Youth4PeaceAgenda Tanzania

Youth4PeaceAgenda Tanzania A youth-led mobilization in championing realization and implementation of Youth, Peace, and Security Agenda in Tanzania.

18/06/2026

Amani ni zaidi ya kukosekana kwa vita.
Amani ni hali ya utulivu wa ndani, mshikamano katika jamii, heshima kwa kila mmoja, na uwepo wa haki na usawa kwa wote.

Ni pale tunapoweza kuishi kwa usalama, kushirikiana bila hofu, na kujenga mazingira yanayowezesha kila mtu kufikia ndoto zake.

Amani ni vitendo vya kila siku, kuheshimiana, kusaidiana, na kutatua changamoto kwa njia ya mazungumzo badala ya migogoro.

Tunapochagua amani, tunachagua maendeleo, mshikamano na mustakabali bora wa jamii yetu.

Katika Manispaa ya Singida, Balozi wa amani Mariki James alizungumza kuhusu mada ya Uzalendo, akisisitiza misingi muhimu...
17/06/2026

Katika Manispaa ya Singida, Balozi wa amani Mariki James alizungumza kuhusu mada ya Uzalendo, akisisitiza misingi muhimu inayounda taifa lenye mshikamano na maendeleo. Misingi hiyo ni pamoja na kujitoa, uaminifu, uadilifu, kufanya kazi kwa bidii, na kuheshimu alama za Taifa.

Aliwahimiza vijana kutambua nafasi yao katika kuimarisha uzalendo kwa kutumia mitandao ya kijamii kwa uwajibikaji, kuwa walinzi wa amani na rasilimali za taifa, kujitolea, na kuwa wabunifu katika kuchangia maendeleo.

Alihitimisha kwa kuwasihi vijana kulinda na kuheshimu tunu za Taifa, kulinda rasilimali za nchi, kuwa na moyo wa kujitolea na uzalendo, na kuepuka vitendo vyote vya ukatili, uhalifu na ukanadamizaji wa aina yoyote.

17/06/2026

Amani ni utulivu wa nafsi na akili.
Katika mazungumzo yetu na vijana, kila mmoja ana mtazamo wake kuhusu maana ya amani, kwa wengine ni usalama, kwa wengine ni mshikamano, na kwa wengine ni hali ya kuwa na utulivu wa ndani bila hofu wala machafuko.

Lakini swali linabaki kwako: wewe je, amani ina maana gani kwako? 🤔

Tushirikishe mtazamo wako katika maoni, tuendelee kujifunza na kujenga uelewa wa pamoja kuhusu amani katika maisha yetu ya kila siku.

16/06/2026

Podcast yetu ya pili sasa ipo hewani! 🎙️
Tunaleta pamoja vijana mahiri katika masuala ya amani na usalama ili kushiriki maarifa, uzoefu na mitazamo yao kuhusu masuala muhimu yanayoathiri jamii zetu.

Hii ni nafasi ya kipekee ya kujifunza, kupata ‘madini’ ya uongozi, amani na ushirikishwaji wa vijana.

Kaa mkao wa kupata maarifa mapya na mazungumzo ya kina kutoka kwa vijana wanaoleta mabadiliko chanya.

Usikose kutazama episode nzima kwenye YouTube channel yetu ya The African Leadership Initiative for Impact.

10/06/2026
09/06/2026

This August at Kazimzumbwi Forest, Pwani Region for an immersive experience where youth connect, learn, and actively contribute to peace, leadership, and community building.

Don’t miss this chance to be part of a transformative journey that empowers young changemakers to create lasting impact.

Apply now before 11th July 2026 and invest in peace today!

🔗 bit.ly/Youth4PeaceCamp2026

06/06/2026

Kaa tayari kwa sehemu ya pili ya mjadala wa Podcast unaowakutanisha na na kuangazia nafasi ya vijana katika kudumisha amani.

Je Amani kwako inamaanisha nini na unafanya nini kuhakikisha kuna amani?

Tofauti zetu ni fursa muhimu katika kudumisha amani, haki, na umoja wa kitaifa. Kila mmoja wetu anapothamini utofauti wa...
03/06/2026

Tofauti zetu ni fursa muhimu katika kudumisha amani, haki, na umoja wa kitaifa.

Kila mmoja wetu anapothamini utofauti wa wengine, kuonyesha heshima, na kushirikiana kwa mshikamano, tunachangia katika jamii yenye mshikamano, usawa, na maendeleo endelevu.

Kauli hii inatufundisha kuwa kila hatua ndogo ya kuheshimu na kuthamini tofauti ni mchango wa kweli katika kuunda taifa lenye amani na mshikamano wa kudumu.

30/05/2026

Jukwaa la Kitaifa la Vijana, Amani na Usalama ni nafasi muhimu kwa vijana kushirikiana, kubadilishana mitazamo, na kujifunza mbinu bora za kuendeleza amani katika jamii.

Kupitia mazungumzo haya ya kina, vijana wanapata fursa ya kuelewa changamoto za usalama, kushiriki suluhisho bunifu, na kujenga uongozi unaolenga mshikamano na maendeleo endelevu.

Jukwaa hili linawahimiza vijana kuchukua nafasi ya uongozi wa amani, kudumisha haki, na kueneza mshikamano katika jamii zao, ikithibitisha kuwa kila sauti ya kijana ina thamani kubwa katika kuunda taifa lenye amani na usalama wa kudumu.

29/05/2026

Habari njema kwa vijana wabunifu!

Kambi ya Kitaifa ya Vijana, Amani na Usalama 2026 itafanyika Agosti, sambamba na maadhimisho ya Siku ya Vijana Duniani.

Kambi hii ni fursa ya kipekee kwa vijana kuungana, kubadilishana mawazo, na kuchangia kikamilifu katika kujenga utamaduni wa amani, ushirikiano, na uongozi1.

Usikose – jiandikishe kabla ya 11 Julai 2026 na uwe sehemu ya tukio la kipekee linalowapa nguvu viongozi vijana kuleta mabadiliko chanya katika jamii zao.

Tuwekeze katika amani na kusherehekea nguvu ya vijana pamoja!

Address

Dar Es Salaam

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Youth4PeaceAgenda Tanzania posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to Youth4PeaceAgenda Tanzania:

Share