Fawopa-Tanzania

Fawopa-Tanzania 🌍For Benefit to all together
📖Founded on 18th April 2004 in Tanzania

An NGO based in Mtwara - Tanzania : Building Poverty free and Sustainable Local communities with justice and Equality for, Women, Youths and Children.

05/06/2026

Katika Kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani, Tumevutiwa na Ujumbe Huu Unaowasilishwa na Mtoto Jackline, Ambao unaunga Mkono Kaulimbiu ya Kitaifa; "Dira 2050, Tuwajibike Kukijanisha Tanzania"

Heri ya Siku ya Mazingira Duniani!

Habari, Rafiki yetu!Je, Unafahamu kuwa?Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 (iliyofanyiwa marekebisho 2023) inatamka u...
02/06/2026

Habari, Rafiki yetu!
Je, Unafahamu kuwa?

Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 (iliyofanyiwa marekebisho 2023) inatamka utoaji wa Elimu Bila Ada kuanzia ngazi ya msingi mpaka sekondari. Hata hivyo, sera hii haimaanishi kuwa kila kitu ni bure; inafafanua kuwa serikali inagharimia uendeshaji wa shule (k**a vile vifaa vya kufundishia, ukarabati, na mishahara), wakati wazazi na jamii wana wajibu wa kuchangia malezi na ustawi wa mtoto, ikiwa ni pamoja na chakula.

Miongozo ya serikali kupitia Wizara ya Elimu inasisitiza kuwa utoaji wa chakula shuleni ni jukumu la ushirikiano kati ya:

✅K**ati za Shule: Zinaratibu na kusimamia mchakato.
✅Wazazi/Walezi: Wanachangia chakula chenyewe au fedha.
✅Uongozi wa Vijiji/Mitaa: Unahakikisha usalama na uhamasishaji.

Haya Maelezo yasiwe Mengi...😀😀😀

Bango linajieleza👇👇👇👇👇

Leo ni siku ya NGO duniani, Shirika la FAWOPA tunafurahia siku hii kwakuwa kupitiakazi zetu kwa kipindi cha miaka 20 tum...
27/02/2026

Leo ni siku ya NGO duniani, Shirika la FAWOPA tunafurahia siku hii kwakuwa kupitia
kazi zetu kwa kipindi cha miaka 20 tumefanikiwa kuchangia utekelezaji wa Dira ya taifa 2025, hasa hasa katika kuboresha Maisha ya watu, Tumekuwa na juhudi kubwa katika kuchechemua na kushawishi utungaji wa sera bora, Kutoa elimu ya maswala mbalimbali ya kijamii na maendeleo, Kuunganisha wananchi na fursa mbalimbali zilizopo, na zaidi tunafurahi kuwa sehemu ya msaada kwa Wanawake, Watoto na Vijana wengi nchini Tanzania.

Tunajivunia mafanikio makubwa katika maeneo ya Elimu na Uwezeshaji wa Kiuchumi kati ya maeneo yetu manne ya kipaumbele;
1- Elimu: Kwa kipindi hicho tumeweza kuwasaidia watoto na Vijana elfu 1706 kupata, msaada wa vifaa vya Shule (Stationeries), Mentorship, Lishe na ufadhili wa masomo katika ngazi mbalimbali za kielimu (Fawopa tunatoa kipaumbele kikubwa katika elimu na tunaamini kuwa, Mabadiliko ya kuondokana na umasikini, maradhi na ujinga yanaanzia kwenye Elimu)
2- Uwezeshaji wa Kiuchumi: Tumeweza kuwafikia na kuwawezesha Vijana na Wanawake, 12794 kupitia elimu ya ujasiriamali, mitaji, sambamba na kuwawezesha kuzitambua na kuzitumia fursa mbalimbali katika maeneo yao.

Siku, hii inatupa nafasi ya kujitafakari, na kutafakari mchango wetu katika kujenga, Taifa lenye maendeleo jumuishi ambalo rasilimali zilizopo zinatumika kikamilifu kwa manufaa ya watu wote, na vizazi vijavyo.

Tunaendelea kuwashukuru na kuwakaribisha wadau wetu wa maendeleo ambao wamekuwa na mchango mkubwa katika kufanikisha kazi zetu, Mafanikio haya ni yakwetu sote, Tunatarajia ushirikiano zaidi.

Siku hii inamaana gani kwako?


Fawopa-Tanzania  inaungana na Ujumbe wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania kutoa pongezi za dhati Kwa Wakili Onesmo Olenguru...
29/01/2026

Fawopa-Tanzania inaungana na Ujumbe wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania kutoa pongezi za dhati Kwa Wakili Onesmo Olengurumwa kwa kutajwa kuwa miongoni mwa wagombea bora duniani katika nafasi ya Mshauri Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya watetezi wa haki za binadamu duniani.

K**a wadau wa Haki za Binadamu, Nchini Tanzania Tunathamini Mchango wa Onesmo katika kuendeleza na kulinda haki za binadamu na watetezi wake nchini Tanzania na kwingineko, Tunamtakia kila la Kheri

Tanzania Human Rights Defenders Coalition

Ujumbe wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania unatoa pongezi za dhati Kwa Wakili Onesmo Olengurumwa kwa kutajwa kuwa miongoni mwa wagombea bora duniani katika nafasi ya Mshauri Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya watetezi wa haki za binadamu duniani.

Ni utambuzi muhimu wa dhamira yake ya muda mrefu katika kuendeleza na kulinda haki za binadamu na watetezi wake nchini Tanzania na kwingineko.

———

The EU Delegation to Tanzania warmly congratulates Adv. Onesmo Olengurumwa on being ranked among the top global candidates for the mandate of UN Special Rapporteur on the situation of human rights defenders.

A powerful recognition of his long-standing commitment to advancing and protecting human rights and their defenders in Tanzania and beyond.

Hello, EveryoneWe are now on  LinkedIn Please follow us, www.linkedin.com/company/fawopatzAhsante.
06/01/2026

Hello, Everyone
We are now on LinkedIn
Please follow us, www.linkedin.com/company/fawopatz
Ahsante.

FAWOPA TZ | We believe in 'Shared Prosperity' where Development is Community-led, Sustainable & Inclusive that's Faidika Wote Pamoja | FAWOPA - Faidika Wote Pamoja is a local, women and youth-led non-governmental organization established in 2004 in Mtwara Region, Southern Tanzania. F...

Address

Dar Es Salaam
63114

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Fawopa-Tanzania posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share