01/04/2026
Karibu 19% ya chakula chote Duniani (UNEP) huaribika Kila mwaka kwa kuzalisha taka za Kuoza, kiasi hichi huchochea kuzalisha kwa hewa ukaa na huaribu Rasilimali muhimu k**a vile udongo, maji nk.
Katika muendelezo wa Siku ya Kimataifa ya Taka Sifuri, Mazingira Plus tuliungana na Manispaa ya Temeke, TCCI, na United Planet katika kuadhimisha siku tajwa kwa kutoa mafunzo kwa vijana 40 kutoka taasisi mbalimbali, vyuo vikuu, na wanafunzi wa shule za Sekondari kuhusu kubadili Taka za Kuoza na kuwa mbolea ya asili (mboji) kwa nadharia na vitendo katika shule ya Sekondari Kibasila - Manispaa Temeke.
Toka mwaka 2023 Mazingira Plus kwa kushirikiana na TCCI tumekuwa tukitekeleza mradi wa Taka Sifuri ngazi ya Shule ili kubadili tabia za wanajamii za kutenganisha taka katika umri sahihi.
Tunaishukuru sana ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke, Uongozi wa taasisi ya TCCI, United Planet nk kwa ushirikiano na uratubu wa pamoja.