Room to Read Tanzania

Room to Read Tanzania Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Room to Read Tanzania, Nonprofit Organization, Room to Read Tanzania/Country Office, Mlimani City Office Park, Block 5, Ground Floor, Sam Nujoma Road Ubungo, Dar es Salaam.

Room to Read is a global organization transforming the lives of millions of children in low-income communities by focusing on literacy and gender equality in education.

Jumamosi (Juni 6, 2026), tulishiri katika "Hafla ya Utoaji wa Zawadi kwa Washindi wa Shindano la Taifa la Stadi za Ufund...
10/06/2026

Jumamosi (Juni 6, 2026), tulishiri katika "Hafla ya Utoaji wa Zawadi kwa Washindi wa Shindano la Taifa la Stadi za Ufundishaji kwa Walimu wa Elimu ya Awali, Msingi na Sekondari." Hafla hiyo ilifanyika katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambapo walimu 35 kote nchini walitambuliwa kwa ubora na ubunifu wao katika ufundishaji. ilishiriki katika hafla hiyo ili kuunga mkono juhudi za Serikali za kuimarisha stadi za kusoma na kuandika.

Hafla hiyo iliandaliwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kupitia Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa elimu. Mgeni rasmi, Prof. Riziki Shemdoe (Mb), Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI, aliwahimiza walimu kutumia mbinu bunifu za ufundishaji na matumizi ya teknolojia ili kuwasaidia wanafunzi kukuza uwezo wa kufikiri kwa kina na kutatua changamoto, stadi ambazo ni muhimu katika karne ya 21.

Tunawapongeza washindi wote, juhudi zenu ni mwanga unaoangaza mustakabali wa elimu nchini.

Tunajivunia ushirikiano wetu na serikali na wadau wa elimu nchini katika kuimarisha ujifunzaji na kuhakikisha kila mtoto anajifunza, anakua na kustawi.

09/06/2026

Katika nchi 29, watoto milioni 60.3 wamepata stadi za msingi za kujifunza, na kazi inaendelea. Ripoti yetu ya mwaka 2025 inaonyesha jinsi mbinu zetu za kipekee zinavyotuwezesha kuongeza matokeo kwa miaka ijayo.
Fungua kiungo kusoma ripoti 👉 https://l1nq.com/qxht8yu

Jana tulihitimisha mafunzo ya siku 3 ya Msaada wa Kisaikolojia (Juni 1–3) kwa walimu waratibu wa mradi na walimu wakuu k...
04/06/2026

Jana tulihitimisha mafunzo ya siku 3 ya Msaada wa Kisaikolojia (Juni 1–3) kwa walimu waratibu wa mradi na walimu wakuu kutoka shule tatu za msingi za Manispaa ya Temeke zinazotekeleza mradi ambazo ni Mtoni Sabasaba, Azimio na Bwawani. Mafunzo hayo pia yalijumuisha Maafisa Elimu Kata kutoka kata husika, Mratibu wa Mradi wa Manispaa pamoja na Wahamasishaji Jamii wa Room to Read Tanzania.

Mafunzo haya yameimarisha uwezo wa washiriki kuwasaidia watoto wa k**e na wa wakiume walio katika mazingira hatarishi, si kielimu tu, bali hata kihisia. Pia washiriki wamepata mbinu za kujitunza na kujenga ustahimilivu ili kukabiliana vyema na msongo unaotokana na kazi.

Watoto wengi bado wanakabiliwa na vikwazo vinavyowazuia kushiriki kikamilifu katika elimu. Kupitia mafunzo endelevu k**a haya, walimu na viongozi wa shule wanajengewa uwezo wa kutengeneza mazingira salama na yenye msaada, na hivyo kuchochea mabadiliko ya kudumu katika jamii zao.

Elimu kuhusu hedhi ni hatua ya kuelekea usawa na afya bora.
01/06/2026

Elimu kuhusu hedhi ni hatua ya kuelekea usawa na afya bora.

Hedhi si chanzo cha kukosa masomo, jamii iondoe vikwazo vya hedhi kwa wasichana.
01/06/2026

Hedhi si chanzo cha kukosa masomo, jamii iondoe vikwazo vya hedhi kwa wasichana.

"Tukiwa tunasherehekea siku ya Kimataifa ya Hedhi Salama, ni muhimu jamii kutambua kwamba ukosefu wa vifaa vya kujistiri...
29/05/2026

"Tukiwa tunasherehekea siku ya Kimataifa ya Hedhi Salama, ni muhimu jamii kutambua kwamba ukosefu wa vifaa vya kujistiri au msaada wa msingi wakati wa hedhi haupaswi kuwa sababu ya mtoto wa k**e kukosa elimu.

Kwa pamoja, tushirikiane kujenga jamii inayowajali wasichana kwa kuhakikish wanapata mahitaji muhimu, msaada na mazingira salama kila wanapokuwa katika hedhi.

Hii itawasaidia kuepuka kukosa shule na kuwapa nafasi ya kutimiza ndoto zao."

Hadija Hassan, Meneja Mwandamizi, Mradi wa Usawa wa Kijinsia, Room to Read Tanzania

Hedhi ni jambo la asili, lakini bado wasichana wengi wanakabiliwa na unyanyapaa, ukimya na vikwazo vinavyoathiri kujiami...
28/05/2026

Hedhi ni jambo la asili, lakini bado wasichana wengi wanakabiliwa na unyanyapaa, ukimya na vikwazo vinavyoathiri kujiamini na hata elimu yao.

Kupitia elimu ya afya ya hedhi, stadi za maisha na mazungumzo, tunawasaidia wasichana kuelewa miili yao na kusimama imara bila aibu.

Kwa kuwashirikisha wazazi, walimu, jamii na shule; pamoja na kufanya kazi kwa karibu na wadau, tunajenga mazingira salama yanayowezesha wasichana kujifunza, kukua na kustawi —kwa sababu hakuna msichana anayepaswa kupoteza mustakabali wa maisha yake kwa sababu ya hedhi.

Africa is home to one of the world’s youngest and fastest-growing populations — and investing in foundational learning t...
28/05/2026

Africa is home to one of the world’s youngest and fastest-growing populations — and investing in foundational learning today is critical to preparing the continent’s future workforce for tomorrow.
In a new feature with Africa , Room to Read CEO Dr. Murali shares how literacy and life skills development can help unlock opportunity for millions of children across Africa and beyond.
Read the full article for more on Room to Read’s growing work across Africa: https://okt.to/Gwb4dZ

Africa is home to one of the world’s youngest and fastest-growing populations — and investing in foundational learning today is critical to preparing the continent’s future workforce for tomorrow.

In a new feature with Africa , Room to Read CEO Dr. Murali shares how literacy and life skills development can help unlock opportunity for millions of children across Africa and beyond.

Read the full article for more on Room to Read’s growing work across Africa: https://okt.to/Gwb4dZ

Jana Room to Read Tanzania, kwa kushirikiana na Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) imezindua Usambazaji wa Vitabu vya Kiada...
13/05/2026

Jana Room to Read Tanzania, kwa kushirikiana na Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) imezindua Usambazaji wa Vitabu vya Kiada na Ziada kwa ajili ya utekelezaji wa Mradi wa Usomaji unaojulikana k**a "Accelearete 2.0" unaotekelezwa na Room to Read Tanzania katika Wilaya ya Kilosa.

Uzinduzi huu ulifanyika katika Shule ya Msingi Madaraka na uliongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa TET Dkt. Aneth Komba, mbele ya watumishi wa Room to Read Tanzania wakiongozwa na Mkurugenzi Mkaazi, Bi. Joan‑Ndaambuyo Minja, pamoja na maafisa wa elimu wa ngazi ya mkoa na wilaya.

Akizungumza wakati wa tukio hilo, Dkt. Komba alisisitiza umuhimu wa kuimarisha ufundishaji wa kusoma na kuandika katika shule za serikali, huku Bi. Minja akisisitiza kuwa usambazaji wa vitabu hivyo ni mchango wa katika kampeni ya TET ya "Kitabu Kimoja, Mwanafunzi Mmoja."

Zaidi ya vitabu 127,000 vitasambazwa katika shule zote za msingi za serikali 178 za Wilaya ya Kilosa na vinatarajiwa kunufaisha zaidi ya wanafunzi 105,000 katika shule hizo.

Mradi wa Usomaji wa "Accelerate 2.0" ni mpango wa majaribio wa miaka mitatu, unaolenga kutoa mfano wa gharama nafuu na unaoweza kupanuliwa ili kuboresha ujuzi wa kusoma nchini kote.

Kutana na Mwalimu Delphina, mwalimu shupavu wa Darasa la Pili ambaye kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita amebadilisha...
11/05/2026

Kutana na Mwalimu Delphina, mwalimu shupavu wa Darasa la Pili ambaye kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita amebadilisha namna wanafunzi wanavyosoma na kuandika.

Kupitia kujitolea kwake, wanafunzi sasa wanatambua kwa ujasiri sauti, herufi, silabi, sentensi na hata hadithi fupi—wanazosoma kutoka ubaoni au kwenye vitabu vya wanafunzi. Mwanzo walikuwa na changamoto ya kuandika vizuri, lakini kupitia mazoezi ya mara kwa mara, maelekezo ya vitendo na hamasa, wanafunzi wake sasa wanaweza kuandika kwa ufasaha.

Mwalimu Delphina huwapa motisha wanafunzi wake kwa njia za ubunifu zifuatazo

- 🎖 Kuwazawadia wanafunzi waliopiga hatua kwa kuwapa nafasi ya kuandikia kalamu za wino badala ya penseli
- 🤝 Kuchanganya wanafunzi walioimarika katika ujifunzaji na wale wanaohitaji msaada ili kuimarisha ujifunzaji wa wenzao
- đź“– Kutumia maktaba ya shule kwa usomaji wa pamoja, kuwapa nafasi wanafunzi wake kujisomea maktaba wakati wa mapumziko na kuazima vitabu

Maktaba ya shule imekuwa kitovu cha udadisi na ukuaji. Wanafunzi hupata nafasi ya kusoma mara kwa mara, kujenga tabia ya usomaji na kufurahia hadithi. Kupitia mazoezi ya kila siku, ufuatiliaji wa karibu na ziara za msaada wa kitaalamu kila mwezi kutoka Room to Read Tanzania, matokeo yanaonekana wazi—wanafunzi hawa wachanga wanastawi na kuimarika!

Address

Room To Read Tanzania/Country Office, Mlimani City Office Park, Block 5, Ground Floor, Sam Nujoma Road Ubungo
Dar Es Salaam

Opening Hours

Monday 08:00 - 17:00
Tuesday 08:00 - 17:00
Wednesday 08:00 - 17:00
Thursday 08:00 - 17:00
Friday 08:00 - 17:00

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Room to Read Tanzania posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share