (Dondoo 1-3 katika sehemu hii imetoka kwa Rhoads 2004: 26, 48-66, 121, 152-53, 173, na 252).�2. Kiwango cha testosteroni hudhihirika katika, muonekano wa wanaume; vile vile ukweli huo ni sawa kwa wanawake kuhusiana na kiwango cha estrogeni. Kiwango cha estrogeni kina uhusiano na uzuri na rutuba ya uzazi. Homoni hizi zina uhusiano na utungaji wa hisia za mvuto kwa wanaume na wanawake.3 Kwa kawaida wanaume hufikiri kuwa wanawake huvutia zaidi katika kipindi ambacho kiwango chao cha estrogeni kiko juu zaidi (kati ya miaka 20-40); wanawake wenye umri zaidi waonekanao kuwa wadogo kuliko umri wao wana kiwango cha juu cha estrogeni kuliko kile cha kawaida. Kwa hakika, utafiti unaonyesha kuwa uzuri wa mwanamke huathiri ubongo wa mwanamume kimsingi, katika hali k**a ya mwanamume mwenye njaa apatapo chakula au mlevi apatapo dozi. Wanaume huthamini sana uzuri wa maumbile ya wapenzi wao kuliko wanawake kwa wapenzi wao wa kiume. Wanaume huonyesha upendeleo kwa wanawake wenye umri mdogo kidogo kuliko wao, wenye ngozi nyororo, nywele zenye mng’ao, midomo iliyojaa, maumbile yenye kiuno ambacho ni k**a 1/3ya nyonga. Kwa upande mwingine, wanawake hupendelea wanaume wenye nguvu, warefu kidogo kuliko wao, wakubwa kidogo kiumri kuliko wao, hujali pia vyanzo vya mapato vya mwenzi, uwezo na hadhi kuliko wanaume. Matakwa haya yapo kwa wanawake na wanaume wa jamii zote duniani, bila kujali asili au rangi (Ibid.: 56; Brizendine 2006: 61-63, 85-86).�3. Wanawake huthamini ukak**avu, nguvu na ujasiri kwa wenzi wao, ambapo wanaume kwa ujumla hawavutiwi na wanawake wapendao kutawala na huona kuwa wanawake wapendao kutawala na mashindano ya kuwa hawavutii (Rhoads 2004: 152-53, 173).�4. Wanaume huonekana kuwa wakaidi zaidi, wasiopenda kubadilika, na hutaka nafasi zaidi kuliko wanawake; makundi ya wanaume huweza kushik**ana katika kufanya mambo wayapendayo, lakini wavulana huvutiwa zaidi na vitu kuliko watu. Kwa upande mwingine wasichana tangu utotoni huvutiwa zaidi na mahusiano ya karibu na hasa rafiki wa karibu.4 Hivyo, taadhima ya wanaume yatokana na uwezo wao wa kutunza uhuru wao kutoka kwa wengine, wakati kwa wanawake inatokana na uwezo wao wa kutunza mahusiano ya karibu na wengine (Brizendine 2006: 41).�5. Dondoo hizo hapo juu zaonyesha tofauti za msingi za tabia kati ya jinsi k**a inavyoonekana katika Mwanzo 2-3, kabla na baada ya “anguko” la mwanadamu. Wanaume huonekana kuwa na uhusiano wa uhakika na “kazi”na uzalishaji kuliko walivyo wanawake.5 Katika Mwz 2:15 Mungu “akamtwaa
3Rhoads anaongezea kwamba, ingawaje uso wa mwanamume waweza kuonekana wa kiume hasa, wa mwanamke mara chache ungeonekana wa k**e hasa” (Rhoads 2004: 57). Kwa maana hiyo, ingawaje kuna, kwa kweli, viwango tofauti vya testosteroni kwa mwanamume, inaonekana ipo “aina” moja ya msingi kwa mwanamume wakati ambapo, aina tofauti za viwango vya testosteroni huonekana kutokea katika “aina mbili za wanawake” (ina maana. Wale ambao wana sifa za k**e hasa na wale ambao wana sifa na tabia mchanganyiko za k**e na kiume”) (Ibid.: 29-32).
4Brizendine anadondoa ya kuwa mchanganyiko wa oxytosini na dopamini husababisha msingi wa kibaiolojia unaosukuma kujamiiana na matokeo yake ni kupunguza msongo. Uzalishaji wa oxytosini na dopamini huchochewa na estrogeni za ovari wakati wa kubalehe, na kwa wakati wa maisha ya rutuba ya mwanamke. Hii ina maana wasichana waliobalehe hupata raha zaidi katika muunganiko kuliko kabla ya balehe- “ni hisia zile zile za dopamini ambayo walevi wa kokeini au heroini hupata watumiapo madawa hayo” (Brizedine 2006: 37-38).
5Tofauti iliyopo kati ya wanaume na wanawake kuhusiana na kazi na shughuli nyinginezo si swala la akili hasa (jinsi zote zina kiwango sawia cha akili), uwezo, au kipaji – lakini ni za kimwelekeo au mwenendo; tofauti za kihomoni zaonekana kuwa ndizo sababu hasa ya tofauti hizi (Brizendine 2006: 7-8). mwanamume akamweka katika bustani ya Edeni ailime na kuitunza.” Mwanamume pia alipewa wajibu wa kuwapa wanyama majina (Mwz 2:19-20). Zaidi ya hapo, k**a matokeo ya dhambi ya Adamu, adhabu aliyotoa Mungu iliyompasa ilikuwa ni kuilani ardhi, hivyo kuzidisha ugumu wa kazi kwa mwanamume (Mwz 3:17-19). Kwa upande mwingine mwanamke aliumbwa kwa kusudi la kuwa “msaidizi” wa mwanamume (Mwz 2:18-22); hiyo yaonyesha kwa asili wanawake ni thabiti katika kumudu mazingira ya mahusiano. Uwezo wao wa kumudu mazingira huonekana kihalisi, kipekee kwa jinsi wanawake wanavyozaa na kulea. Hali kadhalika dhambi ya Hawa ilihukumiwa adhabu ambayo ilielekezwa katika asili ya mwanamke maalum: maumivu zaidi katika uzazi na mabadiliko ya mahusiano na mume (Mwz 3:16).
C. Uelewa wa Tofauti za Me-Ke Katika kutatua Mizozo.�1. Wanawake wanapofadhaishwa, wanapokwazwa, wanapokuwa na maumivu, huo si wakati wa kuwapa utatuzi, ingawaje hiyo itafaa baadea sana atakapotulia. Mwanamume huridhishwa na ushauri na kukosolewa anapoviomba. Wanaume wanataka kufanya maendeleo wanapohisi kufuatwa k**a watatuzi wa tatizo na si k**a tatizo lenyewe. 2. Wanaume wana uhitaji mkubwa wa hadhi na uhuru (hukazia hali ya upekee na tofauti); wanawake wana uhitaji wa penzi na muunganiko (mkazo katika ukaribu na kuwa sawa).�3. Wanawake huhitaji kupokea matunzo, maafikiano, kuheshimiwa, kupendwa, uhalali, na kuhakikishiwa. Wanaume wanahitaji kuaminiwa, kukubaliwa, kutambuliwa, upendezewaji, kuthibitishiwa, na kutiwa moyo.�4. Wanawake huhamasika wanapojisikia wa kipekee au wanapopongezwa. Wanaume wanahamasika wanapojihisi kuhitajiwa. Hofu kubwa ya mwanamume ni pale ajionapo kuwa na viwango vya chini au visivyo na ushindani, ingawaje hatasema hivyo kamwe (Relationship n.d.).�5. Brizendine anahitimisha akiwa na matokeo ya kazi zake za kitabibu (neuropsychiatry): “Wakati wanaume na wanawake wanapoongezeka umri wa kati na uzeeni, wanapopata uzoefu wa maisha zaidi, na wanapojisikia salama zaidi, mara nyingi hujisikia vizuri sana wakionyesha hisia zao kwa kiwango cha juu, pamoja na wale—hasa wanaume—ambao walikuwa na mkandamizo wa kimawazo. Lakini hatuwezi kukwepa ukweli kuwa wanawake wana uwezo tofauti wa kuhisi, uhalisi, mwitikio na kumbukumbu wanapolinganishwa na wanaume, na tofauti hizi—kutokana na mfumo wa utendaji wa ubongo—ndicho kiini cha migogoro mingi. Evan na Jane walifikia hatua ya kutambua uhalisia uliopo kati yao. Wakati Jane alipoanza kulia ghafla pasipo chanzo kufahamika, Evan alijihoji endapo alishindwa kuwajibika katika eneo fulani. Wakati Jane aliposhindwa kufanya ngono kwa kuwa amechoka, Evan alipambana na utashi wake na kumwelewa. Wakati Evan alipokosa furaha na kuonyesha kukerwa na mwenye hali ya kummiliki, Jane alitambua kuwa hakuwa amemvutia vyakutosha kingono (Brizedine 2006: 133-34)
TOFAUTI ZINGI UTAZIPATA NDANI YA KITABU.

Sijui inatokana nanini, napenda sana watoto wa k**e, yaani hata nikiwa nao 10. Sijui sasa mke wa kunizalia nitampata😀
22/05/2023

Sijui inatokana nanini, napenda sana watoto wa k**e, yaani hata nikiwa nao 10. Sijui sasa mke wa kunizalia nitampata😀

28/01/2023

Address

Box 78191, Ukonga Dar Es Salaam
Dar Es Salaam

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Single Parent Family Foundation - SPFF posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to Single Parent Family Foundation - SPFF:

Share