NACOPHA

NACOPHA Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from NACOPHA, Non-Governmental Organization (NGO), Dar es Salaam.

Strengthening  Community Support Groups  for Sustained Access to HIV, SRHR  and GBV Services among Adolescents and Young...
06/01/2026

Strengthening Community Support Groups for Sustained Access to HIV, SRHR and GBV Services among Adolescents and Young People in Kasulu DC, Kasulu TC and Uvinza DC-Kigoma Region

At the end of December 2025, NACOPHA, in collaboration with NYP+ and with support from UNAIDS, conducted an orientation for Adolescents and Young People (AYP) across three Councils of Kasulu TC, Kasulu DC, and Uvinza DC. The orientation aimed to equip AYP data collectors with ethical, effective, and high-quality approaches for community-led monitoring (CLM) and project implementation. As part of the exercise, participants also received working tools that includes tablets to enhance efficient, timely, and reliable data collection within their communities. This initiative strengthens community support structures and promotes sustained access to HIV, SRHR, and GBV services for Adolescents and Young People in Kigoma Region.

Leo tunaungana na dunia kuadhimisha Siku ya UKIMWI Duniani. Tuongeze nguvu kwenye mwitikio, tupaze sauti dhidi ya unyany...
01/12/2025

Leo tunaungana na dunia kuadhimisha Siku ya UKIMWI Duniani. Tuongeze nguvu kwenye mwitikio, tupaze sauti dhidi ya unyanyapaa, na tuhakikishe kila mmoja anapata huduma na elimu sahihi. Pamoja tunaweza kutokomeza UKIMWI.

Baraza la Taifa la Watu Wanaoishi na VVU Tanzania linawasihi WAVIU wote nchini kuendelea kupata huduma na matibabu ya AR...
25/11/2025

Baraza la Taifa la Watu Wanaoishi na VVU Tanzania linawasihi WAVIU wote nchini kuendelea kupata huduma na matibabu ya ARVs bila wasiwasi katika vituo vyote vya kutolea huduma za VVU na kuwa huduma hizi ni bure nchni kote. Tunaendelea kutetea haki, ufuasi sahihi wa tiba, na ustawi wa WAVIU wote.
Havionekani, Haviambukizi.

18/12/2024

Matumizi ya ARV ni HALISI.

Tumia ARV kwa USAHIHI ili UFUBAZE VVU. Matokeo yake utaishi na VVU bila kushambuliwa, bila kuambikiza na ukipima HAVITAONEKANA. Ila haimaanishi vimeisha, VINAFUBAA TU.

Endelea kutumia ARV zako kwa USAHIHI.

Havionekani=Haviambukizi

YALIYOJILI WAKATI WA KONGAMANO LA KITAIFA LA KISAYANSI NA UZINDUZI WA USAMBAZAJI WA RIPOTI YA UTAFITI WA VIASHIRIA NA MA...
30/11/2024

YALIYOJILI WAKATI WA KONGAMANO LA KITAIFA LA KISAYANSI NA UZINDUZI WA USAMBAZAJI WA RIPOTI YA UTAFITI WA VIASHIRIA NA MATOKEO YA UKIMWI MWAKA 2022 - 2023 LEO NOVEMBA 29, 2024 MKOANI RUVUMA.

Aliyosema Waziri wa Afya, Mhe. Jenista Mhagama.

# Leo tunazindua usambazaji wa ripoti ya matokeo ya utafiti wa viashiria vya UKIMWI mwaka 2022 - 2023 katika Kongamano lililohusisha wadau kutoka maeneo mbalimbali nchini. Takwimu hizi zitasaidia makundi mbalimbali katika mipango ya maendeleo.

# Ripoti hii ya utafiti inaiwezesha Tanzania kufahamu hali halisi ya kiwango cha maambukizi ya VVU pia kuonesha mafanikio, changamoto na mikakati inayopaswa kuchukuliwa katika mapambano dhidi ya VVU.

# Nalipongeza sana Baraza la Watu wanaoishi na VVU nchini Tanzania (NACOPHA) kwa kuwa imara kuishauri Serikali na kuwaelimisha Watanzania kuhusu mapambano dhidi ya VVU.

# Kiwango cha ushamiri wa maambukizi ya Virusi vya UKIMWI nchini Tanzania kimepungua kutoka 7% mwaka 2003/2004 mpaka 4.4% mwaka 2022/23 pia kiwango cha maambukizi ya VVU kutoka mwa Mama kwenda kwa mtoto kimepungua kutoka 18% mwaka 2010 hadi 8.1% mwaka 2023 na sasa usalama wa watoto ni mkubwa.

# Natoa wito kwa viongozi wenzangu na watu wenye uwezo wa kusambaza taarifa hizi wakiwemo wanamichezo, viongozi wa dini, wanasiasa, waandishi wa habari washiriki kikamilifu katika usambazaji wa takwimu hizi.

Makamu M/Kiti wa Baraza akipokea maelezo kuhusu Shughuli za Vikundi katika Banda la NACOPHA lililopo Kijiji Cha Jamii...
28/11/2024

Makamu M/Kiti wa Baraza akipokea maelezo kuhusu Shughuli za Vikundi katika Banda la NACOPHA lililopo Kijiji Cha Jamii...

Mdahalo wa vijana na viongizi wa dini na kimila umeanza na umezinduliwa rasmi na RAS wa Ruvuma. Mdahalo umeanza kwa kuan...
28/11/2024

Mdahalo wa vijana na viongizi wa dini na kimila umeanza na umezinduliwa rasmi na RAS wa Ruvuma. Mdahalo umeanza kwa kuangazia mchango na majukumu ya viongozi wa dini katika kupambana na maambukizi ya VVU na UKIMWI. Viongozi wa dini wamewakilishwa dini ya kiislamu na kikristo. Kwa ujumla viongozi wa dini wamejadili yafuatayo:
1. Viongozi wa Dini wananafasi kubwa ya kutoa elimu kuhusu masuala ya VVU na UKIMWI pamoja na masuala ya afya ya uzazi.
2. Viongozi pia wana nafasi kubwa sana ya kuhakikisha wanapambana na unyanyapaa na unyanyasaji wa watu wanaoishi na maambukizi ya VVU
3. Viongozi wa dini wanajukumu la kuonya, kusisitiza na kukalipia tabia hatarishi

Katika maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani mwaka 2024 Kitaifa. NACOPHA inaungana na Serikali na Wadau kushiriki maadhi...
28/11/2024

Katika maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani mwaka 2024 Kitaifa. NACOPHA inaungana na Serikali na Wadau kushiriki maadhimisho hayo mkoani Ruvuma. WAVIU katika makundi ya Vijana, Wanawake, Watu wenye Ulemavu, na Wanaume wameshiriki maandamano ya Ufunguzi wa Maadhimisho hayo yakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe. Kanali. Ahmed Abbas Ahmed.

Address

Dar Es Salaam
DARESSALAM

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when NACOPHA posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to NACOPHA:

Share