08/10/2026
📍Tulikutana tarehe 01 Octoba 2026 nna wadau mbalimbali wa Elimu pamoja na RYC’s na kuzungumza kwa lengo moja tu - Kujadili changamoto zinazowakabili wanafunzi, walimu na jamii, pamoja na mahitaji muhimu ya kuboresha ubora, usawa na ujumuishi wa elimu.
📌 Kushirikishana uzoefu kuhusu namna taarifa zinavyokusanywa na kuchakatwa kuanzia ngazi ya shule, wilaya na mikoa hadi kufikia ngazi ya kitaifa, pamoja na namna taarifa hizo zinavyoweza kutumika katika kupanga na kufanya maamuzi sahihi katika sekta ya elimu.
📌 Kujadili umuhimu wa kuwashirikisha wadau mbalimbali, hususan jamii, vijana na makundi yaliyo pembezoni, katika michakato ya kupanga, kutenga, kutumia na kufuatilia rasilimali za elimu ili kuhakikisha fedha za elimu zinawanufaisha wanafunzi wote kwa usawa.
📌 Kujenga jukwaa la kubadilishana uzoefu, maarifa na mbinu bora kati ya vijana wa vijijini, Serikali, mashirika ya kiraia na wadau wengine, huku kikisisitiza umuhimu wa uwajibikaji na ushiriki wa vijana katika kuimarisha mifumo ya elimu.
📌 Kubadilishana uzoefu kuhusu namna jamii na vijana wanaweza kutumia taarifa, ushahidi na ushiriki wa wananchi kufuatilia utekelezaji wa mipango ya elimu na kushirikiana na wenye dhamana katika kutafuta suluhisho.