13/08/2026
Kwa siku mbili mfululizo, tumepata fursa ya kuambatana na ugeni kutoka Ubalozi wa Ireland nchini Tanzania Embassy of Ireland in Tanzania katika ziara ya kukagua maendeleo ya Mradi wa Climate Smart Agriculture Project II (CSAP II), unaotekelezwa kwa ushirikiano kati ya ActionAid Tanzania na WFP WFP Africa , kwa ufadhili wa Ubalozi wa Ireland.
Katika ziara hii, tumetembelea Wilaya za Chamwino (Nhinhi) na Kongwa mkoani Dodoma, ambapo tumejifunza na kushuhudia kwa vitendo namna mradi unavyowezesha wakulima kupitia kilimo himilivu cha zao la mtama.
Miongoni mwa mambo tuliyoyaona ni matumizi ya umwagiliaji kwa njia ya matone (drip irrigation), juhudi za kuboresha upatikanaji wa lishe na uhifadhi wa chakula, uimarishaji wa vikundi vya wanawake vya kusaidiana, upatikanaji wa masoko ya mazao, pamoja na matumizi ya mashine katika kupura mtama baada ya kuvuna.
Mbinu na teknolojia hizi zinaendelea kuwasaidia wakulima kuongeza uzalishaji, kupunguza changamoto za baada ya mavuno, kuboresha lishe na kuongeza fursa za kipato, huku wakijenga ustahimilivu dhidi ya athari za mabadiliko ya tabianchi.