08/06/2026
Kuimarisha Upatikanaji wa Haki kwa Wote!
WiLDAF Tanzania kwa kushirikiana na Wizara ya Katiba na Sheria ilishiriki katika Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia (MSLAC) Awamu ya Pili katika Wilaya ya Kishapu, Mkoa wa Shinyanga.
📍 Kata 28 na vijiji 36 vilifikiwa
👥 Wananchi 54,869 walipatiwa elimu ya kisheria
⚖️ Migogoro 44 ilitatuliwa papo kwa papo
Kupitia kampeni hii, wananchi walipata elimu na huduma za msaada wa kisheria kuhusu masuala ya ardhi, ndoa na talaka, mirathi, wosia, matunzo ya watoto, ukatili wa kijinsia pamoja na huduma za usuluhishi na uandaaji wa nyaraka za kisheria.
Mafanikio haya yanaonesha umuhimu wa kuendelea kupeleka huduma za msaada wa kisheria karibu na wananchi ili kuimarisha uelewa wa sheria, haki za binadamu na utawala bora.
WiLDAF Tanzania itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali kuhakikisha kila mwananchi anapata haki, elimu ya kisheria na fursa sawa bila ubaguzi.