great achievement in any society is the target of any organization in the world” “Positive achievement for the negative challenge”Safina Widows and Child Care Foundation (Sawichifo) has so many objectives in serving the community Safina ni makao ya kulelea watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi, yatima na watoto wa mitaani, makao haya yalianzishwa tarehe 6/2/2006 mwananyamala, wilaya ya kino
ndoni yakiwa na watoto wapatao kumi tano, kutokana na makazi kuwa finyu idadi ya watoto ilizidi kuongezeka na kufikia 25, mnamo mwaka 2007 makao yalihamia kitunda wilaya ya ilala kwa muda mfupi wa miezi miwili tu, baada ya hapo yalihamishiwa mbagala mnamo mwaka 2008 na idadi ya watoto ilizidi kuongezeka na kufikia watoto hamsini (50) na ilipofika mwaka 2009 makao yalipata usajili wa kudumu,
UKUSANYAJI WA WATOTO
Watoto wanaolelewa katika makao haya wametoka mikoa mbali mbali, kwa kuyataja machache:- Tabora, Morogoro, Pwani, Tanga, Musoma, Singida, Lindi na Dar es salaam,
Watoto wanaopokelewa ni wa jinsia zote wa k**e na wa kiume bila kujali dini, kabila wala kasoro za kimaumbile kwa ajili ya malezi, watoto hao ni kuanzia umri wa siku moja hadi miaka 12
UONGOZI WA KITUO;
1) ASHURA MOHAMED SAIDI:
Mama mlezi /mwenyekiti wa makao haya.
2) MBARAKA MOHAMED HASSANSHAH
Mweka hazina
3) SAIDI ATHUMANI MGOMBA
Katibu
ELIMU;
Watoto wote wanasoma kuanzia shule za awali, msingi na Sekondari,
Pia watoto huwa wanapata elimu za uhamasishaji kutoka asasi mbali mbali k**a vile:- Pasada, pathfinder na asasi za kiraia (civil organizations.) kuhusu matumizi ya madawa ya kulevya , uvutaji bangi, madhara ya sigara na matumizi ya mirungi na pia kujiepusha na magonjwa ya zinaa k**a vile ukimwi, bila kusahau usafi wa mazingira na mtoto kwa ujumla
MALENGO YA MAKAO
1) Kuboresha makao ya kulelea watoto kwa kujenga makao ya kudumu kuepuka kupanga,
2) Kuongeza idadi ya watoto na kufikia 200 kutoka idadi ya sasa ya watoto 50 waliokuwepo,
3) Na kuhakikisha kuwa ufanisi katika malezi unaongezeka. MATARAJIO
1) Makao yanalenga kuwalea watoto kwa kuwapatia haki zao za msingi kimalezi, k**a vile afya, lishe, mavazi, michezo, elimu na malazi
2) Kuhakikisha wanaomaliza elimu wanapatiwa stadi za kazi ili waweze kujiajiri wenyewe na kuanza maisha ya kujitegemea,
3) Kuendelea vipaji vya watoto watakaojitokeza kuwa na vipaji hivyo. MATATIZO
Matatizo yapo mengi katika makao
a) Ukosefu wa makazi ya kudumu,
b) Kutokuwa na bima ya afya kwa watoto,
c) Vifaa vya kusomea ,vitabu vya kusomea kutoka shule za msingi mpaka sekondari na madaftari imekuwa ni tatizo sugu pamoja na sare za shule kwani inahitajika kila mtoto awe na pea 4 za shule kuliko kutegemea pea moja tu wanazotumia kwa sasa, vitabu vya mafundisho ya dini vinahitajika,
d) Magodoro futi 6 kwa 3½, vitanda futi 6 kwa 3½, vinahitajika shuka, taulo na kandambili (sandals)
e) Chakula kuna uhaba wa chakula wa mara kwa mara kwa watoto
f) Kodi ya pango nalo ni tatizo sugu kwa sababu hatuna wafadhili wa kudumu kuweza kutulipia kodi
Kwa hayo machache tusingependa tuwachoshe tunawakaribisha wageni wetu tufurahi pia muendelee na moyo huo wa kutembelea makao haya mara kwa mara na kutusaidia katika malezi , mungu atakuwa pamoja nanyi
Asanteni karibuni sana.