02/06/2026
Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA) tumefanya mafunzo ya kuongezea ujuzi wadau wa sekta ya utoaji haki (Justice sector actors) katika masuala ya Ukatili wa kijinsia kwenye Halmshauri ya wilaya Arusha.
Wadau walioshiriki ni pamoja na viongozi wa serikali za mitaa, wasaidizi wa Kisheria, Afisa ustawi wa jamii, Dawati la polisi la jinsia na watoto, na Mawakili wa Serikali waendesha mashtaka.
Mafunzo hayo shirikishi yalilenga kutambua majukumu ya wadau hao, kuimarisha ushirikiano baina yao na kuimarisha misingi ya kulinda utu wa wahanga wa vitendo vya ukatili wa kijinsia wakati wakitoa taarifa, upelelezi na uendeshaji wa kesi.