Ecotourism Program

Ecotourism Program Spreading knowledge and free market ideas for social economic change.

Kumbukumbu, Dkt Jane akipanda mikoko, Mbweni, Kinondoni, Dar es Salaam   Roots & Shoots USA
03/10/2025

Kumbukumbu, Dkt Jane akipanda mikoko, Mbweni, Kinondoni, Dar es Salaam Roots & Shoots USA

NI UTAMADUNI, UNAENZIWA, NI UTAMBULISHONa Nkungu Hango 30.06.2025UTAMADUNI ni mkusanyiko na muunganiko wa namna jamii fu...
30/06/2025

NI UTAMADUNI, UNAENZIWA, NI UTAMBULISHO

Na Nkungu Hango 30.06.2025

UTAMADUNI ni mkusanyiko na muunganiko wa namna jamii fulani inavyoishi katika maisha yao.

Katika tamaduni kuna mambo ya msingi yanayoibeba na kuitambulisha jamii husika ambavyo ni mila na desturi katika imani zao, mavazi na uvaaji wake, chakula na ulaji wake, uzalishaji wa mali, ndoa na uoaji wake, ngoma na nyimbo zao, michezo yao, uongozi na ufanyaji wa maamuzi yao na mengineyo yenye kuakisi jamii fulani.

Ni kweli utambulisho wa jamii fulani hutokana na utamaduni wao.

Kuna misemo inasema, ukipoteza utamaduni wako, umepoteza utambulisho wako.

Uimara wa utamaduni katika jamii fulani ndiyo msingi wa uimara wa kukuza maendeleo kulingana na nyakati na mabadiliko katika nyanja tofauti za kijamii, kiuchumi, kiuongozi(kisiasa), kiutamaduni na kimazingira.

Kwa sasa baadhi ya jamii zimebadilika kutokana na sayansi na teknolojia, mabadiliko hayo ya sayansi na teknolojia hayajafanya jamii hizo kutokukumbatia utamaduni wao bali misingi yao ya kiutamaduni wameiingiza huko na kuiendeleza kisayansi na kiteknolojia bila kupoteza asili na ladha yao.

Mdau wa Nkungu Hango, Mtaalam Mwandamizi katika Sekta Fedha, Emmanuel Gyuzi, anasema " "Sio jamii za Kihindi tu zinazohifadhi mila hata kwa jamii zingine za Ulaya zinafanya hivyo.

Mathalani nilikuwa masomoni Uholanzi Chuo nilichosoma Erasmus University walikuwa na Programme nyingi tu za kutuletea mafunzo ya uasili wa Uholanzi Kuanzia vyakula na ulaji wake, utengenezaji wa chizi na ngoma zao za asili vile vile kulikuwa na programme za kututembeza kwenye site za makumbusho yao mbalimbali ili kujionea utengezaaji vitu vya asili k**a vIatu vya mbao ambavyo mababu zao walivaank..."

Kuna nguli aliyekuwa mfanyabiashara na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Vodacom Tanzania, Hayati Ali Mufuruki, amewahi kusema kuwa Utamaduni ni bidhaa ya kibiashara inayokua kwa kasi ikiwa imekubatia utajiri mkubwa uliohifadhiwa huko ambao jamii inatakiwa kuwekeza eneo hilo.

Kwa mantiki hiyo, Mufuruki alikuwa anaiasa na kuikumbusha jamii kutambua katika tamaduni zetu kuna utajiri, ijitazame namna ilivyohifadhi utajiri huo, na itafute namna ya kuuwekeza utajiri huo ili uzalishe mapato.

Nikishabihisha maneno ya Bw. Gyuzi na Bw. Mufuruki, unaweza kuiangalia nchi k**a Brazil jinsi inavyofanya vizuri katika kunufaika na utamaduni katika nyanja tofauti ikiwemo sherehe za kitaifa na kimataifa za kitamaduni za samba na nyinginezo.

Tukienda Uchina tunashuhudia wakati usherekeaji wa sikukuu zao, masuala ya kitamaduni ndiyo hushika hatamu katika unogeshaji wa sherehe zao kuanzia mavazi, chakula, ngoma, mapambo, michezo nk.

Kumbuka Wachina wana namna ya kuadhimisha mwaka wao wa Kichina, ni tukio kubwa ambalo Wachina duniani kote hufanya sherehe na inasherehekewa kweli kweli, Mchina akikosa tukio hilo hujihisi katenda kosa kwa nchi yake.

Na nchi za Ulaya karibu zote zinaenzi utamaduni wao nje ya kuwa na utamaduni wa kisasa.

Unaweza kukumbuka mazishi na maziko ya Malkia, Elizabeth yalitawaliwa na masuala ya kitamaduni pia hadi mwili wake ukienda kuhifadhiwa katika nyumba yake ya milele, tukio hilo lilikuwa la kitamaduni lililopelekea wageni waliohudhuria kuzuia kuingia huko kwenye usiri wa kitamaduni (mirimu).

Hata Rais wa Marekani, Joe Biden alizuiwa kuhudhuria tukio hilo la kimila lililofanywa na wahusika tu.

Hata hivyo, Waingereza wote walikuwa wanafuatilia kwa umakini hiyo hatua wakisubiria nje ya Kasri la Kifalme/Kimalkia.

Hapa hatuwezi kusahau matumizi ya maua, bila kununua maua kwenda kuweka kwenye kaburi au mahali maalum palipotengwa itakuwa hujakamilisha maombolezo yako.

Ni utamaduni, unaenziwa, ni furaha na utambulisho wao.

Tukiwatembelea Wahindi, hawa nao wanatupa somo kupitia sherehe za LIWALI ambao Wahindi huazimisha tukio hilo popote walipo wakifungamanisha na ibada za Miungu wao.

Hapa tuangalie malighafi zinazotumika kufanikisha tukio hilo, kiasi gani tukio linaweza kutoa kipato kwa jamii husika.

Nje ya hapo tukio limezalisha umoja, upendo, kukuza imani, mshik**ano, kukuza uchumi, kujenga nguvu ya pamoja na matokeo yake ni uzalendo halisi wenye fungamano na uasili wa Miungu wao.

Nisikupoteze, kumbuka hizi ni tamaduni zenye kuendana na usasa na zinaandaliwa kisasa lakini zimetimiza utamaduni wao wa asili katika usasa au dunia ya leo.

Nikirejea kwetu, utamaduni uko wapi, unaenziwa wapi, bidhaa yake imetambuliwa kiasi gani, nguvu yake iko wapi katika maendeleo na mshik**ano? Tumepoteza.

K**a tulivyoona hapo juu, utamaduni unaileta jamii pamoja, kuiunganisha kuwa na nguvu moja.

Tukitazama hapa kwetu, ni makabila mangapi ambayo bado yanaunganishwa na utamaduni wao na kishik**ana ipasavyo k**a watoto wa mama mmoja.

Bila shaka kila mmoja atakumbuka Wasaai k**a vile wao ndiyo wamezaliwa wakikumbatia utamaduni wao pekee.

Hata watu wengine, wakienda nje ya nchi, wakiambiwa tuonyeshe utamaduni wenu, utashangaa Mnyiramba, Mnyaturu, Mnyaisanzu, Mgogo, ataruka kimasaai na kuivaa kimasaani, eti anaona fahari kwa utamaduni wa kukopa.

Ajabu lakini ndiyo kweli. Hayo makabila niliyoyataja yanawakilisha makabila mengi yaliyokaribu kupoteza uasili wake wa kitamaduni.

Tusiishie hapo, tujiulize, k**a taifa au nchi tunaurithi upi wenye kutufanya au kutuunganisha tuwe kitu kimoja katika kujivunia utaifa wa kiutamaduni.

Utamaduni ni njia ya kipekee yenye muunganiko na Mungu katika kuileta jamii pamoja yenye nguvu na uzalendo wa kujivunia uwepo wao.

Katika uongozi wa Rais, Mh Jakaya Kikwete kulianzishwa mchakato wa kupata Vazi la Taifa ili libebe utambulisho, ila kwa sasa ni zaidi ya miaka 10, bado hakuna Vazi la Taifa, usishangae kwa sababu utamaduni wetu haujapewa kipaumbele kwa sababu wanaoendeleza utamaduni wao walisema wetu ni wa kishenzi.

Ni rai yangu, kwa siku zijazo Utamaduni utakuwa ni bidhaa inayozalisha uchumi k**a tunavyoona kwa wenzetu, nasi tuamke tuanze au tuendeleze kuenzi utamaduni wetu ili tuweze kuwa na utambulisho wetu na kuondokana na dhana kuwa utamaduni wetu ni wa kishenzi.

K**a taifa lenye makabila mengi, hakuna budi, nchi ijikite kuainisha mambo ambayo yanatuweka pamoja k**a vile VAZI LA TAIFA ili tuwe na utambulisho rasmi nk.

Pia kila kabila liwajibike kuirejesha jamii yake katika misingi ya kitamaduni ili liweze kurithisha asili yake kwa kizazi kijacho.

Ni aibu utamaduni wa jamii fulani kufa kisa kukumbatia utamaduni wa kigeni ambao wenye utamaduni wao wanaukumbatia, kuulinda na kuuenzi kwa wivu mkubwa, ukiambatana na imani za kiroho.

Picha: Hisani ya Mitandao

IKIWA leo ni Siku ya Maji Dunia, uhifadhi wa ardhioevu na vyanzo vya maji ni muhimu kwa ustawi endelevu na uhakika wa ma...
22/03/2022

IKIWA leo ni Siku ya Maji Dunia, uhifadhi wa ardhioevu na vyanzo vya maji ni muhimu kwa ustawi endelevu na uhakika wa maisha ya viumbehai.

2022 tuitumie kuiokoa dunia kutokana na mabadiliko ya tabianchi.
01/01/2022

2022 tuitumie kuiokoa dunia kutokana na mabadiliko ya tabianchi.

Je umewahi kufikiria kutembelea hifadhi ya mikoko k**a sehemu ya utalii?
28/12/2021

Je umewahi kufikiria kutembelea hifadhi ya mikoko k**a sehemu ya utalii?

Kuwa sehemu ya mabadiliko kuilinda dunia dhidi ya ongezeko la joto.
23/12/2021

Kuwa sehemu ya mabadiliko kuilinda dunia dhidi ya ongezeko la joto.

Chura
17/12/2021

Chura

Tembelea utalii wa fukwe, ukajionee pori la mikoko aina ya Aviccenia  marina, (Mchu), ili ukafurahie mandhari nzuri yeny...
07/06/2021

Tembelea utalii wa fukwe, ukajionee pori la mikoko aina ya Aviccenia marina, (Mchu), ili ukafurahie mandhari nzuri yenye upepo mwanana, unaotoa 'stress' na kufanya mwili wako ku relax na kuwa mwenye nguvu upya.

02/06/2020

SIKU ya pili ya maadhimisho ya Wiki ya Mazingira Duniani.

Kila mmoja naamini anaweza kuwa anatenga bajeti ya masuala ya usafi na mazingira nyumbani kwake.

Ni ukweli usiopingika kuwa kuna gharama kubwa zinatumika katika kuweka nyumba yako katika mazingira nadhifu,

Je ni wangapi ambao wanatenga bajeti hiyo kwa kushirikishana na familia nzima???

Uwajibikaji katika sekta ya mazingira unaanzia kwa familia na ni kwa kiasi gani tumekuwa mstari wa mbele kuitisha kikao/vikao cha/vya familia kupanga mikakati ya usafi na utunzaji wa mazingira ya nyumba zetu??

Je tumeweza kuwashirikisha mtoto/watoto wetu kwa kiasi gani katika vikao vya bajeti zetu za mazingira ili nae/nao achangie/wachangie mawazo kwa changamoto a/wanazoziona katika harakati zake/zao za kila siku hapo nyumbani??

Msingi wa ukuzaji kizazi huanzia kwa kumjengea uwezo mtoto, mazingira ni kila kitu kinachotuzunguka na kila siku tunapambana nayo katika maisha yetu.

Hebu tuchukue fursa za kufanya vikao vya kibajeti katika masuala ya mazingira majumbani mwetu kwa kuwashirikisha watoto ili wajue thamani na wajibu wao katika utunzaji na uhifadhi wa mazingira.

Hii itapanua wigo mpana kwa mtoto kujua kila kitu chake kinagusa mazingira.

Vivyo hivyo atatambua kuwa mazingira ni msingi wa maendeleo yake na anawajibu wa kuyatunza, kuyalinda na kuyahifadhi kwa mstakabali mwema wa maisha yake na ya kizazi chake kijacho.

Uwajibikaji katika sekta ya mazingira kwa mtoto ni hazina ya kesho yetu iliyohai na imara zaidi.

Na hiyo itasaidia kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Mtoto ni chanzo cha mabadiliko chanya kwa uhifadhi wa mazingira, MPE UWEZO, MPE SAUTI, MUONYESHE NJIA.

Mazingira ni maisha yetu, Maisha yetu yanategemea mazingira.

24/05/2020

Uongozi wa EP unawatakia EID MUBARAK

Kuwa alama ya utamaduni wako. Picha kwa hisani ya rafiki yangu.
12/04/2020

Kuwa alama ya utamaduni wako. Picha kwa hisani ya rafiki yangu.

Address

P. O Box 68080
Dar Es Salaam

Telephone

+255755897906

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Ecotourism Program posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share