Shabu Foundation

Directions

Shabu Foundation Tunagusa maisha kwa elimu, afya, mazingira & maendeleo ya jamii.
🌍 Tanzania | 📩 DM for collaboration

MATOKEO YANAONGEAMnufaika mwingine wa Mradi wa KESHO YANGU ameendelea kuonesha matunda ya mafunzo kwa vitendo 💪🏽Batiki h...
27/01/2026

MATOKEO YANAONGEA

Mnufaika mwingine wa Mradi wa KESHO YANGU ameendelea kuonesha matunda ya mafunzo kwa vitendo 💪🏽
Batiki hizi ni ushahidi kuwa ujuzi ni mtaji wa maisha, na pale fursa inapokutana na nia, ndoto huanza kutimia.

Tunaendelea kuibua vipaji, kujenga uwezo, na kufungua milango ya kujitegemea kwa wasichana na vijana wetu.

Shukrani kwa kila mmoja anayesimama nasi katika safari hii ya kugusa maisha 🙏🏽



KESHO YANGU



NDOTO ZINAANZA KUTIMIAMatokeo halisi ya NDOTO ITIMIE HUB – SE1 💙Mnufaika wetu ameweza kutengeneza batiki bora kwa mikono...
11/01/2026

NDOTO ZINAANZA KUTIMIA

Matokeo halisi ya NDOTO ITIMIE HUB – SE1 💙

Mnufaika wetu ameweza kutengeneza batiki bora kwa mikono yake mwenyewe, baada ya kushiriki mafunzo chini ya Mradi wa KESHO YANGU.

Huu sio tu ujasiriamali
👉 ni ujuzi
👉 ni tumaini jipya
👉 ni hatua ya kujitegemea

Shukrani kwa wote waliogusa maisha haya kwa namna moja au nyingine. Safari bado inaendelea, na ndoto nyingi zaidi zipo njiani kutimia 🌱

Tunagusa Maisha.
Naijenga Kesho Yangu Bora.






RIPOTI FUPI YA TUKIO – NDOTO ITIMIE HUB SE1 & UZINDUZI WA MRADI KESHO YANGULeo tumeshuhudia hatua muhimu katika safari y...
30/11/2025

RIPOTI FUPI YA TUKIO – NDOTO ITIMIE HUB SE1 & UZINDUZI WA MRADI KESHO YANGU

Leo tumeshuhudia hatua muhimu katika safari ya .

Tukio letu la NDOTO ITIMIE HUB SE1 limefanyika kwa mafanikio makubwa, likiwaunganisha mabinti wenye malengo na ari ya kujifunza.

Washiriki wote walijifunza kwa vitendo, walipata ujuzi wa kutengeneza batiki na sabuni ya maji, na zaidi ya yote waliinuka kifikra na kuamini katika ndoto zao.

Katika shamrashamra na hamasa kubwa, tumefanikiwa pia kuzindua rasmi Mradi wa KESHO YANGU, mradi unaolenga kuwa msaada wa elimu, ujuzi na fursa kwa vijana na yatima.

Uzinduzi huo umefanywa na Mheshimiwa Abdallah Chibwana, Mjumbe wa Serikali ya Mtaa wa Dovya, Chamazi, ambaye amepongeza jitihada za Shabu Foundation katika kugusa maisha ya jamii.

Tukio hili limeacha alama ya matumaini, furaha na mwanga mpya kwa mabinti wote 15 walio shiriki.

Ni mwanzo mzuri wa safari ndefu ya kuwajengea vijana wetu kesho iliyo bora, imara na yenye thamani.

Shabu Foundation
Tunagusa Maisha.

TAARIFA NJEMA kutoka SHABU FOUNDATION 💚Tarehe 11 Novemba 2025, Shabu Foundation kupitia mradi wa KESHO YANGU imefanikish...
12/11/2025

TAARIFA NJEMA kutoka SHABU FOUNDATION 💚

Tarehe 11 Novemba 2025, Shabu Foundation kupitia mradi wa KESHO YANGU imefanikisha kuwapeleka mabinti wawili kuanza mafunzo ya ushonaji katika kituo cha Styles & Skills Tailoring Hub.

Hatua hii ni sehemu ya jitihada zetu za kuwawezesha wasichana waliopo katika mazingira magumu kupata ujuzi wa kujitegemea na kujenga maisha bora.

Tunapenda kutoa shukrani za dhati kwa wote waliogusa, kuchangia, na kuunga mkono safari hii ya matumaini.
Kwa pamoja, tunagusa maisha — tunajenga kesho bora. 💫

📍 Shabu Foundation – Tunagusa Maisha

Kwa heshima na upendo, Shabu Foundation kupitia mradi KESHO YANGU tunazindua rasmi hatua ya kwanza ya mafunzo chini ya p...
08/11/2025

Kwa heshima na upendo, Shabu Foundation kupitia mradi KESHO YANGU tunazindua rasmi hatua ya kwanza ya mafunzo chini ya programu NDOTO ITIMIE HUB.

Katika awamu hii, wasichana 15 kutoka mazingira magumu watapata mafunzo ya vitendo ya kutengeneza batiki na sabuni ya maji, lengo likiwa kuwawezesha kujipatia kipato halali, kujiamini, na kujenga msingi wa kujitegemea.

Kwa nini haya mafunzo ni muhimu?

Wengi hawana fursa ya kusoma au kupata ajira

Ujuzi mdogo unaweza kubadilisha maisha kabisa

Tunapunguza utegemezi na kuongeza kipato cha familia

Tunawajenga mabinti kuwa wanawake wenye nguvu, thamani na uwezo

📍 Chamazi, Dovya – Dar es Salaam
🗓 29/11/2025
⏰ 04:00 Asubuhi

Tunawaalika:
✅ Wadau wa maendeleo
✅ Wafadhili
✅ Makampuni yanayoweza kusaidia vifaa
✅ Watu wenye moyo wa kujitolea

Kwa ushiriki au ufadhili:
📞 0780 940 110
📩 [email protected]

"Kesho Yangu – Naijenga Kesho Yangu Bora"

*“NDOTO ITIMIE HUB”*Hapa tunawapa mabinti na vijana ujuzi wa vitendo wa ujasiriamali – kuanzia batiki, sabuni ya maji na...
06/11/2025

*“NDOTO ITIMIE HUB”*
Hapa tunawapa mabinti na vijana ujuzi wa vitendo wa ujasiriamali – kuanzia batiki, sabuni ya maji na bidhaa za kujitengenezea kipato.
Lengo letu ni moja: kuibadilisha ndoto kuwa ajira.

Tunakemea utegemezi, tunajenga uwezo, na tunawasha matumaini.

Tunagusa maisha kwa mikono ya ubunifu.

🕊️ KESHO YANGU | Naijenga Kesho Yangu Bora 🕊️Tunayo furaha kutambulisha rasmi Mradi wa KESHO YANGU, mpango maalum wa kuw...
29/10/2025

🕊️ KESHO YANGU | Naijenga Kesho Yangu Bora 🕊️

Tunayo furaha kutambulisha rasmi Mradi wa KESHO YANGU, mpango maalum wa kuwasaidia watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira magumu kupitia elimu, ujuzi na malezi bora ya kijamii.

Kupitia mradi huu, tunalenga kuwajengea watoto na vijana wetu maarifa ya kujitegemea, uongozi wa maadili, na ndoto zenye mwelekeo wa mafanikio.

🎯 Lengo Kuu:
Kuwajengea vijana na watoto msingi imara wa maisha bora kwa kuwapatia ujuzi wa kazi k**a ushonaji, batiki, sabuni, useremala, na fursa za elimu.

🤝 Tunakaribisha wadau wote, mashirika, na watu wenye moyo wa kusaidia kushirikiana nasi kujenga kesho yenye matumaini zaidi kwa vijana wetu.

📍 Mradi huu unatekelezwa na shabu_foundation
📞 0780 940 110
📧 [email protected]

📍 Dovya, Chamazi – Temeke

Kauli mbiu: “Tunagusa Maisha, Tunajenga Kesho Bora.” 💚

MLO WA UPENDO – SE2 | Tarehe 25/10/2025Tumekamilisha tukio letu la Mlo wa Upendo kwa mafanikio makubwa.Tumekula, tumeshi...
26/10/2025

MLO WA UPENDO – SE2 | Tarehe 25/10/2025

Tumekamilisha tukio letu la Mlo wa Upendo kwa mafanikio makubwa.
Tumekula, tumeshirikiana, tumecheka na watoto yatima, na zaidi tumezindua rasmi mradi wetu KESHO YANGU.

Tunatoa shukrani za dhati kwa:
✅ Wafadhili wote waliogusa maisha ya watoto hawa
✅ Wageni wa heshima waliohudhuria
✅ Walimu na wajitolea waliofanikisha kila hatua
✅ Timu ya maandalizi na wenye nia njema

Kwenu—tumegusa tabasamu na kuamsha matumaini. 💛

Tunaendelea kusema:
“Tunagusa Maisha”

Tukio letu pendwa la Mlo wa Upendo Se2 ni kesho tukio hili litakuwa live Youtube katika channel ya  karibu ujumuike nasi...
17/10/2025

Tukio letu pendwa la Mlo wa Upendo Se2 ni kesho tukio hili litakuwa live Youtube katika channel ya karibu ujumuike nasi

MLO WA UPENDO SE2Shabu Foundation kupitia mradi “Tabasamu Letu” tunawaalika wadau, marafiki na watu wa moyo wa huruma ku...
02/09/2025

MLO WA UPENDO SE2
Shabu Foundation kupitia mradi “Tabasamu Letu” tunawaalika wadau, marafiki na watu wa moyo wa huruma kushiriki nasi katika safari ya kugusa maisha ya watoto yatima.

🙏 Changia leo ili mtoto apate chakula na tabasamu jipya la matumaini.
➡️ Kila shilingi yako ni faraja na baraka kwao.

📞 Mawasiliano: +255 780 940 110
📧 [email protected]

Pamoja tunaweza kujenga kesho yenye mwanga. ❤️

Shabu Foundation


Address

Dovya/Chamazi
Dar Es Salaam

Opening Hours

Monday 08:00 - 15:00
Tuesday 08:00 - 15:00
Wednesday 08:00 - 15:00
Thursday 08:00 - 15:00
Friday 08:00 - 15:00
Saturday 08:00 - 15:00

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Shabu Foundation posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share