23/01/2026
MAOMBI YA SHUKURANI•
🔥Asante Bwana Yesu kwa zawadi ya uhai katika mwezi huu na mwakahuu
🔥Asante Mungu kwa zawadi ya kulala, kuamka, katika mwezi huu na pia kwa sababu, ya rehema zako na hifadhi njema.
🔥 Mwezi huu, pesa zinazokusudiwa kwa ajili yangu kuwa baraka hazitatumika kwenye mazishi yangu/ya familia kwa jina kuu la Yesu. nitaishi (Zaburi 118:17).
🔥 Ee Bwana Yesu, Baba yangu! Tafadhali, fanya maisha yangu na ujaribu kunifanikisha sana dhidi ya tabia mbaya zote katika mwezi hu kwa jina kuu la Yesu.
🔥 Kazi yangu yote mwezi huu izae kitu kizuri, katika jina la Yesu.
🔥Mwezi na mwaka huu utaleta mafanikio ya ghafla, Furaha na vicheko maishani mwangu kwa jina kuu la Yesu.
🔥Naamuru kwa jina kuu la Yesu, mwaka huu ndoto na maono yangu yote mema yataanza kudhihirika kwa jina kuu la Yesu.
🔥2026 naamuru! Maadui zangu wapende wasipende, mambo mazuri hayatanipita kamwe, kwa jina la Yesu.
🔥Katika mwaka huu, nitavaa taji la Utukufu wangu kwa jina kuu la Yesu.
🔥Ee Bwana Yesu, acha Wasaidizi wapya na Fursa zianze kunipata kwa jina kuu la Yesu. Ninaahidi kushuhudia na kutimiza nadhiri zangu.
🔥Utukufu wa Mungu, Kibali cha Mungu, Rehema za Mungu, zianguke juu ya maisha yangu na acha maisha yangu yasonge mbele kihuduma, kifedha, kindoa (taja) kwa jina kuu la Yesu.
🔥Ee Bwana Yesu, nijalie nipate uzoefu na kukutana nawe kwa nguvu mwezi huu, katika jina la Yesu.
🔥Naamuru! 2026 mwaka wangu wa milango wazi ya Kimataifa, Kazi za faida, ndoa katika jina kuu la Yesu (Anza kutaja kwa kutabiri - Ayubu 22:28).
🔥Ee Bwana Yesu achilia malaika wako watakaonisaidia katika maeneo yote Mwaka huu na wanipate sasa kwa jina kuu la Yesu.
🔥Malaika niliopewana Mungu,watawaangamiza maadui na maadui hawatanipita kwa jina la Yesu.
🔥 mtu yoyote aliyenibebesha mizigo kwenye maisha yangu mizigo ya magonjwa, umaskini, kukataliwa, madeni hiyo mizigo irudi mara saba juu yao, hiyo mizigo ya kukataliwa imrudie mara saba kwa Damu ya Yesu Kristo.
🔥 Roho yoyote inayoibua matatizo miezi iliyoko mbele yangu hiyo roho inayoibua magonjwa yanayopelekea kutumia fedha iliyokusudiwa kufanya malengo fulani hiyo roho iwake moto kwa jina la Yesu Kristo.
*Hosea 14:7*
🔥 Eeeh Bwana Yesu naomba nguvu ya urejesho vile vitu vya thamani ambavyo nimevikosa miaka iliyopita....naomba nguvu yako mwaka huu nvipate kwa wepesi.....nguvu ya kumalisha nifanye vitu vinavyoonekana......kwa jina la Yesu Kristo.
🔥 Eeeh Mungu Baba tunaomba harufu nzuri ya manukato ya Roho wako Mtakatifu wale watu wazuri walioondoka kwenye maisha yetu watutafute na watupate kwa jina la Yesu Kristo....
🔥 Eeeeh Mungu Baba ile harufu nzuri iliyopotea ndani yangu iingie ndani yangu Harufu nzuri ya manukato ya Roho wa Mtakatifu iingie kwenye maisha yangu watu wazuri wanitafe wanipate.......
🔥 Eeeh Mungu Baba kwa Damu ya Yesu niangusha kila utawala uliokaa juu yangu, kiti cha enzi cha shetani kianguke kwa jina la Yesu Kristo
*Zaburi 57:6*
[6]Wameweka wavu ili kuninasa miguu;
Nafsi yangu imeinama;
Wamechimba shimo mbele yangu;
Wametumbukia ndani yake!
🔥 Eeeh Bwana Yesu kila shimo walilochimba juu yangu watumbukie wenyewe, kila aibu walioandaa iwapate wao, kila maneno waliyonena juu yangu yawarudie wenyewe natuma malaika waende kuwahukumu kwa maneno ya vinywa vyao kwa Damu ya Yesu Kristo.
*Isaya 60:1*
"Ondoka uangaze kwa kuwa Nuru imenizukia,"
🔥 Eeeeh Mungu Baba Utukufu wako uangazie maisha yangu Ktk mwaka huu, Nuru ya Bwana iangazie maisha yangu katika maeneo yote ya maisha yangu....popote nitakapokwenda Utukufu wako uangazie maisha yangu
- MAAGIZO YA KINABII
✍🏿Omba mambo makuu 3 unayotamani mwaka huu kwa jina kuu la Yesu kwa "Imani ya Adamu". Tafadhali omba kwa Imani na kwa dhamira.
✍🏿Tabiria ombi lako kwa SADAKA YENYE UDHIHURISHO WA DAMU YA YESU kisha tazama kitakachofuata.. "Dunia itasherehekea pamoja nawe kwa jina kuu la Yesu".
✍🏿Chukua k**a dakika 10 kumwimbia Mungu sifa kabla ya kumaliza maombi yako
Asante Yesu kwa kujibu maombi yangu kupitia mamlaka yenye nguvu na uwezo wako.Yafunike maombi yako kwa damu ya Yesu Kristo Ameni, Ameni. Imekuwa• Napokea ushindi mkuu kuanzia sasa, nimevuka•
Ukisikia amani ndani yako ya kuachilia sadaka yako baada ya maombi haya katika muda na lango hili waweza kufanya hivyo na Mungu akitenda usisahau kunipa ushuhuda wako.
Be blessed